Steji ya kutengeneza bidhaa inayoweza kuchukua mda mrefu inataka mtaji na sio njaa kama hizi za kutengeneza kemikali moja pombe tofauti na madawa tofauti.
Kuna makala nilipata kuangalia jinsi ya kampuni inayotengeneza pilipili aka chachandu kuanza uvunwaji na kuvundikwa kwenye mapipa ili ipate ubore na utofauti kwa miaka mitatu.
Nyengine utengenezaji wa kinywaji hennessy na jack daniel zinavotengenezwa kwa mda mrefu zaidi.
Kampuni kama apple nao wamekuwa wakifanya hivo kwenye vifaa vinavotumia umeme.
Ukiangalia bidhaa nyingi ziwe za vyakula,nguo,madawa,vifaa vya majumbani vinavochukua mda kutengenezwa vinakuwa bora ukilinganisha vile vinatengenezwa haraka haraka.