Unayafahamu madhara kiafya ya kuazimana earphone?

Unayafahamu madhara kiafya ya kuazimana earphone?

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Kama kawaida yetu sisi wa Tanzania tunapendana na Kujaliana hivyo mtu anapoazima kitu tunampatia anatumia na kisha anarudisha na wewe unaendelea kutumia.

Wengi huazimana Earphone kazini, kwenye michezo na sehemu nyingine kama hizo.

Wengine huazimana Nguo, Viatu, hereni, Na kadhalika.

Wataalamu wa Afya wameonya kitendo hicho kuwa si salama kiafya.

Kwa upande wa Earphones wataalamu wa Afya wanaeleza kuwa kitendo cha kushare earphone kinaeneza fangasi kutoka kwa mtu mwenye tatizo hilo kwenda kwa mwingine.

Tunapaswa kuwa makini wakati wote.
 
Uchoyo tu huo hakuna lolote, hizo nguo za mitumba tunazovaa ipo tofauti gani na kuazimana
 
Back
Top Bottom