SoC02 Unene na vitambi janga jipya kitaifa lisilopewa kipaumbele

SoC02 Unene na vitambi janga jipya kitaifa lisilopewa kipaumbele

Stories of Change - 2022 Competition

Angina

Senior Member
Joined
May 13, 2018
Posts
142
Reaction score
137
Unene ni hali ya mkusanyiko au ongezeko la mafuta mwilini.Hii ni hali ambayo mtu anakuwa na uzito mkubwa kuliko uzito ambao mtu anatakiwa awe nao kulingana na urefu wake.

Tatizo hili miaka ya nyuma lilikuwa likiwapa watu wenye maisha mazuri na hasa nchi zilizoendelea ,lakini kwa kipindi Cha Sasa tatizo hili linampata mtu yoyote awe tajiri au maskini,mjini au kijijini .Mwaka 2013 nchini marekani unene ulitambuliwa Kama magonjwa mengine na mtu.Miaka ya nyuma tatizo hili liliwapata Sana wanaume lakini kwa Sasa imekua Tofauti maana hata wanawake nao wana vitambi na ni wanene.

Kwa mujibu wa tafiti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyo chapishwa juni 2021 kuhusu unene uliopitiliza, zaidi ya watu bilioni 1.9 wenye umri kuanzia miaka 18 wana uzito uliopitiliza na watu milioni 650 wana vitambi duniai kote.

WHO imeenda mbali zaidi na kuanisha kuwa wanawake ndiyo wanaongoza kwa kuwa na vitambi kuliko wanaume. Hii inasababishwa na asili ya miili ya wanawake kuwa na uwezo mkubwa wa kuhifadhi mafuta au fati.

Je, utajuaje ya kuwa wewe ni mnene ? .Kwa kutambua BMI yako unaweza fahamu ya kuwa ww ni mnene au laah .BMI inatafuta kwa kupima uzito wako katika mfumo wa kilogram na urefu wako katika mita ,Zidisha urefu wako mara urefu wako mfano Kama una urefu wa mita 1.7 maana yake ni 1.7m x 1.7 m =2.89 m^2 ,Chukua uzito wako Kisha gawanya na 2.89 kwa mfano ukiwa na uzito wa 80kg ,BMI utaipata kwa kugawanya 80kg na 2.89m^2 ambapo utapata 27.68 Kg/m^2 hii ndo BMI yako .

Ukipata BMI chini ya 18.4 maana yake unazito mdogo ni Kama hauna lishe ya kutosha.

Ukipata BMI kuanzia 18.5 adi 24.9 maana yake uzito wako uko sahihi na unafaa.

Ukipata BMI kuanzia 25.0 adi 39.9 maana yake una uzito mkubwa na uko katika hatari ya kuwa mnene

Ukipata BMI kuanzia 40.0 na kuendelea maana yake wewe ni mnene .

NINI KISABABISHI CHA UNENE.
Sababu zko nyingi Sana zinazosababisha lakini sababu kuu ni mfumo mbovu wa ulaji na kutofanya mazoezi ndani ya hizi tunaweza pata sababu nyingine nyingi

1.Mfumo mbovu wa chakula : hii ni pamoja na mtu Kula Sana kupita kiasi hasa vyakula vya mafuta na wanga na vyakula vyenye sukari hasa vinavyozalishwa viwandani mfano bia na soda.

2.Kutofanya mazoezi : unapafanya mazoezi Kuna kiasi kikubwa Cha mafuta kinavunjwa ndani ya mwili ambapo mafuta hayo hubaki ndani ya mwili na kufanya mtu kuwa mnene asipo fanya mazoezi.

3.Hali ya kurithi : Kuna watu hata akifanya mazoezi kiasi gani au Kula chakula vizuri lkn Bado atakuwa mnene hi ni kutokana na kuwa na unene was kurithi kutoka kwa wazazi.

4.Jinsia: wanawake wapo katika hatari zaidi ya kupata vitambi ukilinganisha na wanaume hii Ni kutokana na miili yao kuwa na uwezo mkubwa wa kutunza mafuta.

