Unawezaje kuzijua spark plug mbovu?

Unawezaje kuzijua spark plug mbovu?

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
3,381
Reaction score
9,744
Kuna vitu kadhaa vinavyokuwezesha useme spark plug ni mbovu au lah.

IMG_20220604_114826.jpg

Hebu tuziangalie hapa haraka haraka.

1. Nyufa kwenye Insulator

Ukiikuta spark plug ina nyufa kwenye Insulator ibadilishe.
Spark-plug-torquing.jpg

Spark ikiwa na cracks kwenye Insulator ina maana kuna muda inaweza kuleak voltage na kuignite kabla ya kufika mwisho wa central electrode. Hivyo haitochoma mafuta vizuri.

Mara nyingi spark plug huweka nyufa sababu ya kukazwa sana [Overtightening].

2. Kumeguka au kuisha kwa Insulator tip.

Hii mara nyingi hutokea kama kuna preignition yaani mafuta kuungua kabla ya spark plug kutema cheche. Na hii hutokea endapo joto linakuwa na kali sana kwenye combustion chamber.
Photograph-of-a-Broken-Starting-Tip-in-the-Plug.png

3. Kuisha kwa Central na/au Side electrode.

Kama Central au side electrode ikilika basi itapelekea gap kuwa kubwa na hivi ndio huwa spark plug zinaisha katika matumizi ya kawaida.

wornsparkplug.png

Kujua kama gap limeongezeka au limepungua ni mpaka uwe na proper tool ya kufanya hivyo. Mara nyingi gap huwa ni dogo sana around 1mm hivyo adjustement ndogo sana ya gap inaweza kuathiri hizo plug.

Ukiwa na gapping tool kama hii yangu unaweza kujua kama spark plug zina gap kubwa au dogo kuliko linalotakiwa.

LMC_20220604_122749185_8.4.300.NIGHT.jpg

LMC_20220604_122826597_8.4.300.NIGHT.jpg

Kuhusu spark plug mbovu naishia hapo.

Nyongeza

Corona Discharge Stain

pulled_plug.jpeg

Hiki si kitu kigeni kwa wengi mliowahi kubadilisha plug.

Wengi wakiona spark plug ina rangi hiyo huwa wanasema ni mbovu hata kama sehemu zingine zote ipo fresh. Lakini kiuhalisia plug kuwa hivyo wala siyo ubovu.

Hizo ni deposit tu, Zinaweza kuwa deposit za Oil kama oil inavuja, additives zilizopo kwenye mafuta au particles zingine ambazo huvutwa hapo sababu ya magnetic effect inayozalishwa na high current inayopita ndani ya Central electrode.

Pia sijazungumzia vitu vingine kama spark plug kuwa na Oil, Carbon deposit n.k. sababu vingi ni vitu ambavyo kama matatizo fulani kwenye gari yakirekebishwa hizo deposit hazitaendelea kuonekana kwenye spark plugs.

Ninayo pia spark tester

LMC_20220603_171800079_8.4.300.NIGHT.jpg

Hii ni moja wapo ya best tool ambayo inaweza kutumika kuidentify matatizo ya mfumo wa ignition hasa ignition coils, spark plug wires na vitu vingine kwenye mfumo wa ignition with exception ya spark plug.

Hiyo inaweza kuidentify kama inatoa voltage inayotakiwa au lah.

DIYers

Fine, Umeamua kujibadilishia spark plug mwenyewe, basi usizirushe kama unatupa taka shimoni.

Unaporusha plug kwenye shimo, Side electrode inabend na hivyo kupelekea gap kuwa dogo.

Unaweza ukanunua plug mpya. The moment unamaliza kufunga, gari ikawa na misi mpaka ukahisi umepigwa hizo plug.

Lakini kumbe shida ni wewe mwenyewe.

Mwisho.

1. Tunafanya Diagnosis na kurekebisha gari aina yotote.

Engine Diagnosis Tsh. 30,000/=
Full Systems Tsh. 50,000/=

2. Kuuza GPS trackers na Security Systems zingine.

3. Ushauri.

4. Check up kwa wanaonunua magari n.k.

Tupo Dar, Magomeni Mwembechai.

+255 621 221 606

Karibu sana.
 
Hivi kwa kufanya engine diagnosis unaweza kungundua kuwa tatizo ni sprk plugs zina shida au inakupa general indications tu...

Ni ngumu kufanya diagnosis na kujua kama spark plug zina shida kwa sababu spark plug hazina feedback loop ya kwenda kwenye ECU hivyo haziwezi kukupa code ya moja kwa moja.

Unless kwa Live data ambako ignition na fuel huwa zinaleta data moja hivyo inakuwa kazi ya kuchambua kama ni mafuta au spark. Air huwa inakuwa na data ya peke yake.
 
Asante kwa elimu hii,nina maswali kadhaa;

1.Ni dalili zipi kwenye gari zinaashiria Spark plug zimechoka(mbovu) na zinahitaji kubadilishwa?

2.Kwa uzoefu wako kuna uwezekano katika Plug 4 (mfano) za gari yako zilizokufa zikawa 2 au moja na ukabadili zilizo mbovu na zingine ukaacha?au ni lazima ubadili zote hata kama zingine ni nzima? au huwa zina tabia ya kufa zote?

3.Lazima fundi akague plug?Kama naweza kufikia zilipo siwezi kufungua nikakagua?
 
Kwa mjep warning [emoji3544] ya check engine inaweza kuwaka

Lakini kama gari lako unaendesha siku zote utanotice
-ku miss
-kuishiwa nguvu
-kuchelewa kubadili gia
-mlio wa engine kubadilika na kutoa moshi mweusi

Japo hizo dalili sio specific tu kwa plug

Lkn piaa nashauri kubadili zote kwa pamoja zinakaa sana kuliko kubadili moja moja.

Hata we unaweza kukagua inategemea na engine ya gari lako kikubwa ni ujue jinsi ya kufungua zile plug maana zina spana maalum.kama huna uzoefu acha nenda kwa fundi kagua nae
 
Ok, asante kwa ufafanuzi
 
Back
Top Bottom