...Ungekuwa wewe ungefanyeje

Maswalala

Senior Member
Joined
Mar 30, 2011
Posts
149
Reaction score
12
Unamkewako wa ndoa unaishi naye vizuri tu ndani ya nyumba na anakutimizia haja zako zote na unamwamin sana naye pia anakuamin lakin kwa upande wako unamwanamke mwingine nje ya ndoa na hupendi mkeo wala watu wa karibu wajue hilo... Siku moja mnapanga kukutana na huyo kimada wako kula raha dunian na mnakubaliana kukutana gesti iliyoko nje kidogo na mji, so unabuni safari ya ghafla na unamuaga mkeo kuwa umepata dharura ya kikazi kwa mda wa ck 2 unaondoka na kumuacha mkeo....kumbe huku nyuma alikuwa na mahusiano ya siri sana na mwanaume mwingine bila ya wewe kujua so nae akaona hiyo ndo chansi ya kutumia wakawasiliana na mtu wake wakutane na wakakubaliana kutoka nje ya mji(gest)
....so we mwanaume umekutana na hawara yako mmeingia gest na mhudumu wa gest kawakabiz chumba then kilichofwata mkafurahia penzi motomoto, inafika wakati wakutoka chumbani ukiwa we na hawara yako ghafla pasipo kutarajia unamwona wife wako naye anatoka chumba opposite na kile ulichotoka akiwa na mwanaume wake mnakutanisha macho kumbuka kabla ya hapo hakuna aliyewahi kumhic mwenzake kama anamahusiano nje ya ndoa. Je kama wewe mwanaume/mwanamke unafanya nn kwa wakati huo, na utachukua reaction ip
karibun kwa maon yen
 
Aisee...Great thinker umenikuna sana hapa.............ngoja niendelee kudownload..........
 
Kwa kuwa sitarajii kucheat...

Hiyo scenario hainihusu...

Ila kuna rafiki yangu wa kihindi yalimkuta..alikuwa hajui kama mkewe ni girlfriend wa rafiki yake..ingawa mke wa rafiki yake huyo alikuwa anaujua mchezo mzima..

Kuna siku waliamua kwenda disko..kila mtu aje na mkewe.. Wakaanza kufakamia pombe..wakawa wanatoka wanaenda kudensi,ambapo ilikuwa kitu udhungu hivi.. Umamnyanyua shemeji yako time yoyote mziki unaokonga moyo wako unapopigwa...

Ilifikia wakati yule rafiki yangu akawa hamwoni mkewe wala rafiki yake.. Ila shemeji yake alikuwepo,na alionekana kama kakolea kilevi hivi.. Rafiki yangu alipouliza walipo wenza wao,yule mwanamke akasema anajua waliko,hivyo wachukue taxi wawafuate..

Cha ajabu rafiki yangu alishangaa safari ikiishia hotelini,na ni baada ya kuwa ameliwa denda na vituko vingine kadhaa..jamaa akalipa wakaingia room.. Pamoja na malavidavi yaliyoendelea,alishangaa kumwona shemeji yake alivyokuwa relaxed as if hakuna jipya wala la ajabu linaloendelea.

Asubuhi yake rafiki yangu baada ya kubrain storm saaana uongo atakaoutumia kumpeleka shemeji yake kwa mumewe,na kwamba angemuomba rafiki yake waende pamoja kwa mkewe akamsaidie kuapologize..
Cha ajabu pea zote mbili zilikutana lounge! Rafiki yangu alipigwa sana na butwaa.. Alishindwa kuamini kama mkewe ingetokea hata siku moja angemsaliti..ndipo alipoamini maneno ya shemeji yake..kwamba relationship ya mkewe na rafiki yake ilikuwepo muda mrefu!

Alichoniambia yeye hakukasirika,zaidi ya mkewe kuwa katika hali ya kutamani ardhi ipasuke adumbukie ndani. Rafiki yake sasa alikasirika sana,na kumzoa mkewe hobelahobela hadi car park kutafuta taxi bila kuagana na wenzao!

Hiyo ni Dar,na ni kama miaka 15 hadi 20 iliyopita kisa hiki kilipotokea!
 
Watu wa mjini wanasema ngoma droo unaseti mambo mengine yaende kwenye mtandao.
 
hakuna la kufanya zaidi .. kwani umeshaelewa wewe na wmenzako mna tabia za aina ipi
 
ni vgum kutokea hii ni ya kufikirika 2
 
nyote.............ni majeruhi watupu....................mkajitibu maumivu
 
Ni majuma kama matatu tu yaliyopita mkasa wa aina hii umetokea Kibaha.Tena wote walitokea Dar.Sijui ndio huu?
 
Hizi ndo challenge za ndoa vijana mjue! hapa hakuna cha ndoa kuvunjika ! Sioni nani hapa kati ya hawa ambae hajakosea!! Hahahaaaaaaa! cd imekula deki!!


 
Jambo hili linaonekana rahisi kama linavyo somwa ila ni GUMU mno

kila mwanadamu anajinsi tofauti ya kupokea mambo

Umeoan huyo Dada alifahamu muda kua mumewe ana Cheat

Lakini hakuonyesha kitu mpaka alipopata nafasi alioona ni njema ikatumika kulipiza

Lakini mwingine ataona wapotezee mambo yasonge mbele,

Mwingine Talaka kama ilivyoonekana hapo juu

Mwingine Urafiki mwisho , mwingine urafiki utabaki wa mashaka wengine watakaa na kusuluhishana wengine.......

Nikuomba neema ya Mungu hayo yasikukute kabisa

Maana hujui utaamuaje pindi ukiyaona live
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…