Unga kilo shilingi 2,200, Serikali iingilie kati

Mbona vingine ni kidogo lakini bei ipo juu? Shukuru kupata huo unga maana kama huna Family ni mlo wa siku 2
 
Serikali inaingiaje hapa.Serikali inalima mahindi?
Miaka miwili ilopita mahindi yalikua mengi sana na Bei ilikua nzuri na ya kawaida hiyo serikali ikasema mahindi yasivushwe kwenda nje.soko likashuka mahindi yaliuzwa mpaka elfu 20 gunua.imagine umelima heka kwa laki tano umepata magunia yako 15 unauza kwa elfu ishirini.Watanzania walishangilia sana sana kwamba unga umeshuka Bei. Ila hawakujua soko Mara nyingi hutegemea demand and supply


Wakilima wakubwa wa mahindi walizira kulima.hata Mimi sikuthubutu kulima heka nyingi nililima ya kula na watoto Basi na sitegemei kuuza kamwe hata mahindi yapande vipi
Ila serikali yetu tukufu imeelewa kwa Sasa haiingilii tena bei za mazao hasa ya chakula kikiwa kichache utapata kwa ghali kikiwa kingi utapata rahisi.usitake mteremko kwa gharama za mkulima
 
Hiyo bei itakua imesababishwa na mzozo wa iran na marekani serikali inabidi iingilie kati
 
Huu ndo ukweli
 
Kuna mahali ilisemwa ukiona bei ghali lima mahindi yako!!!
=====
Kwa mikoa mitano niliyotembelea, kilo ya unga wa mahindi ni 1500 bei juu kabisa.
 
Kaekari kangu kamoja kanaendelea vizuri huko shamba, next week nikatie mbolea nisubiri kuvuna.
Kila mtu ashinde mechi zake
 
Hivi tambi zinashibisha?. Mimi naona huwa zinanikinaisha ila nabaki na njaa.
tambi zina njaa halafu bei, mfano unga kilo tano unanua 6500,je ukinunua tambi bei huyo si unapata 4 zinaisha Siku 3 tofauti na Inga wiki moja na nusu
 
Wakulima tumeuza kilo Tsh. 700 mwanzo wa msimu. Wateja wengi walikua jirani zetu kina Kenya, Zimbambwe and co.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi tambi zinashibisha?. Mimi naona huwa zinanikinaisha ila nabaki na njaa.
Mimi sipendi hata kuziona hizo kitu.

Ila watu wanachukulia mambo kirahisi sana hapa jukwaani. Eti 'kula wali, kula keki, kula tambi' dahh 😂😂.

Arusha hapa kilo ya unga 1500 hadi 1600.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…