Hapana Fidel, classroom itakuwapo UDSM ila lecture zitakuwa zinatoka India tena ni LIVE LECTURES, unamuona lecturer muda huo huo anapokuwa anafundisha, naye anakuona. Ukitaka kuuliza swali unanyoosha kidole na anakuchagua uulize. Ni kupitia big screen kwa mfumo wa Videoconference. Nilipoliona hili tangazo ilibidi niende mwenyewe kuona itakavyokuwa inafanya kazi, na bahati nzuri muda huo kulikuwa kuna lecture inaendelea from India kwenda kwa wanafunzi wa Kigali. Nimesema LIVE LECTURES ili uone kuwa hii ni tofauti na online degrees ambazo watu huwa wanafanyiana paper wakati mwingine, lakini kwa hii usipoingia class umeumia.