Unene Uliopitiliza (Obesity)

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363



Tatizo la Unene Uliopitiliza (Obesity)


Tatizo hili la unene uliopitiliza kuliko inavyohitajika kiafya huwa linaletwa na kuongezeka kwa

kiwango cha mafuta mwilini. Njia rahisi na inayokubalika ya kuweza kugundua kama mtu ni

mnene kupita kiasi (obese) inafahamika kama kipimo cha Body Mass Index (BMI). Vipimo hivi

vya BMI ndio vinaweza kukujulisha kama unene ulionao unastahili kulingana na umri, urefu na

uzito wako. Vipimo hivi ni kama ifuatavyo:


Jinsi ya kupima BMI yako


Kanuni ya BMI hutumia uzito wa mtu pamoja na urefu wake. Uzito wa mtu hupimwa katika kilograms (kg) na urefu wake katika mita (m) au sentimita (cm). Ikumbukwe pia kuwa mita moja ni sawa na sentimita 100 na mita² = mita x mita.

Underweightfrom 15 to 18.4
Obese

[TD="align: center"] Category [/TD]
[TD="align: center"] BMI range – kg/m[SUP]2[/SUP] [/TD]

[TD="align: center"] Emaciation [/TD]
[TD="align: center"] less than 14.9 [/TD]

[TD="align: center"] Normal [/TD]
[TD="align: center"] from 18.5 to 22.9 [/TD]

[TD="align: center"] Overweight [/TD]
[TD="width: 306, align: center"] from 23 to 27.5 [/TD]

[TD="width: 306, align: center"] from 27.6 to 40 [/TD]

[TD="align: center"] Morbidly Obese [/TD]
[TD="width: 306, align: center"] greater than 40 [/TD]

BMI (kg/m[SUP]2[/SUP]) = Uzito katika kilograms/Urefu katika meters². Maana yake ni kwamba ili kuweza kupata BMI itakayokuwezesha kujifahamu kama u mnene ama la, chukua uzito wako gawa kwa kipeo cha pili cha urefu wako.


Tatizo la unene uliopitiliza husababishwa na nini ?


Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha unene uliopitiliza. Mambo hayo ni pamoja na


  • Vyakula vya mafuta - Ulaji wa vyakula venye mafuta mengi au calories nyingi.
  • Kutofanya mazoezi - Wale wasiofanya mazoezi mara kwa mara huwa wanene tofauti na wale wanaofanya mazoezi.
  • Kurithi viashiria vya asili (genes) - Viashiria hivi vinaweza kuwa moja ya vichocheo vya kuongeza uzito kwani ndivyo huamua wapi mafuta huhifadhiwa mwilini na kwa kiwango gani. Lakini haimanishi kuwa mtu akiwa navyo basi ndio atakumbwa na tatizo hili.
  • Umri - Watu wengi huongezeka uzito au hunenepa kadri umri unavyoongezeka kwa sababu wanakuwa hawajishughulishi sana (less active) na huwa wanapungua maumbile ya miili yao (muscles mass)
  • Matatizo ya kisaikolojia - Wakati mwengine watu wenye matatizo ya kisaikolojia au msongo wa mawazo (stress) huwa na tabia ya kula sana, matokeo yake ni kunenepa.
  • Dawa - Baadhi ya dawa zenye madhara ya kuongeza unene ni kama corticosteroids, blood pressure medications, tricyclic medications na kadhalika.
  • Matatizo ya afya - Baadhi ya magonjwa yanachangia kuongezeka kwa uzito au kenenepa kama cushings syndrome, hypothyroidism, osteoarthritis na kadhalika

Vihatarishi vya tatizo la unene wa kupitiliza


Aidha yapo mambo kadhaa ambayo yanaweza kumuhatarisha mtu kupata unene wa kupitiliza. Mambo haya ni pamoja na


