UNHCR: Watu milioni moja wameachwa bila makao Somalia kutokana na ukame

UNHCR: Watu milioni moja wameachwa bila makao Somalia kutokana na ukame

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Umoja wa Mataifa unasema ukame wa kihistoria nchini Somalia umepelekea watu milioni moja kuyakimbia makaazi yao sasa na kuiacha nchi hiyo ikikabiliwa na baa la njaa.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR linasema, zaidi ya watu 755,000 wameyakimbia makaazi yao ila wanasalia kuwa ndani ya nchi hiyo na wakijumlishwa na wale walioikimbia nchi, idadi kamili ni milioni moja.

UNHCR inasema idadi ya watu wanaokabiliwa na mzozo wa njaa nchini Somalia inatarajiwa kuongezeka kutoka watu milioni 5 hadi zaidi ya milioni 7 katika miezi kadhaa ijayo, jambo lililochangiwa na mabadiliko ya tabia nchi na vita vya Urusi na Ukraine.

Somalia na majirani zake Ethiopia na Kenya wanakabiliwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 40 baada ya kufeli kwa mvua kwa misimu minne.

DW
 
Back
Top Bottom