MADHARA YA UNENE
Unene na vitambi ni chanzo kikuu cha magonjwa Kama
. kisukari ,presha ,magonjwa ya moyo hii mara nyingi hutokea kwa sababu ya mafuta kuganda ndan ya mishipa ya dami.

.Upotevu wa nguvu za kiume na kushindwa kutungisha mimba kwa wanaume na wakati mwingine kwa wanawake hii ndo chanzo cha mimba kutoka.

.Miguu kuvimba na kuwaka Moto hi Ni kutokana na Miguu kuzidiwa na uzito mkubwa wa mwili.

.Kupoteza umbo halisia hii ni kutokana na kuwa nyama uzembe na nyama nyingi kulegea

NINI KIFANYIKE
1.Serikali inabidi iipatie kipao mbele unene Kama magonjwa mengine yanavyo pewa kipaumbele lengo kubwa likiwa ni kupunguza hili janga ,Kama Serikali inabid ifanye vifuatavyo

.Kuhakikisha kila mtaa unakuwa na ma afisa lishe ambao kazi yao kubwa itakuwa ni kutoa elimu juu ya lishe na mpangilio wa lishe nyumba kwa nyumba ,na watu hao Kuhakikisha wanajua BMI za watu wanaowapa iyo elimu hii itasaidia endapo mtu akijulikana ana uzito mzito wampe wa aina gani ya lishe inabid atumie lengo kubwa ikiwa ni kupunguza uzito wake .

Hivyo hivyo kwa watu wenye uzito mdogo ni aina gani ya vyakula watumie ili waweze kuongeza uzito wao adi kufikia ule unaohitajika.

Kama ilivyokuwa kwa gonjwa la Corona lilivopewa kipaumbele na elimu yake kutangazwa kwenye magazeti ,vyombo vya habari ,kwenye madaladala ,mashuleni hivyo Serikali inabidi iongeze elimu juu ya hili swala maana jamii haijui kuhusu visababishi ,jinsi ya kuzuia hii kitu .Maana elimu kwa jamii inaweza punguza kwa kiasi gonjwa hili maana ni shida inayoondoa watu taratibu.

.Serikali kupitia serikali za mitaa inabidi ihakikishe Kuna kuwa na klabu mbalimbali ndani ya jamii ambazo zitakuwa zinafanya mazoezi mbalimbali walau mara tatu kwa wiki na serikali kusapoti hizo klabu za mazoezi kwa kuzipatia pesa za vifaa mbalimbali na za kujikimu.

2. Jitihada binafsi hii ni pamoja na kuwa na mpangilio mzuri wa chakula ikiwa pamoja na kupunguza ulaji wa vyakula vya wanga ,soda ,bia na kupunguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta Kama chipsi .Maana hata Kama unatumia dawa za kupunguza uzito lkn hauna mfumo mzuri wa chakula hii bado itakuwa shida na hauwezi kujisaidia kwa lolote hapo.

3. Matumizi ya juisi za kupunguza mwili (slimming juice) kama vile juisi ya maji ya ndimu na asali, chai ya tangawizi, mdalasini, mchai chai na limao ambavyo hutumiwa asubuhi dakika 40 au saa 1 kabla ya kupata kifungua kinywa kingine.

Nawasilisha kwenu.
 
Upvote 8
Hapo kwenye upunguzaji wa kula vyakula pendwa yaani chipsi, kuku, sosage , soda [emoji3047], beer [emoji481][emoji482] mishkaki, burger [emoji488] pizza [emoji487] hapo ni vita na wadada kuacha ni mtihani mkubwa sana.
 
Hapo kwenye upunguzaji wa kula vyakula pendwa yaani chipsi, kuku, sosage , soda [emoji3047], beer [emoji481][emoji482] mishkaki, burger [emoji488] pizza [emoji487] hapo ni vita na wadada kuacha ni mtihani mkubwa sana.
Ni changamoto Sana kuacha Lkn hicho ndo chanzo kikuu cha unene uliopitiliza
 
Back
Top Bottom