  • Kukua kwa uchumi wa nchi - Wananchi wengi wanaoishi kwenye nchi zilizoendelea au wenye kipato kikubwa ndio wanaopata tatizo hili kutokana na kuishi mfumo wa maisha ya kivivu na hali ya kutokufanya mazoezi (sedentary lifestyle).
  • Historia ya kuongezeka uzito uliopitiliza kwenye familia nayo yaweza kuhatarisha mtu kupata tatizo hili. Aidha, si jambo la kushangaza kuona karibu familia nzima au wengi wa wanafamilia kuwa wanene kupitiliza.
  • Kutojishughulisha na chochote (inactive).
  • Kupenda kula sana kuliko kawaida (overeating).
  • Kula vyakula vya mafuta mengi
  • Kutumia dawa zenye madhara ya kuongeza uzito uliopitiliza.
  • Kuwa na ugonjwa wa vichocheo mwilini (hormonal disorders) kamacushing syndrome, hypothyroidism.
  • Kuwa na msongo wa mawazo au kuathirika kisaikolojia.

Magonjwa yanaoweza kuambatana na tatizo la unene uliopitiliza


  • Kisukari
  • Shinikizo la damu (hypertension)
  • Kiharusi (Stroke)
  • Magonjwa ya moyo
  • Tatizo la kutopumua vizuri wakati mtu yupo usingizini (Sleep apnea)
  • Vijiwe katika mfuko wa nyongo (Gallstones)
  • Kiwango cha juu cha lijamu kwenye damu(cholesterol ikiwemo triglycerides)
  • Ugonjwa wa mifupa kama yabisi (osteoarthritis).
  • Saratani ya matiti
  • Saratani ya tezi dume (prostate cancer)
  • Saratani ya utumbo mpana pamoja na maeneo ya haja kubwa (Colorectal cancer)
  • Matatizo ya mzunguko na mishipa ya damu kama vile kuvimba kwa vena za miguuni (varicose veins)

Tiba ya kuongezeka unene kupita kiasi


Tiba ya tatizo hili ni mhusika kujitambua ya kwamba ana tatizo na kuwa tayari kupunguza uzito. Mabadiliko ya tabia ya mhusika ni muhimu sana, mabidiliko haya yawe ndio mfumo wa maisha yake ya kila siku.

Kupungua uzito na kujilinda au kutunza uzito ulionao baada ya kupunguza uzito ni jambo la msingi sana na inahusisha mazoezi, chakula na madiliko ya tabia ya mtu.

  • Mabadiliko ya tabia - Hii inahusisha muhusika kupunguza kiwango cha chakula anachokula lakini kiwe chenye virutubisho vyote muhimu vya afya na kuongeza kiwango cha ufanyaji mazoezi.
  • Mazoezi - Mazoezi husaidia kupunguza uzito hasa kipindi cha miezi sita ya mwanzo na hutunza uzito uliokusudiwa kwa muda mrefu. Pia hupunguza mafuta ya mwilini, huongeza ufanisi wa moyo, hupunguza tatizo la shinikizo la damu (hypertension), na kuweka sukari katika kiwango kinachohitajika mwilini.
Kama hujazoea kufanya mazoezi ni vizuri uanze taratibu na ujiwekee lengo kwa kufanya mazoezi kwa muda wa nusu saa kila siku, siku tano kwa wiki,(dakika 30 kila siku kwa siku tano kwa wiki). Mazoezi mazuri ni kama kuogelea, kuendesha baiskeli, kutembea, kunyanyua vitu vizito (visiwe vyenye uzito mkubwa), mazoezi ya viungo na kadhalika. Kama mtu ni mnene sana basi ni bora kuzungumza na daktari wako kabla ya kuanza mazoezi mapya. Baada ya kuanza mazoezi kwa mara ya kwanza, mwili utakuwa na maumivu, hii ni kawaida lakini kama mtu atapata maumivu zaidi ya masaa 2 baada ya kufanya mazoezi ni vizuri kumuona daktari.

