BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Mimi ni Mwananchi ambaye nimekuwa nikipata huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Magharibi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja (Hospitali ya Ijitimai) kuna kero ambayo imekuwa ikinisumbua muda mrefu na ninaamini inasumbua watu wengi pia.
Nimekuwa nikifika kituoni hapo kupata huduma ya Ugonjwa wa Sukari (Diabetes), changamoto iliyopo hospitalini hap oni kuwa hakuna usiri kwa Wagonjwa, unakuna muda mwingi tunawekwa katika chumba kimoja hadi wagonjwa Watano.
Unakuta wote watano au zaidi ya mmoja mpo kwa Daktari mkitakiwa kueleza shida ya kila mtu binafsi, sasa haki ya faragha iko wapi hapo?
Kinachotokea unakuta wengi wetu tunabakaki na dukuduku, tunashindwa kuwa na uhuru wa kuzungumza, hilo jambo siyo zuri kabisa.
Tunaomba kama Madaktari hawawezi kutuweka katika vyumba tofauti au kutusikiliza mmoja mmoja basi itafutwe njia nyingine mbadala badala ya hiki kinachoendelea ambacho kinatuumiza wengi.