Anna Meleiya Mbise
New Member
- Sep 7, 2022
- 3
- 0
Jina la Shairi: Undugu Wetu Matatani
Jina la Mtunzi: Anna Meleiya Mbise
1.Waungwana nauliza, twaishije duniani,
Wanadamu twashangaza, zaniwasha zangu mboni,
Undugu tunapoteza, tumekuwa hayawani,
Tumeshatokwa imani, twaishi bora liende.
2.Kwa sasa tumetengana, hatupo kama zamani,
Njiani tunapitana, tadhani hatujuani,
Misaada kupeana, ishakuwa mtihani,
Tumeshatokwa imani, twashangaza wanadamu.
3.Hasa linalo niuma, ni hili lilo hewani,
Mtu akipatwa homa, ndugu hatuonekani,
Sote tunarudi nyuma, si ndugu wala jirani,
Nani amepeperusha, ule wetu uungwana.
4. Hakuna wakuthubutu, kujitolea hisani,
Kidonge cha buku tatu, anakosa mdhamini,
Mifuko eti mibutu, kauli zetu vinywani,
Twasahau ya wahenga, kuwa wema hauozi.
5.Hajabu akifariki, hufurika wahisani,
Watao funga miziki, na vyungu tele jikoni,
Sanduku halibebeki, limechongwa kwa thamani,
Si sare si manukato, hakika ni maigizo.
6.Marumaru kaburini, huwekwa ya kazi gani,
Keshatoka duniani, hatotoa shukurani,
Biriani msibani, mhusika halioni,
Kila kitu kwa kadiri, undugu utu kulinda.
7.Ninapo hisi kuchoka, mwaliko wa harusini,
Kadi zinapotufika, tunafanya ushindani,
Fedha zinavyotutoka, malaki mamilioni,
Nguvu shereheni, umwa ukose mteja.
8. Tusijotoe akili, kusema tumesahau
Himizo kila mahali, upendo kutosahau
Jamii toka awali, misikiti madhabau
Ililiweka bayana, ngao yetu ni undugu
9.Tubadili mtazamo, tutendeane hisani,
Duniani tungalimo, kwenye kheri na shidani,
Hili nalo kubwa somo, tuliweke akilini,
Undugu tuudumishe, Maamuma apendezwa.

Upvote
0