Unga wa Donor

Unga wa Donor

Kiziwanda chema

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2016
Posts
288
Reaction score
478
Ulikua na umri gani ulipogundua kuwa ugali wa Dona sio unga unaotokana na mahindi yasiyokobolewa bali ni unga wa msaada kutokana na njaa ya mwaka 1984 *(unga wa Donor... From Donor country)* 😄

Wewe endelea kusema Dona ni unga wa mahindi yasiyokobolewa 😊😊
 
Hahaha na mimi nlikuwa na sikia watu tukio dogo tuu wanasema "sitaki mada kesi" nikaja kujua imetokana na kizungu "murder case" yaan kesi ya mauaji sasa wabongo kitu kidogo tuu utasikia sitaki mada kesi.
 
ahaaa sasa ndo nimeelewa,
Unga wa yanga,,unga wa donor,
Donor kauntiri (kama anavyotamka mwenyewe)
 
Ni wewe tu ndiye mpaka sasa bado unaishi kwa mazoea
Ni kweli historia inasema hivyo lakini kutokakana na kukua kwa lugha yetu neno UNGA WA DONA lina maana tofauti na ile iliyowahi tumika miaka hiyo na sioni kwanini bado tunautukuza ubeberu kwa kuwalisha watu watango pori kwamba kila tutumiapo unga wa dona bado tunaenzi ufadhiri au misaada ya nchi za kimagharibi
 
Kutumia jina UNGA WA DONA sidhani kama tunaenzi ufadhiri wa mabeberu, hilo jina lilikua miongoni mwa maneno ya misimu tu ambayo kwa bahati nzuri yamepata kutumika kwa muda mrefu hadi leo hii. Hilo sio tango pori
 
Mleta mada 1974 kulikuwa na njaa kali sana, tulipata unga wa njano na unga wa uji wenye sukari na maziwa uliitwa bulger
 
Mleta mada 1974 kulikuwa na njaa kali sana, tulipata unga wa njano na unga wa uji wenye sukari na maziwa uliitwa bulger
Aiseee hatari, ila huo mwaka sidhani kama dingi alikua na wazo au tegemeo kupata kidume kama Mimi.. I came into existence baadae sana
 
Back
Top Bottom