Tatizo sio wao, bali utamaduni wetu ambao mara baada ya kujifungua huanza kuwalisha kupindukia tena kwa kuwasimamia, tangu asubuhi hadi usiku utakuta mzazi mara ana bakuli la supu, mara uji wa mafuta, mara mtori, mara viazi mara................hee. Kula ni muhimu kwa ajili ya afya ya mtoto na mama lakini kuwalisha sana ni tatizo kubwa. Nimewaona baadhi yao wamekula supu nyingi yenye mafuta hata wameharisha wakalazwa.