Unawezaje kuishi na mpenzi asiyependa kukosolewa pale anapokosea?

Unawezaje kuishi na mpenzi asiyependa kukosolewa pale anapokosea?

Kifaru86

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2017
Posts
1,734
Reaction score
3,822
Kuna aina flani ya watu mkiwa katika mahusiano hujiona ni watu ambao wako very perfect katika mahusiano ni watu hujiona wapo right kwa kila jambo wanalolifanya na huwa hawapendagi kupingwa na hata ndani ya mahusiano kwa kila jambo hujiona wao ndio final say.

Lakini watu wa aina hii inapotokea siku unamuelekeza jambo flani sio zuri au anavyofanya kitu fulani unamuelekeza amekosea hupandwa hasira hadi wanapaniki, wanakuwa wakali mnoo, wanajiona kama vile hawakustaili kukosolewa.

Je, shida inakuwa nini?
 
Zuli - Zuri

Watu wengi hawajui tabia za kawaida za kibinadamu; hakuna mkamilifu kinachotakiwa kila mmoja amstahi mwenziwe , ukijua mpenzi wangu hataki kukosolewa/mjuaji mno unaishi nae kama alivyo mkosoe kwa vitendo sio maneno.

Watu ukiwajua hupati tabu, la! kama hutaweza unamuacha atapata wa kufanana nae usitegemee kwamba kuna siku utabadili tabia ya mtu mzima.
 
Ni mwanamke?[emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji27][emoji27][emoji27][emoji1][emoji1][emoji1787][emoji16][emoji16][emoji3526][emoji35][emoji848][emoji28][emoji30]

Dalili moja ya kujua unaenda kupata shida kwenye maisha yako ya ndoa ni kukubali kumuoa/kuolewa na mtu asiyekubali kukosolewa niamini mimi usimvumilie huyo piga chini tu.Kwa shauri huu naomba unilipe kabisa maana sio ushauri mdogo.

Ila km una good sense of humor unaweza kumuoa lakini sharti lake ni moja tu ili mdumu kila anapokosea ingiza utani flani hivi wa kumkosoa mtu bila kumuuzi ni wachache sana wanakipaji hiki kama huna hicho kipaji USIOE HUYO unadumbukia shimoni.

Wife ana huo udhaifu kiasi chake ila mwamba hapa namkosoaga mpk mwenyewe anashindwa kuelewa km kakoselewa anabaki kucheka tu.Saivi hata nikimkosoa sio km zamani anaweza kuvumilia vumilia kama huna asili ya ujinga ujinga na ucheshi achana nae km una hiyo asili basi ingiza utani unapomkosoa
 
Mara nyingi watu wa aina hiyo ni wale wenye uwezo mdogo mno kiakili, hujihami kwa kuhisi kukosolewa ni kudharauliwa.
Ni ngumu kuielewa hii kwa haraka, ipo pia nafasi ya kuwa huyo mtu kwa mtazamo wake anakuzidi wewe kila kitu akili na etc. pia haupo katika muktadha wa kweli katika maisha yake mfano.. kiburudisho, kifaa tu cha jambo fulani. Mila, desturi, kurithi, jamii atokayo etc.
 
Hiyo inaitwa absolute advantages ambayo yule anaepedwa zaidi huitumia kama silaha ya kumuendesha anavyotaka yule aliyependa asiwe na sauti.

Haya mambo hujitokeza pale unapoingia ktk mahusiano na mtu ambaye hajiamini.
 
Back
Top Bottom