  • Dawa - Zipo dawa nyingi za kupunguza uzito lakini ikumbukwe ya kwamba hakuna tiba ya tatizo hili na dawa hizi zina madhara mengi kama kuongeza shinikizo la damu (hypertension), matatizo ya moyo, kuharisha,msongo wa mawazo (depression) na mengineyo.
  • Chakula - Msingi wa kupunguza uzito au unene ni kujua ni kiwango gani cha calories mwili wako unahitaji kwa siku ili uwe unakula chakula ambacho hakitazidisha au kupunguza kiwango cha calories unazohitaji kwa siku. Mlo mzuri ni ule ulio na matunda kwa wingi, mboga za majani, nafaka ambazo hazijakobolewa, mafuta kidogo (less saturated fat). Vyakula vengine ni kama mayai, nyama isiokuwa ya mafuta (lean meat), samaki, kuku na vingineyo.
  • Tiba ya upasuaji - Kuna aina nyingi za upasuaji ambao unasaidia kupunguza uzito aina hizi ni kama gastric banding, gastric bypass (Roux-en-Y-procedure), liposuction. Kabla ya kufanyiwa upasuaji, muhusika atahitaji kupimwa kisaikolojia (psychological testing) na kupewa ushauri nasaha kwani tiba hii pia ina madhara yake.

Wanawake ambao wana uzito wa kupitiliza (obese women) wakiwa wajawazito wako kwenye hatari ya kupata madhara yafuatayo;


  • Kisukari cha mimba (Gestatitional diabetes) - kisukari hiki kinatokea wakati wa ujauzito na hupotea baada ya kujifungua mtoto.
  • Shinikizo la damu (hypertension)
  • Shinikizo la damu wakati wa ujauzito pamoja na kifafa cha mimba (pre-eclampsia & eclampsia)
  • Kuzaa kwa njia ya upasuaji (caesarean section)
  • Tatizo la kiumbe kutopata hewa vizuri wakati wa ujauzito (fetal distress).

KWA WALE WENYE KUTAKA KUPUNGUZA UNENE WANIONE MIMI KWA NJIA YA EMAIL BARUWA YA PEPE EMAIL ADDRESS YANGU HII HAPA fewgoodman@hotmail.com AU WAWEZA PIA KUTEMBELEA BONYEZA HAPA.
Topic: Good news kwa wale wenye kutaka kupunguza uzito wa mwili na unene na mafuta mwilini
 
Watu wanene au wenye Fetma (Obesity) hukumbwa na hali ya kupenda kula kula au kwa maneno rahisi shauku ya kula. Ndio maana licha ya kujitahidi kufanya mazoezi au kufanya diet unakuta mhanga wa tatizo bado anaendelea kuwa na tatizo. Wengi wamefikia hatua ya kukata tamaa na kujiona ndio basi tena. Wengine wamejikuta wakiingia gharama kubwa kununua na kutumia madawa ya kupunguza unene bila kujali athari za madawa hayo kwenye miili yao. Sasa ngoja nianze kukueleza jinsi ya kukata shauku ya chakula.

Ipo njia moja tu ya kuondokana kabisa na tatizo la hamu au uchu wa vyakula ambayo ni kuondoa taka za asidi mwilini kwa kuufanya mwili uwe na alkali yaani ‘to alkalize your body to eliminate food cravings'. Unapaswa ufuate hatua mbili ili kuondokana kabisa na tatizo la uchu wa vyakula, moja ni kuchagua aina ya vyakula kulingana na uwezo wa mwili wako kuyeyusha vyakula hivyo (customize your diet to your own digestive metabolism). Hatua ya pili ni jenga tabia ya ku-alkalize mwili wako mara kwa mara kwa kutumia mlo wa viazi vyeupe (white potatoes). Ipo aina tatu za milo ya viazi ambayo nitaileza na jinsi ya kuiandaa. Kila aina ya mlo wa viazi vyeupe una tofautiana kidogo na aina nyingine kwa upande wa manufaa ya kiafya na pia hutofautiana kwa muda/kipindi mpaka manufaa yake kuonekana.

Viazi vilivyoiva Nusu (Semi-Raw Potatoes)
Manufaa ya aina hii ya mlo wa viazi ni ya muda mrefu. Unahitaji kutumia mlo huu kila siku kwa kipindi cha miezi 2 hadi mitano ili kufikia utatuzi wa tatizo la uchu wa chakula au kupunguza tatizo la kupatwa njaa mara kwa mara. Lakini pia mlo huu hutibu tatizo la gesi au kiungulia ndani ya kipindi cha wiki chache tu. Kwa watu wenye tatizo la kupatwa na asidi (acid reflux) huu ni mlo mzuri kwao kwani huyeyushwa vizuri mwilini.

