Unawezaje kudhibiti mdomo wa mtu mzima usikae wazi muda wote?

Hapana mimi sina utaalamu wala experience ya hilo tatizo ila nimecheka tu baada ya kukumbuka rafiki yangu wa utotoni alikuwa na tatizo hilo.
Tuna mcheza mpira naona ana hilo tatizo
 
Kichwa kimejitosheleza.

Na je hiyo ni "unconscious"/involuntary au ipo more psychological?
View attachment 3257527

Kushindwa kufunga mdomo ni tatizo ambalo linaweza kusababishwa na:

-udhaifu wa misuli ya kufunga na kufungua mdomo

-tatizo la upumuaji mfano pua kuziba kutokana uvimbe, mafua nk hulazimisha mtu kupumua kwa mdomo hivyo kuacha mdomo wazi muda wote

-mpangilio mbaya wa meno hasa meno ya juu yanapojitokeza mbele zaidi na hivyo kupisha na yale ya chini

-kupooza kwa mshipa wa fahamu wa uso/mdomo (facial nerve palysis)

-muundo/mpangilio mbaya wa mifupa ya uso

-nk

Ili kumsaidia mwenye tatizo hilo ni muhimu akaonane na daktari bingwa wa kinywa na meno.

Kila la kheri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…