PostGE2025 United Kingdom of Tanzania? Why Samia appointing her daughter and son-in-law as ministers is a terrible idea that Mugabe himself later regretted

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Call it the United Repugnance of Tanzania under queen Samuya Sulubu Hassarani
 
Anachotaka kusema watu msibaki kushangaa bali chukueni hatua madhubuti kumzuia .....
Umenielewa Mkuu, kwanini ushangae jambo ambalo liko wazi, nikama ulitegemea matokeo tofauti.

Ni kama TZ imekuwa jamhuri 2025, kumbe ipo kitambo na hichi tunachoona ndio matunda, sasa hatukuuona mti ukikua?
 
Umesema vyema mkuu.
 
“Ukitaka kumuua mbwa, mpe jina baya.” Hicho ndicho kinachoonekana sasa. Tunaweza tusikubaliane kwenye hoja fulani, lakini angalau tukubaliane kwenye hoja itakayotufikisha kwenye Tanzania yenye amani, haki na upendo. Mpaka sasa, taasisi zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinamtambua Mh. Samia Suluhu Hassan kama Rais wa Tanzania. Kwa mamlaka aliyopewa, wananchi wanapaswa kutii na kutekeleza maelekezo yake kwa maslahi ya taifa, si vinginevyo. Iwapo baadhi yetu tunaona mambo fulani hayapo sawa, tunaweza kuyatoa kwa njia inayostahili na kwa hatua zinazokubalika kisheria.

Kama tulitumia nyundo kupigilia msumari, basi tusitumie nyundo hiyo hiyo kugongomelea pini ya kubandika karatasi kwenye ubao wa matangazo.

Unajiuliza kwa nini amemteua mwanawe au mkwewe? Tatizo lipo kwenye kuwepo kwa watu ambao uso kwa uso wanacheka na wewe, lakini ndani wana chuki na wako tayari kuvuruga hata mambo mema unayokusudia kwa wananchi. Ni muhimu sana kuchagua watu wanaoaminika na wanaoweza kufanya kazi kwa uadilifu. Pia, ni mapema mno kuhukumu utendaji wa waliopewa nafasi za uwaziri. Tuwape muda tuone namna watakavyotekeleza majukumu yao.

Naomba, chonde chonde, tuwekeze nguvu na fikra zetu katika kuijenga Tanzania yenye amani, haki na upendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…