Hisa ni nini tafadhali? Na ni namna gani naweza kununua hizo hisa na ninazinunua wapi?
Fikiria Kwa Mfano Tunaanzisha Kampuni Watu Watatu, Mtaji wa Kampuni ni Shilingi Milioni Moja. Bwana A Anachangia Laki Tano ya Mtaji Sawa na 50%, Bwana B Anachangia Laki Mbili na Nusu Sawa na 25 na Bwana C Anachangia Laki Mbili na Nusu Sawa na 25%.
Sasa, Ili Kila Mtu Apate Mgawanyo Sawa wa Faida Unaoendana Kiasi Alichochangia.. Ndio Kila Mtu Anakua na Document Maalum Inayoonyesha Kiasi cha Umiliki Wake Kwenye Kampuni, Document Hiyo Huitwa HISA.
Ina Maana, Kampuni Ikifanya Biashara na Ikipata Faida ya Milioni Mbili, Bwana A Anayemiliki 50 ya Hisa Atapata Gawio la Shilingi Milioni Moja, BwanaB na Bwana C Wote Wanamiliki Hisa za 25% Kila Mmoja Atapata Laki Tano.
Gawio Ndio Huitwa Dividend.
Sasa Hizo Hisa Katika Hatua ya Kwanza Huitwa Primary Market. Kampuni Ikiingia Kwenye Soko la Hisa (Dar es Salaam Stock Exchange Market -DSE) Wale Wanahisa wa Mwanzo Wana Uwezo wa Kuuza Hisa Zao. Mfano Bwana A Anaweza Kuamua Kuuza Asilimia 25 za Hisa Anazomiliki Kwenye Kampuni. Na Hata Wewe Unaweza Kwenda Kununua Vipande na Ukawa Sehemu ya Wamiliki au Wanahisa wa Kampuni Japo Hukushiriki Kipindi cha Kuanzisha Kampuni. Inategemea na Bei Husika Lakini Kipande Chaweza Kuanzia Shiligi Mia Tatu au Vinginevyo.Hiyo Ndio Inakua Secondary Market.Gawio Hufanyika Mwakani na Bila Shaka Ushawahi Kusoma Matangazo ya Mkutano wa Wanahisa wa Kampuni Fulani.
Hope Utapata Picha Mkuu, Nimejaribu Kurahisisha Sana Kwa Ajili ya Uelewa. Wataalam Watakufafanulia Zaidi.