'Unela': Ichungulie biashara hii

The August

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2018
Posts
1,080
Reaction score
2,026
Habari ya usiku wana JF!

Nataka kushare kile nilichojifunza katika msimu huu wangu wa kwanza wa biashara ya kuchakata mkonge na kutoa nyuzi za katani (wasukuma wanaita Unela).

Kwanza nikiri biashara hii niliianza nikiwa na mwanga mdogo sana lakini niliongozwa na imani yangu kuwa 'ardhi haimtupi mtu'.

Mwaka huu mwezi june nilimtembelea ndugu yangu wilayani kishapu. Katika connections nikabahatika kuonana na bwana mmoja ananunua nyuzi za katani. Ilinivutia na kuamua ngoja nitajaribu kidogo kidogo. Kikubwa kwake nilijua bei ananunua ni sh 1,300 kwa kilo na alinihakikishia ununuzi ni guarantee ( na hivyo nikapata nguvu kuwa soko lipo). Nikaamua sbb msimu wa kilimo tumemaliza na mpunga tumehifadhi ndani walau kwa hii miezi michache ya kiangazi nijaribu kuifanya kazi hii

Hivyo nikajikuta ninahitaji kupata vitu vitatu.

1. mashamba yenyewe ya mkonge.
2. Mashine ya 'kunela'.
3. Wafanyakazi.

1. Mashine

Mashine ilinipa changamoto sana sbb niliwaona watu wa SIDO shinyanga (kwa kweli wakawa wababaishaji sana), hatimaye nikapata kwa mtu kunikodishia kwa bei ya sh 350,000/- kutoka mkoani morogoro. Ilinilazimu kufanya marekebisho fulani sbb ilikuwa imekaa ndani muda kidogo na ni disel engine.

2. Mashamba.

Sbb ya ugeni wa kazi eneo hili lilinipa tabu kidogo. Maeneo mengi ya usukumani mkonge wanapanda kama mipaka ya mashamba. Hivyo kukodisha mashamba hayo ilibidi mtembee sana kuhesabiana urefu wa eneo na kisha mnakubaliana bei gani mnalipa (magadala). Yapo maeneo tuliyokodi kwa ef 40, ef 50 na mengine laki 1.

3. Wafanyakazi

Nashukuru sikuhangaika sana kuwapata wafanyakazi. Hawa niliwapatia wilayani kishapu na ilihitajika team ya watu wa 4 hadi 5. Shida kubwa ni kudeal na watu. Hivyo ilijikuta ninabadili watu hawa mara kwa mara. Hivyo inakugharimu nauli, wengine unawatumia lakini wanazama mitini. Pia inahitaji uwalishe na kuwakodishia nyumba. Chakula kikuu ilikua ni ugali wa mtama, michembe, dagaa na majani ya maboga yaliyokaushwa( ukiwafuata watakavyo watataka pilau na kuku kambini) but siku moja moja tulibadili diet.

Kambi na kazi.

Kazi hii mara yingi huanza 12 asubuhi hapa wanakatakata hadi saa 4, kisha chai, na wanaanza kuzikusanya na kuzirundika hadi mida ya saa 7. Wanaingia kula na kupumzika. Saa 1 jioni wanaanza kuzichuna hadi mida ya saa 6 usiku. Wanafanya usiku sbb ya kupunguza kuwasha. Kisha wanalala hadi saa 12 kuanza tena kazi.

Gharama.

1. Mafuta

Sbb tunatumia mafuta ya diesel niliona kuwa takribai lita 5 zinatumika kutoa kilo 200.

-pia shambani mule kuna muda ilibidi kukodi tela la ng'ombe kubeba mzigo kwenda kwenye collection point ilipo mashine

2. Labour

Wafanyakazi hawa tunawalipa sh ef 80 kwa kila kilo ef 1000 ( tani 1).

3. Usafirishaji.

Ilihitaji takribani sh 80 hadi 150 kusafirisha mzigo kupeleka kishapu.

Hizi zilobadilika kutokana na gari inavyopatikana. Muda mwingine nilipata fair free , muda mwingine niliweka mafuta tu, muda mwingine ilibidi nikodi.



4. Msimamiz.

Sbb muda mwingine sikua nakaa mwenye shambani , hivyo ilibidi nitafute 'shushushu' ambaye nililimlipa wastani wa sh ef 50 kwa mwezi.

Changamoto

1. Mashamba

Hili jambo lina gharimu sana. Kama nilivyosema usukumani katani nyingi ni mipaka ya mashamba. Hivyo ilibidi mara kwa mara kuhamisha mashine, ilibidi kukodisha usafiri ambao ulicost wastai wa ef 20 hadi 50 kutegemea na umbali. Hadi nafunga kambi nilikua sehemu moja karibu na samuye-shinyanga-nzeg to dar road. Hapa kidogo ilipunguza gharama sbb nilipata mashamba as mashamba.

2. Ubora wa mkonge

Sehemu nyingine unakuta ule konge umebabuka, hiyo nyuzi yake inatoka nyeusi, hiyo ni hasara hivyo inapunguza kilo sbb inabidi ukate sehemu mbovu.

3. Wafanyakazi

Kuishi na hawa watu inahitaji kiwango cha juu sana cha uvumilivu. Kukuta wametoka jioni kwenda kununua 'malaya' na kuacha kambi ni kawaida

Way forward.

1. Kuwa na mashine ya kisasa. Inapungunza uhutaji wa wafanyakazi pia inapunguza muda wa kazi. Hii mashine ya kawaida, inanipa kilo ef 1 ndani ya wiki moja na nusu.

2. Mashamba na si mipaka.

Nitaleta mrejesho tena kila muda unavyoenda na hasa msimu ujao.
 
Soko....mashine ukiipata dukani inauzwaje
 
Umeishiaje
 
Hakika we unaijua biashara ya mkonge kweli kuna changamoto mm ni mkazi wa mikoa uliyotaja mara nyingi mikoa hiyo wanalima mazao ya chakula na si biashara hata pamba wameitupilia mbali.kidogo dengu wanalima cause hata wasipouza watatumia kama mboga.mkonge wanafanya kama mpaka kama ilivyo minyaa wanaifanya kua fensi ya nyumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…