Unaweza Vipi Kujenga Uaminifu Kwenye Biashara, How Can You Building a Trust in Business

Unaweza Vipi Kujenga Uaminifu Kwenye Biashara, How Can You Building a Trust in Business

King Loto

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2018
Posts
1,581
Reaction score
1,357
Helo JF members
Greatings to you all, Kama title ilivyo hapo.
Ebu Leo tufafanue kidogo na tulipe uzito hili neno linaloitwa 'UAMINIFU' whitemens called it Trust.... Tuongelee Uaminifu hasa pale linapotumika kwenye namna au muktadha wa kibiashara.
Maswali ya kujiuliza ni haya ambayo Mimi na wewe saa nyingine kwa sababu ya ubinadamu wetu tumekuwa na tabia ya kusahau nini tufanye juu ya Kuaminiana...

Maswali ya kujiuliza ni ???
1. Je Kuna Umuhimu gani wa kuwa waaminifu tunapo fanya biashara? Au upo Umuhimu wowote mkubwa wa kuenenda hivo...?

2. Unadhani ni watu gani wa kuwajengea uaminifu kwenye biashara yako?

3. Ni wapi uliwahi kuona mtu au wewe umefanikiwa kwa sababu ya uaminifu?

4. Ni fursa ngapi tunashindwa kufanya sababu ya kutoaminiana?

5. Unafikiri ni kwa jinsi gani unaweza ukajenga uaminifu kwa Karne hii hasa kwenye biashara na ukafanikiwa.

6. Uaminifu unapokuja kwenye biashara ni zaidi ya urafiki, undugu wa damu, na usiri baina ya mlioaminiana. Unafikiri kwa Nini?

7. Wewe unazani ni kwa nini walio fanikiwa na kujulikana wameweza kuwa hapo, Unazani walikuwa na Mtaji mkubwa wa pesa?

8. Wewe Unazani ili uanze biashara lazima uwe na Mtaji pesa na pia Mtaji Ujuzi Pekee yake ?

9. Kwani wewe unaweza kukaa mahali ukafikiria kuwa Mtaji wa pesa au cash dola ndiyo jibu au mwafaka wa kuanza biashara?

8. Ebu fikiri ni namna gani Mtaji wa pesa unaweza kubwebwa na Mtaji mwingine na ukabebeka yaani covered up, ni jinsi gani unaweza kufanya maujanja.

Tujiulize haya maswali pengine ni mepesi au marahisi ila nachotaka tuongelee hapo ni namna gani ya kujenga uaminifu na kuaminika. How to build a trust

Mi naweza kuita Uaminifu ni Mtaji mkubwa wa biashara wapo wengi walio tumia huo Mtaji kwa nguvu na bidii na wakafanikiwa na pengine hadi Leo ndiyo wanachofanya japo wana milioni dola zao zimepozi kwa benki.... $$$$$ Sasa wewe ndugu endelea kufikiria ni mpaka upate milioni 5, milioni 7, milioni 10 ndio uanze biashara. Au Endelea kuilamu serikali.
Unapoona fursa ya biashara inakuja na huna pesa tumia maujanja yote kuona ni vipi unaweza kuonekana mwaminifu.... Ukishindwa hapo ndio basi pesa zinapass like a shadow
.

Mwisho fikiria wewe mwenyewe mambo yanayo haribu uaminifu na jibu la kwanza lazima litakuwa ni,??? Tabia yako yaani wewe mwenyewe mwenendo wako.
1. Kutokujiamini.
2. Uongo.
3. Kuwa na tamaa. Na vingi vinavyo fanana na hivyo...

Kwa dunia ya Sasa hivi kuaminiwa sio rahisi lakini tumia akili sana uaminiwe.

Imeandikwa na Mimi......E. N 🔨🔨🚫🚫🚫🚫🚫 No fake zone
 
Back
Top Bottom