UNICEF yaingilia kati kuokoa watoto Korogocho Kenya

UNICEF yaingilia kati kuokoa watoto Korogocho Kenya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, kwa msaada wa shirika la Uingereza, UK Aid, linasaidia kutoa huduma ya ulinzi kwa watoto katika makazi duni au yasiyo rasmi, Korogocho, walioathiriwa na kufungwa kwa shule kutokana na janga la COVID-19.

Korogocho, Kenya, eneo la makazi duni lenye ukubwa wa kilomita moja na nusu za mraba na idadi ya watu inayokadiriwa kufikia laki mbili.

Kama ilivyokuwa kwa maeneo mengine duniani, watoto wa Korogocho nao wamelazimika kubaki nyumbani kutokana na kuzuka kwa janga la virusi vya corona. Athari hazijaishia tu katika kukosa masomo bali pia wamekumbana na unyanyasaji kama anavyoeleza mtoto huyu mwenye umri wa miaka 7, amepewa jina Kijana, ili kuhifadhi jina lake halisi. Mtoto huyu anasema, “nilikuwa ninacheza mchezo wa kujificha na kufichuana wakati vijana wawili waliponiita, wakanivua nguo kisha waakanza kunivuta (sehemu zangu za siri). Kisha wakanipiga. Nilikuwa nasikia uchungu. Nilienda haja ndogo nikasikia uchungu. Nikarudi nikamwambia mama akanipeleka hospitali.”

Kesi ya mtoto huyu ilifikishwa katika Idara ya huduma za watoto na polisi baada ya kuwa amepatiwa matibabu, lakini vijana waliomfanyia unyanyasaji hawakupatikana.

Eugenia Olliaro ni afisa wa UNICEF katika kitengo cha ulinzi wa watoto katika dharura anasema wakati wa kufungwa kwa shule wameona ongezeko la unyanyasaji dhidi ya watoto ukiwemo unyanyasaji wa kingono na kijinsia. Matukio haya ni theluthi ya matukio yote ya uhalifu yaliyoripotiwa nchini Kenya tangukuanza kwa COVID-19.

UNICEF kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la TDH linalopigania haki za watoto, wamefadhili mafunzo ya washauri jamii 130 ndani ya Kogorogo. Hawa wanaripoti matukio ya unyanyasaji kwa walinzi wa watoto au polisi. Margaret Mbala ni mmoja wa washauri hao, anasema, “nilikuja kuwa mshauri jamii. Kwa sababu ninapenda mahali ninapoishi. Na nilipokuwa naona watu wanafanya makosa kwa sababu hawajui, TDH walinichukua wakanipeleka kwenye mafunzo, wakanifunza vile ambavyo ninaweza kufundisha hata wale wengine mbao hawakuwa wanajua kuwa wanakosea, sasa nilianza kuwafunza ili wasije wakafanya tena makosa mengine ambayo yanaweza kuja kuwadhuru baadaye.”
 
Poleni watoto wa korogocho. Mzazi asipokuwa na hekima ni mateso na maumivu kwa watoto. Ona sasa, serikali kulazimishia kuwa kuna korona, wakati haiko kwa kiwango ambacho wanatakachotaka tuamini, ndiyo matokeo yake haya. Kenya wanawaumiza wananchi bila ya sababu yoyote ile. Hata ukiangalia kwa umakini hamna wanachofanya, kupima wameacha, lockdown siyo lockdown, curfew siyo curfew. Hawajielewi. Ona sasa madaktari wana siku ya 17 wamegoma. Hospitali za umma hazitoi huduma. Shida juu ya shida. Sasa watoto wananyanyaswa mtaani.

Hawajui ya kuwa kufunga kila kitu unachodhani kinafungika siyo ndiyo kusema utazuia maambukizi kabisa. Huo ni mtazamo tu.


 
Tony254 Njoo huku uone. Matatizo yote haya yanaletwa na ile timu mkali wa mifupa nyikani.
 
Nchi yenye GDP kubwa EA ,mtapigwa makwenzi ya kichwa na Mungu mpaka muache unafiki.Aya we mk.....u 254 njoo ujibu tuhuma izi.ikiwezekana tuletee na vidata vya ku Google
 
Watakuja soon apa wako tempered vibaya na matusi yao ya "https://jamii.app/JFUserGuide https://jamii.app/JFUserGuide" wakijiona ni wamarekani kumbe hamna kitu.
 
Back
Top Bottom