Elections 2010 Ungependelea Rais wako wa 2010 awe na mikakati gani?

Elections 2010 Ungependelea Rais wako wa 2010 awe na mikakati gani?

Mutensa

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2009
Posts
421
Reaction score
92
Mara nyingi huwa tunajadili nani anastahili kuwa rais, nani ana nafasi kubwa ya kuwa rais, nk. Mimi najiuliza swali moja ambalo labda lingemsaidia yeyote anayeingia IKULU kujua watanzania wanahitaji nini au wanategemea nini kutoka kwake .... Je, Ungetaka raisi wako afanye nini na nini?

Tafadhari weka vitu ambavyo vinanufaisha nchi kwa ujumla .... Kwa mfano sitegemei umwombe rahisi akujazie mapesa mfukoni ukiwa nyumbani umelala.
 
Arejee yale mema yote yaliyofanywa na Mwalimu, Mwinyi na Mkapa kwa manufaa ya Taifa na kuyaendeleza. Apambane na ufisadi wa aina yoyote ile kwa dhati bila kumuonea huruma wala soni yeyote ambaye ana hata harufu ya shutuma.
 
Mkakati wa kutokuwa na mkakati wowote. Mikakati imekuwepo mingi na mizuri sana (nenda kasome ilani ya uchaguzi ya ccm) kwa kiwango fulani ila utekelezaji ndio tatizo.
 
.Kuhakikisha rasilimali zetu zinawanufaisha Watanzania wote badala ya wageni na mafisadi wachache.
.Kupambana na mafisadi bila woga wala kificho
. Kuboresha maisha ya Watanzania kwa kuongeza ajira, mishahara, kuwapa msaada mkubwa wakulima wa mazao ya chakula na biashara.
.Kuhakikisha shule zetu zinakuwa na hadhi ya kuitwa shule Tanzania nzima na kuwa na walimu wenye sifa za kufundisha katika shule hizo kuanzia shule za msingi hadi vyuoni.
 
Back
Top Bottom