Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363

Tatizo la Unene Uliopitiliza (Obesity)Tatizo hili la unene uliopitiliza kuliko inavyohitajika kiafya huwa linaletwa na kuongezeka kwa kiwango cha mafuta mwilini. Njia rahisi na inayokubalika ya kuweza kugundua kama mtu ni mnene kupita kiasi (obese) inafahamika kama kipimo cha Body Mass Index (BMI). Vipimo hivi vya BMI ndio vinaweza kukujulisha kama unene ulionao unastahili kulingana na umri, urefu na uzito wako. Vipimo hivi ni kama ifuatavyo:Jinsi ya kupima BMI yakoKanuni ya BMI hutumia uzito wa mtu pamoja na urefu wake. Uzito wa mtu hupimwa katika kilograms (kg) na urefu wake katika mita (m) au sentimita (cm). Ikumbukwe pia kuwa mita moja ni sawa na sentimita 100 na mita² = mita x mita.
| Underweight |
| Obese |
[TD="align: center"] Category [/TD]
[TD="align: center"] BMI range – kg/m[SUP]2[/SUP] [/TD]
[TD="align: center"] Emaciation [/TD]
[TD="align: center"] less than 14.9 [/TD]
[TD="width: 306"] from 15 to 18.4 [/TD]
[TD="align: center"] Normal [/TD]
[TD="width: 306, align: center"] from 18.5 to 22.9 [/TD]
[TD="align: center"] Overweight [/TD]
[TD="width: 306, align: center"] from 23 to 27.5 [/TD]
[TD="width: 306, align: center"] from 27.6 to 40 [/TD]
[TD="align: center"] Morbidly Obese [/TD]
[TD="width: 306, align: center"] greater than 40 [/TD]
- Vyakula vya mafuta - Ulaji wa vyakula venye mafuta mengi au calories nyingi.
- Kutofanya mazoezi - Wale wasiofanya mazoezi mara kwa mara huwa wanene tofauti na wale wanaofanya mazoezi.
- Kurithi viashiria vya asili (genes) - Viashiria hivi vinaweza kuwa moja ya vichocheo vya kuongeza uzito kwani ndivyo huamua wapi mafuta huhifadhiwa mwilini na kwa kiwango gani. Lakini haimanishi kuwa mtu akiwa navyo basi ndio atakumbwa na tatizo hili.
- Umri - Watu wengi huongezeka uzito au hunenepa kadri umri unavyoongezeka kwa sababu wanakuwa hawajishughulishi sana (less active) na huwa wanapungua maumbile ya miili yao (muscles mass)
- Matatizo ya kisaikolojia - Wakati mwengine watu wenye matatizo ya kisaikolojia au msongo wa mawazo (stress) huwa na tabia ya kula sana, matokeo yake ni kunenepa.
- Dawa - Baadhi ya dawa zenye madhara ya kuongeza unene ni kama corticosteroids, blood pressure medications, tricyclic medications na kadhalika.
- Matatizo ya afya - Baadhi ya magonjwa yanachangia kuongezeka kwa uzito au kenenepa kama cushings syndrome, hypothyroidism, osteoarthritis na kadhalika
- Kukua kwa uchumi wa nchi - Wananchi wengi wanaoishi kwenye nchi zilizoendelea au wenye kipato kikubwa ndio wanaopata tatizo hili kutokana na kuishi mfumo wa maisha ya kivivu na hali ya kutokufanya mazoezi (sedentary lifestyle).
- Historia ya kuongezeka uzito uliopitiliza kwenye familia nayo yaweza kuhatarisha mtu kupata tatizo hili. Aidha, si jambo la kushangaza kuona karibu familia nzima au wengi wa wanafamilia kuwa wanene kupitiliza.
- Kutojishughulisha na chochote (inactive).
- Kupenda kula sana kuliko kawaida (overeating).
- Kula vyakula vya mafuta mengi
- Kutumia dawa zenye madhara ya kuongeza uzito uliopitiliza.