Namna ya kuandaa: kata viazi (potatoes) katika vipande vidogo vidogo, ikiwezekana usivimenye maganda yake. Weka kwenye chombo cha kupikia. Weka maji lakini yasifunike viazi. Pika kwa kutumia moto usio mkali taratibu mpaka vianze kuwa laini lakini visiive mpaka ndani. Kisha ipua. Kula viazi na kunywa maji uliyopikia. Usiyamwage hayo maji.

Grated Potatoes
Hapa ni kwamba viazi vinakuwa kama vinasagwa au katwakatwa katika vipande vidogo vidogo kama ambavyo karoti husagwa. Vipande vipande hivyo vya viazi vina mucilage nyingi na husaidia kukata hamu ya vyakula ndani ya siku tatu au nne.

Namna ya kuandaa: Menya viazi kuondoa maganda yake. Hii hufanya viazi kuachilia mucilage nyingi zaidi. Kisha baada ya kuvimenya visage kwa kutumia kifaa cha kusagia (grate the potatoes). Kusaga viazi hufungua fiber za viazi kiasi kwamba joto wakati wa kuvipika hufanya mucilage kuachiliwa zaidi. Weka vipande vya viazi kwenye ‘an 8-inch frying pan'. Weka maji lakini usifunike viazi hivyo. Funika. Pika kwa joto la juu kidogo na pale maji yakianza kuchemka subiri dakika 2-3 kisha punguza joto (medium to low). Endelea kupika kwa dakika zingine 5-10. Mara nyingine itakulazimu kuwa unaongeza maji kidogo kidogo hadi viazi viive. Kwa aina hii ya mlo, viazi huiva kabisa. Lengo sio kutunza (preserve) vimeng'enywa (enzymes) na vitamin bali lengo ni kupata mucilage nyingi zaidi kadri iwezekanavyo kutoka kwenye viazi.

Namna ingine ya kuandaa mlo huu: menya kiazi kimoja kikubwa na kikate/kisage (grate). Weka siagi (butter) vijiko vidogo vitatu kwenye kikaango (frying pan) na weka kwenye moto hadi iyeyuke. Weka vipande vya viazi kwenye kikaango. Pika kwa joto la wastani kwa dakika 3 – 4. Punguza moto na endelea kupika kwa dakika zingine 4 hadi viazi viwe laini.

Alkalizing Potato Water
Kunywa maji ya viazi gasi moja au mbili kila siku. Ukitumia maji hayo kwa miezi miwili au mitatu mfululizo tatizo la njaa iliyopitiliza (excessive hunger) litatoweka.

Namna ya Kuandaa: Kata viazi viwili vikiwa na maganda yake katika vipande (Slices) na weka kwenye chombo cha kupikia. Weka maji hadi kuvifunika viazi. Chemsha vizi kisha viipue ila usiviondoe kwenye maji mpaka baada ya dakika 15. Mimina maji ya viazi kwenye chombo kingine. Viazi unaweza kuvitupa au kuvila maana nutrients tayari zimeondolewa kwenye hivyo viazi na ziko kwenye maji ya viazi.

Dondoo:

Ulaji wa kipande cha kiazi kibichi kabla ya kula chakula kinacholetea tatizo la gesi au asidi tumboni (hyperacidity) kutasaidia kukuepusha na tatizo la uyeyushaji chakula tumboni (indigestation).

Kula kipande cha kiazi kibichi baada ya kuwa umepatwa na tatizo la gesi (acid reflux) kutasaidia kuondoa tatizo hilo katika mfumo wa mwili wako unahusika na usagaji na uyeyushaji wa chakula.

Ulaji wa kipande cha kiazi baada ya kunywa chai au kahawa husaidia kukata asidi kinywani.

Aina ya milo ya viazi ambaye nimeieleza hapo awali inasaidia sio tu kukabiliana na tatizo la asidi inayopelekea mataizo ya uzito ulizidi au utapiamlo (obesity) bali pia kukabiliana na matatizo yatokanayo na mfumo wa chakula (digestive disorders) kama vile vidonda vya tumbo (ulcers), colitis, diverticultis na Crohn's disease.

