Unga wa dengu

Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2012
Posts
52,160
Reaction score
48,974
Nina tatizo la kuota chunusi usoni, nimeshauriwa na mtu nitumie unga wa dengu. Hii itasaidia kumaliza tatizo?
 
Unachanganya unga wa dengu kiasi na kiini cha yai. Paka then kaa nayo hadi uone imekauka. Kujua imekauka utaona imekakamaa usoni na inaweka kama ufa. Sugua kwa mkono kutoa halafu osha kwa maji safi na salama. Hakikisha una kitaulo special kwa ajili ya kujifutia usoni.
 

asante kwa ushauri.
 
Sababu za wanawake kuandamwa na chunusi

TATIZO la chunusi, linawasumbua wengi wanawake sana hadi baadhi yao kufikia hatua ya kukata tamaa kutokana na kukosa ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hilo.

Je, unaelewa kuwa kwa asilimia 99, chunusi kwa mwanamke husababishwa na yeye mwenyewe?

Mambo yanayosababisha chunusi kwa mwanamke ni haya yafuatyo:

Ulaji usio makini: Wakati mwingine ulaji wa vyakula vyenye mafuta humweka mlaji hususani mwenye ngozi ya mafuta kupata chunusi. Si hivyo tu, wakati mwingine kutokula chakula bora kunaweza kukuletea tatizo hilo.

Matumizi ya nguo chafu: Kulala kwenye foronya chafu zenye vumbi na mafuta pia hukuweka kwenye hatari ya kupata chunusi, ni vyema hili likatambuliwa na kila mwanamke.

Unashauriwa kuvaa kofia ya kulalia wakati wa kulala ili kuepuka kuchafua foronya zako, na pia kufanya usafi wa mara kwa mara wa foronya na shuka za kulalia.

Kujishika usoni mara kwa mara: Wanawake wengi wanapenda kujishika usoni mara mwa mara, bila kuwa na hawana uhakika na usafi wa mikono yao. Jambo hili mara kadhaa limekuwa likisababisha, maambukizo ya bakteria katika ngozi wanaoleta maradhi kama vile ya chunusi na mengineyo.

Kuzembea wakati wa kuosha nywele: Kwa kawaida vipodozi vya nywele huambatana na mafuta wingi. Hivyo mhusika asipokuwa makini wakati wa kuosha, wakati mwingine husababisha mabaki ya mafuta hayo kuingia usoni na hivyo kuiweka ngozi ya uso katika hatari ya kupata chunusi.

Matumizi yasiyofaa ya vipodozi: Kutumia vipodozi bila kufuata ushauri wa wataalamu, husababisha wahusika kuzalisha chunusi. Kwa mfano mwenye ngozi ya mafuta anapotumia vipodozi vya mafuta husababisha kutokea kwa chunusi.

Ukosefu wa elimu ya utunzaji wa ngozi: Kila ngozi ya mwanamke inatakiwa kufanyiwa huduma mbalimbali kama vile scrub, kuondoa seli zilizokufa, kuwekewa mvuke na nyingine nyingi. Wakati mwingine ikiwa haya hayakufanyika , huwa ni chanzo cha uzalishaji wa chunusi katika ngozi.

Kulala na vipodozi: Hili ni tatizo sugu kwa wanawake wengi. Wengi kutokana na hali fulani hushindwa kuondoa vipodozi wakati wa kulala hivyo kujiweka kwenye hatari ya kupata chunusi. Hakikisha unaondoa vipodozi vyote kabla ya kwenda kulala.

Dawa ya kutibu Vipele (chunusi) Na Ngozi:

Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, ½ (nusu) kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha (apple). Paka katika sehemu

inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi.
 


WOTE tunaamini kuwa wanaume hawapendelei masuala ya urembo. Pia watu wengi wanaamini kuwa mambo ya urembo ni kwa ajili ya wanawake tu. Tafiti za hivi karibuni zimeonyesha kuwa wanaume pia wanapenda urembo. Kwa mantiki hiyo, si vibaya ikiwa tutawaletea dondoo muhimu za urembo kwa wanaume.

• Usafishaji wa uso

Kuondoa chunusi usoni.Hakikisha uso wako unakuwa safi muda wote. Pia unashauriwa kutumia sabuni zisizo na kemikali kuosha uso wako. Ni vema uoshaji uso ufanyika si chini ya mara mbili kwa siku. Fanya steaming’ uso wako, kwani husaidia kukuondolea tatizo la chunisi usoni.


Kama utatumia ‘toner’ni vizuri ukatumia zenye ‘alovera’ au vitamini E kwa wingi. Kwa upande wa midomo, unaweza kutumia Vaseline kulainisha ngozi ya midomo yako.

• Matunzo ya nywele Kwa maisha ya sasa, hata wanaume wamekuwa makini katika kuboresha muonekano wa nywele zao. Tofauti na wanawake, wanaume hawaitaji vipodozi vingi. Pakaa mafuta nywele kila siku.

Kama utaratibu huu utakupa shida, basi hakikisha unafanyia ‘masaji’ ya mafuta ngozi ya kichwa chako kila mwisho wa wiki. Kisha osha nywele zako kwa shampoo baridi isiyo na kemikali zinazodhuru. Ikiwa unasumbuliwa na tatizo la kukatika kwa nywele, hakikisha unachagua nywele fupi badala ya ndefu. Ikiwa umri unaruhusu si vibaya ukatumia jeli ya nywele.


• Matunzo ya mwili Wakati mwingine inawezekana ukawa na vinyweleo vingi mwilini. Ili kuonekana mtanashati unashauriwa kupunguza, hasa vinavyokuletea kero au kuharibu muonekano wako.

Ukiachilia mbali suala la vinyweleo, mapumziko ya mwili ni muhimu sana katika kuboresha muonekano na pia afya ya mwili wako.

Unashauriwa kufanya ‘masaji’ ya mwili wako mara moja kwa wiki. Hii itasaidia kurahisisha mzunguko wa damu mwilini mwako na hivyo kukufanya ujione mwepesi na usiye na uchovu.


Boresha muonekano wa kucha zako za mikono na miguu kwa kuzikata mara kwa mara. Pia unashauriwa kufanya mazoezi na kula mlo kamili,hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kujenga mwili wako.


• Vipodozi Tumia marashi yanayoendana na harufu yako. Usipake marashi kwapani kwani wakati mwingine huunguza na kufanya ngozi ya kwapa kuwa nyeusi. Pendelea kutumia poda kwa vile hupunguza harufu mbaya mwilini. Ikiwa unasumbuliwa na ukavu wa midomo, tumia ‘lip balm’
Dondoo za urembo kwa wanaume
 
kuna aina za cream na ointment zinazodeal na haya matatizo,eg Persol 2.5,persol cream etc,ni tiba njema,personally nilikuwa na tatizo kama hili nilitumia Persol 2.5 nw m doing great kwa moda mfupi,so mtafute mtaalamu wa magonjwa ya ngozi utafanikiwa ol the best,tunasubiria feedback!
 

asante Gilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…