- Kuwa na ugonjwa wa vichocheo mwilini (hormonal disorders) kama cushing syndrome, hypothyroidism.
- Kuwa na msongo wa mawazo au kuathirika kisaikolojia.
- Kisukari
- Shinikizo la damu (hypertension)
- Kiharusi (Stroke)
- Magonjwa ya moyo
- Tatizo la kutopumua vizuri wakati mtu yupo usingizini (Sleep apnea)
- Vijiwe katika mfuko wa nyongo (Gallstones)
- Kiwango cha juu cha lijamu kwenye damu(cholesterol ikiwemo triglycerides)
- Ugonjwa wa mifupa kama yabisi (osteoarthritis).
- Saratani ya matiti
- Saratani ya tezi dume (prostate cancer)
- Saratani ya utumbo mpana pamoja na maeneo ya haja kubwa (Colorectal cancer)
- Matatizo ya mzunguko na mishipa ya damu kama vile kuvimba kwa vena za miguuni (varicose veins)
- Mabadiliko ya tabia - Hii inahusisha muhusika kupunguza kiwango cha chakula anachokula lakini kiwe chenye virutubisho vyote muhimu vya afya na kuongeza kiwango cha ufanyaji mazoezi.
- Mazoezi - Mazoezi husaidia kupunguza uzito hasa kipindi cha miezi sita ya mwanzo na hutunza uzito uliokusudiwa kwa muda mrefu. Pia hupunguza mafuta ya mwilini, huongeza ufanisi wa moyo, hupunguza tatizo la shinikizo la damu (hypertension), na kuweka sukari katika kiwango kinachohitajika mwilini.
- Dawa - Zipo dawa nyingi za kupunguza uzito lakini ikumbukwe ya kwamba hakuna tiba ya tatizo hili na dawa hizi zina madhara mengi kama kuongeza shinikizo la damu (hypertension), matatizo ya moyo, kuharisha,msongo wa mawazo (depression) na mengineyo.
- Chakula - Msingi wa kupunguza uzito au unene ni kujua ni kiwango gani cha calories mwili wako unahitaji kwa siku ili uwe unakula chakula ambacho hakitazidisha au kupunguza kiwango cha calories unazohitaji kwa siku. Mlo mzuri ni ule ulio na matunda kwa wingi, mboga za majani, nafaka ambazo hazijakobolewa, mafuta kidogo (less saturated fat). Vyakula vengine ni kama mayai, nyama isiokuwa ya mafuta (lean meat), samaki, kuku na vingineyo.
- Tiba ya upasuaji - Kuna aina nyingi za upasuaji ambao unasaidia kupunguza uzito aina hizi ni kama gastric banding, gastric bypass (Roux-en-Y-procedure), liposuction. Kabla ya kufanyiwa upasuaji, muhusika atahitaji kupimwa kisaikolojia (psychological testing) na kupewa ushauri nasaha kwani tiba hii pia ina madhara yake.
- Kisukari cha mimba (Gestatitional diabetes) - kisukari hiki kinatokea wakati wa ujauzito na hupotea baada ya kujifungua mtoto.
- Shinikizo la damu (hypertension)
- Shinikizo la damu wakati wa ujauzito pamoja na kifafa cha mimba (pre-eclampsia & eclampsia)
- Kuzaa kwa njia ya upasuaji (caesarean section)
- Tatizo la kiumbe kutopata hewa vizuri wakati wa ujauzito (fetal distress
Kwa wenye kutaka Dawa ya kupunguza Unene kwa kutumia Dawa za Tiba Mbadala Mitishamba nendeni hapa bonyeza https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/345085-good-news-kwa-wale-wenye-kutaka-kupunguza-uzito-wa-mwili-na-unene-na-mafuta-mwilini.html
au waweza kuwasiliana na mimi kwa njia ya email nitumie barua ya Pepe Email Address yangu hii fewgoodman@hotmail.com