Unawezaje kwenda kwenye ATM kutoa pesa yako halafu uisahau hapo hapo?

Unawezaje kwenda kwenye ATM kutoa pesa yako halafu uisahau hapo hapo?

sifi leo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
5,182
Reaction score
8,948
Sitaki kupoteza muda wenu ni hivi!

Jana majira ya saa mbili za usiku nilifika kwenye ofisi za NMB maeneo ya Himo pale kwenye ATM Kwa lengo kutoa kapesa kidogo Kwa lengo la kununua KITOCHI cha Konyagi pale Mombasa Highway.

Nilishangaa kuingiza kadi kwenye ATM na kutoa pesa Ile napapasa macho nakuta kiasi cha shilingi elfu Kumi kimeachwa hapo tunapowekaga kadi tunapokuwa tunahesabu pesa hasa pale tunapo toaga mzigo mkubwa.

Kilichonishangaza kama sio ugonjwa wa Akili mtu unawezaje kwenda kwenye ATM kutoa pesa, utoe pesa Yako halafu uisahau hapo hapo ulipoitolea uondoke na kadi yako?

Jamani matatizo ya ugonjwa wa Akili ni makubwa na yanazidi kujitokezaa. Ninawasihi wenye mamlaka waache kuwasimanga vijana na kuwasema ovyo Ili janga la kitaifa watu wanaumwa.
 
Afya ya akili ni nini?

Ni hali ya kuwa sawa kiakili na kisaikolojia au kutokuwepo kabisa kwa usumbufu wa akili ya mtu, mfano msongo wa mawazo.

Ni hali ya kuwa na mawazo chanya, kuwa sawa kijamii na kisaikolojia na kuweza kuchangia katika utendaji wako wa kila siku na uwezo wa kuridhisha wa kimawazo na kitabia.

Huhusisha uwezo wa mtu kufurahia maisha na kutengeneza mlingano baina ya shughuli zako kimaisha pamoja na jitihada zako kufikia uwiano mzuri kisaikolojia, kutoka kwenye msongo utokanao na magonjwa, misiba na shida mbali mbali.

Pia ni uwezo wa mtu kuishi katika mabadilko mbalimbali ya kimaisha na kufanyia kazi changamoto mbalimbali kimaisha.

Uwezo wa mtu kuwa timamu kiakili huhusisha mtu kuwez kutatua matatizo mbalimbal yanayomkabili yahusishayo msongo wa mawazo katika maisha, shuguli za uzalishaji na mchango wa mtu husika katika jamii.

Afya ya akili huhusisha…..”ustawi wa akili, kujitambua kwa ufanisi, uhuru, umahiri, utegemezi wa ulimwengu, na kujitambua kwa uwezo wa kiakili na kihemko, kati ya wengine.”

Ustawi wa mtu ni uwezo, kukabiliana na mikazo ya kawaida ya maisha, kazi yenye tija na mchango kwa jamii yao.

Tofauti za kitamaduni, tathmini ya kujifanya, na nadharia za kitaalam zinazoshindana zote zinaathiri jinsi mtu anafafanua “afya ya akili”.

Watu wenye afya bora ya akili wanaweza pia kuwa na magonjwa ya akili, na watu ambao hawana ugonjwa wa akili pia wanaweza kuwa na afya mbaya ya kiakili.

Chanzo: https://www.mht.care/nini-maana-ya-afya-ya-akili-afyayaakili/
 
Bila shaka wewe ndio una ugonjwa wa akili coz umehukumu bila kujua nini hasa kilichotokea. Kwenye ATM sometimes hela inaweza ikachelewa kutoka, so muhusika anaweza kuamua kuondoka, kisha hela ikatoka, muhusika akienda kulalamika Benki wanakukamata kirahisi sana tu na utarudisha hilo hela au itakatwa kwenye Account yako.
 
