United African University of Tanzania

BABA E's

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
354
Reaction score
135
WanaJF kuna kijana wangu kachanguliwa kwenye hichi chuo (UAUT), kipo kigamboni, inaonekana ni chuo kipya kabisa.

Kama kuna mtu anakielewa vizuri tuelimishane ubora wake kama kweli panafaa au nayo ni ya kata!.
 
Hakiwezi kuwa cha kata kwa sababu hakina influence na chama cha siasa,
 
chuo cha wakorea hicho wacha aende ajionee mwenyewe
 
Ni chuo poa saana,ingia kwenye website yao ujionee..,wako internationally sanaa,shida ni hiyo tuition fees yao tu!!!
 
college of business ni 2,500000,college of engineering and technology ni 2,900000...,accomodation total 415,000
 
Leo nimefika Feri nikakuta bango limeandikwa UAUT bila kirefu wala maelezo yoyote, kumbe ndio hao! Hicho chuo kiko maeneo gani wakuu; mimi niko huku Kigamboni lkn sijawahi kukiona na ndio leo nakisikia, tena humu JF.

Tusije kuingizwa mjini.

Vv
 
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Taaluma na Tafiti), Profesa Jo, Do Hyun amewaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa, chuo kiko tayari kuanza masomo na kwamba sasa kiko katika harakati za kusajili wanafunzi wenye sifa zinazotakiwa na kuongeza kuwa, kwa kuanzia, chuo hicho kitachukua wanafunzi 120, ambapo kila moja ya kozi hizo mbili itachukua wanafunzi 60.


Amesema chuo hakitasajili wanafunzi kwa misingi ya dini zao, bali sifa za kitaaluma na kuongeza kwa mwaka wa masomo unaoanza, chuo kitatoa ufadhili kwa wanafunzi 53 na watarajiwa wa ufadhili huo watatakiwa kuwa na vigezo vilivyowekwa. Ufadhili huo umewekwa katika makundi ya aina mbalimbali.

Akielezea zaidi, amesema wanafunzi katika chuo hicho watapata fursa ya mafunzo kwa vitendo kwa muda wa miezi sita nje ya nchi na kwamba hiyo itasaidia kuwajengea mtazamo mpya wa dunia, kujifunza zaidi kivitendo pamoja na kujenga mtandao kwa faida yao na nchi kwa ujumla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…