SI KWELI UNICEF wanatoa pesa kwa watu Mtandaoni kupitia Foundation yao

SI KWELI UNICEF wanatoa pesa kwa watu Mtandaoni kupitia Foundation yao

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Ninahitaji kufahamu ukweli kuhusu hawa watu wa UNICEF kutoa fedha kwa watu kupitia humanitarian Foundation kutoka kenya ni kweli au matapeli, maana wanakupa maelekezo kisha kukwambia ili upate fedha za UNICEF unatakiwa ulipie kiasi fulani kinachoendana na kiasi utakachopatiwa mfano ulipie elfu 20 kwa account fulani wanazijua wao kisha uwaambie kwamba ushalipia ili wakuingizie Tsh. Milioni 1M.

UNICEF Fake.jpg
 
Tunachokijua
UNICEF ni Shirika lisilo la kisiasa linalo jihusisha na kulinda haki za kila mtoto duniani kote katika nchi na maeneo zaidi ya 190.

Wakiwa wasambazaji wakubwa zaidi wa chanjo duniani, UNICEF husaidia afya ya watoto na lishe, maji salama na usafi, elimu bora na kujenga ujuzi, kuzuia na kupambana na VVU kwa akina mama na watoto, na kulinda watoto na vijana kutokana na ukatili na unyonyaji.

Madai ya UNICEF kutoa mikopo Mtandaoni
Madai ya Shirika la UNICEF kutoa mikopo mtandaoni kupitia UNICEF Foundation yamekuwa yakisambaa kwa kasi mtandaoni. Mathalani, baadhi ya Matangazo ya utoaji huu wa fedha yamehifadhiwa hapa na hapa.

Aidha, ujumbe mwingine unaosambaa mtandaoni unawataka watu wakubali baadhi ya maswali na kuwataka watoe kiasi fulani cha pesa ili wapatiwe mkopo.

Hata hivyo, ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa UNICEF haijihusishi na utoaji wa fedha mtandaoni kama inavyodaiwa. Pia, kurasa za Mitandao ya kijamii ya UNICEF ikiwemo X na Facebook haijachapisha taarifa yoyote ya utoaji wa fedha hizi.

Aidha, utafutaji wa maneno muhimu yenye nasaba na tangazo hili, JamiiCheck imebaini kuwa Aprili 20, 2024, ukurasa rasmi wa UNICEF Tanzania kwenye Mtandao wa X ulikanusha madai haya.

"UTAPELI: UNICEF Tanzania inafahamu kuhusu madai ya utapeli yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na WhatsApp na kuahidi zawadi za kifedha kupitia UNICEF Foundation. UNICEF haina uhusiano wowote na UNICEF Foundation. UNICEF hawagawi pesa mtandaoni. Sambaza hii habari" ilisema taarifa ya UNICEF.

glmdcjtwyaafd6l-jpg.3037432


Pamoja na mambo mengine, kanusho hilo liliambatana na ujumbe unaotoa angalizo kwa watu kutokutoa taarifa za kibinafsi kwa watu.
Back
Top Bottom