Bila shaka wewe ndio una ugonjwa wa akili coz umehukumu bila kujua nini hasa kilichotokea,kwenye ATM sometimes hela inaweza ikachelewa kutoka,so muhusika anaweza kuamua kuondoka,kisha hela ikatoka,muhusika akienda kulalamika Benki wanakukamata kirahisi sana tu na utarudisha hilo hela au itakatwa kwenye Account yako.
Nilimshauri mama yako akurudishe shule akagoma,sijakwambia pesa ilibakia pale kwenye kale ka njia ni kuwa iliwekwa juu kabisa mean juu
 
Bila shaka wewe ndio una ugonjwa wa akili coz umehukumu bila kujua nini hasa kilichotokea,kwenye ATM sometimes hela inaweza ikachelewa kutoka,so muhusika anaweza kuamua kuondoka,kisha hela ikatoka,muhusika akienda kulalamika Benki wanakukamata kirahisi sana tu na utarudisha hilo hela au itakatwa kwenye Account yako.
1-Hela kuchelewa kutoka YES.
2-Kumkata kwenye akaunti bila yeye NO.
3-Kulazimishwa kulipa YES.
 
Nilimshauri mama yako akurudishe shule akagoma,sijakwambia pesa ilibakia pale kwenye kale ka njia ni kuwa iliwekwa juu kabisa mean juu
Binti soma ulichokiandika,kwa comment hiyo unaonekana ni mtu wa hovyo sana,uliyepata malezi ya hovyo kabisa,ndio maana ki elfu kumi tu kinakufanya mpaka umekuja kufungua thd JF.
 
Rank ya nchi zenye wananchi wasiokuwa na furaha Tz inashika ngapi
 
Sitaki kupoteza muda wenu ni hivi!

Jana majira ya saa mbili za usiku nilifika kwenye ofisi za NMB maeneo ya Himo pale kwenye ATM Kwa lengo kutoa kapesa kidogo Kwa lengo la kununua KITOCHI Cha konyagi pale Mombasa Highway. Nilishangaa kuingiza kadi kwenye ATM na kutoa pesa Ile napapasa macho nakuta kiasi Cha shilingi elf Kumi kimeachwa hapo tunapowekaga kadi tunapokuwa tunahesabu pesa hasa pale tunapo toaga mzigo mkubwa

Kilichonishangaza kama sio ugonjwa wa Akili mtu unawezaje kwenda kwenye ATM kutoa pesa, utoe pesa Yako halafu uisahau hapo hapo ulipo itolea uondoke na kadi yako?

Jamani matatizo ya ugonjwa wa Akili ni makubwa na yanazidi kujitokezaa Nina wasihii wenye mamlaka waache kuwasimanga vijana na kuwasema hovyo Ili janga la kitaifa watu wanaumwa
Kusahau na ugonjwa wa akili kwani ni kitu kimoja?

Unapotoa hela kwenye ATM, Card yako hupaswi kuweke kwenye eneo lolote la kwenye hiyo mashine zaid ya mfukoni.
 
Unapataje AFYA ya Akili, ili Hali unadaiwa namna hii?

Kanisani.
1. unadaiwa Fungu la kumi
2. Ujenzi wa Kanisa.
3. Kumnunulia gari Mtumishi.
4. Ujenzi nyumba ya Pastor.
5. Mchango kwa wasiojiweza.

Serikalini.
1. TRA
2: TOZO.
3: Leseni ya biashara.
4: Bill ya MAJI
5: Bill ya umeme
6:Tozo ya usafi eneo la biashara.
7: Tozo ya usafi eneo la makazi.
8: Kodi ya Pango eneo la Biashara.
9:

Kijamii.
1: Michango ya harusi, kitchen party, send-off, birthday nk.
2: michango ya misiba.
3: Madeni ya Vicoba/Benk
4: Michango ya ukoo
5: Madeni kwa MANGI.
6: Ada/ michango ya watoto shuleni.

Maisha yenyewe Sasa;
Mafuta Bei juu.
Unga Bei juu
Mchele Bei juu
Maharage Bei juu
Mbolea Bei juu
Nyama Bei juu
Sabuni Bei juu
Maji Bei juu.........nk

Hapa ukiwa na AFYA ya Akili, juwa wewe huna Akili

Copy and paste from another source.
 
Back
Top Bottom