Mimea, matunda na juisi kwa ajili ya tiba ya tatizo la uzito wa mwili
Pamoja na maelezo niliyokwisha kueleza kuhusu suala hili la uzito au unene kupindukia napenda pia nikueleweshe baadhi ya mimea, matunda na juisi kwa tatizo hilo kama ifuatavyo:


  1. Parachichi (Avocado). Husaidia kupunguza rehamu (cholesterol) mwilini na kuzuia uharibufu wa ini (liver damage preventative). Kula tunda moja au mawili kila siku.
  2. Ndizi (banana). Hupunguza tatizo la kuongezeka uzito, kukosa choo na vidonda vya tumbo. Kula ndizi mbivu kila siku.
  3. Iliki (Ginger root). Hutibu tatizo la kukosa hamu ya kula na tatizo la kutofanya kazi ipasavyo kwa mfumo wa uyeyushaji chakula mwilini. Itumie kama chai na pia weka kwenye chakula unachokula kama kiungo (spice).
  4. Zabibu (Grapes). Hupunguza unene na kuimarisha afya ya mwili. Tengeneza juisi ya zabibu na itumie kutwa nzima huku ukiwa umefunga kula chakula na pia unapaswa kunywa maji glasi 4-5 wakati ukiwa kwenye mfungo huo. Fanya hivyo siku moja kwa wiki na siku 6 zingine kula mlo kamili (balanced meals).
Juisi ya zabibu pia husaidia kutibu magonjwa ya moyo (Heart diseases), kiharusi (strokes) na shambulizi la moyo (heart attacks) na kuziba kwa mishipa ya damu (Arteries anti-clotting). Kwa tiba ya magonjwa hayo kunywa glasi moja ya juisi hiyo iliyotengenezwa kwa zabibu nyekundu (red grapes). Ili kuongeza kasi ya matibabu ya matatizo hayo kula saladi iliyonyunyizwa mafuta ya mizeituni (olive oils) na kunywa juisi ya zabibu nyekundu.


  1. Kiwi (kiwifruit). Hutibu tatizo la kukosa choo (constipation and bowel movements). Ulaji wa matunda 2-4 yakiwa na maganda yake hupelekea kupata choo katika kipindi cha ndani ya masaa 24.
  2. Linseed: hutibu tatizo la kukosa choo. Saga mbegu za linseed kufanya unga. Asubuhi kabla ya kula chakula chochote kunywa maji glasi moja yaliyowekwa unga wa linseed kijiko kimoja cha chakula. Vivyo hivyo kunywa glasi mija ya maji yenye linseed saa moja baada ya kula chakula (main meal).
  3. Mapesheni (passionfruit). Hutibu tatizo la kukosa choo, kutuliza akili (calming effect) na kuzuia maambukizi ya njia ya mkojo (Urinary tract infections –UTI). Kula matunda 2-3 pamoja na mbegu/nyama zake za ndani kila siku.
Unywaji wa juisi iliyotengenezwa kwa mchanganyiko wa mapesheni 2, chungwa moja na vipande viwili vya tikiti maji, asubuhi kabla ya kula chochote ni kinywaji safi kwa kuimarisha afya ya mwili wako.



  1. Prunes. Hutibu tatizo la kukosa choo na hupunguza rehamu mwilini. Kula fresh prunes asubuhi kabla hujala chochote na masaa mawili baada ya kula chakula cha usiku. Ukikosa fresh prunes nunua prunes zilizokaushwa (hupatikana supermarkets) na ziloweke kwenye maji hadi zilainike na zile.
  2. Tikiti (watermelon). Husaidia kupata choo na pia huzuia uharibufu wa ini (liver damage preventative). Kunywa glasi moja ya juisi asubuhi nusu saa kabla hujala chakula chochote.
  3. Juisi ya kupunguza uzito iitwayo 'Thai Tango'. Weka kwa pamoja kwenye blender: papai lililomenywa gramu 100, pears mawili yaliyomenywa na kukatwa vipande, juisi ya ndimu moja, maji ya mchele (rice milk) 200ml na unga kidogo wa iliki. Blend pamoja kutengeneza juisi.
  4. Tembelea blog makini Asili Yakoupate mada kamili kuhusu jinsi ya kuondokana na Tatizo la Fetma (Obesity) na matatizo mbalimbali ya kiafya.
 
Asante kamanda kazi kwa elimu barikiwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…