Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Mpango wa kuanzisha elimu ya chuo kikuu Africa ya Kati ulianza 1857 -1965 na mshinikizo huuo uliwekwa na wamisionary hasa wa kanisa la Anglicana, kupitia vyuo vikuu tanzu vya Oxford, Cambridge, Durham na Dublin. Mpango wa kueneza dhehebu la Kikatoliki ndiyo iliyopelekea kuhamisha madaraka kwa maaskofu sehemu walipo kuliko kusubiri maamuzi kutoka Vatican. David Livingstone akiwa mwanzilishi wa mipango hiyo na missionary zilizoanzishwa zilikuwa Zanzibar na Nyasaland ambayo illitwa Malawi baadae. Lengo kubwa la shule hizo lilikuwa kupata mapadre wa Kiafrika.
Kanisa la Anglicana Zanzibar.
Sosayati hiyo iliundwa na kushinikizwa na walimu aliopewa Livingstone baada ya ziara yake ya Afrika, pamoja na kuwa ziliundwa kushabihiana na university na vyuo vikuu mama nilivyovitaja awali lakini ilipokea michango ambayo haikuvishirikisha vyuo hivyo kutoka kwa waliovitakia mafanikio mema. Malengo makuu ya kuanzisha vyuo hivyo yalikuwa (1). Kueneza dini Afrika ya Kati (2) Kupigania kumalizika kwa biashara ya utumwa.
Katika kutekeleza malengo hayo, iliamuliwa kupeleka mission ambazo zitaongozwa na maaskofu katika Afrika ya Kati. Charles Mackenzies alikuwa amejikita katika kuzunguka na kuchunguza maeneo ya kuweka mission, hii ilikuwa 1860-1861. Alizunguka Zambezi mpaka Milima ya Shire. Safari ya kwanza ya upelelezi haikuwa na matukio makubwa. Eneo alilochagua lilikuwa karibu na Ziwa Nyasa (Ziwa Malawi), alipata malaria kali sana na hii ilipelekea kifo cha Askofu Mackenzie.mnamo 31 January 1862, pamoja na wenyeji wengine wengi pamoja na wamissionary wachache. Mazungumzo yaliyofanywa mwanzoni yalileta matunda madogo sana, pia mahitaji yao ya kujikumu inawezekana yalikwisha au yaliharibiwa kwenye kipindi cha njaa kali. Hali hii ilipeleka hatua za kuondoka katika eneo lile na kuliacha kaburi la askofu na wamissionari wengine. Maendeleo yalielekea zaidi Zanzibar na miaka mingi ilipita kabla ya wamissionari kurudi katika eneo lile hatima Askofu Tozer, ambae alichukua nafasi ya Mackenzie alianzisha mission katika mapingamizi magumu.
Mission ya Zanzibar.
Baada ya Askofu Tozer kuchukua madaraka ya Askofu Mackenzie, alihamia Zanzibar mnamo mwaka 1864. Pale alipokelewa kwa uchangamfu mkubwa, alipata mapokezi ya kirafiki kutoka kwa Waarabu na Waafrika walioishi pale. Alianzisha mipango mingi, ikiwemo kuanzisha shule ya mission. Shule ya Mtakatifu Andrew ilijengwa Kiungani. Kazi za kwanza za mission katika Zanzibar zilikuwa ni pamoja na kuwaangalia watoto wa shule na kukomboa watumwa. Makazi ya Mbweni yalianza 1871- hapa waliwekwa watumwa waliokombolewa ili waanze maisha mapya. Chrismtas ya mwaka 1873, jiwe la msingi la Kanisa la Kritu liliwekwa na soko la watumwa lilifungwa miezi sita kabla ya tarehe ya makubaliano. Kanisa lilimalizika na misa ya Chrismtas 1880 ilisherehekewa pale.
Mipango ya upanuzi.
Ilipofika 1874, Tozer alirithiwa madaraka na askofu Edward Steere, ambae alifufua mipango ya kupeleka mission katika Ziwa Nyasa. Kuliko kujaribu njia ngumu ya mto ambayo haikuleta mafanikio kwa waliotangulia, waliamua kwenda Ziwa Malawi, safari hii kwa kupitia barabara wakiendeleza mfumo wa mission na vituo kuelekea kwenye ziwa. Sehemu za muhimu katika hizi zilikuwa Magila ambayo ipo Muheza, Tanga na Masasi; Magila ilichaguliwa baada ya sehemu ya kwanza iliyofikiriwa ambayo ni Vuga Lushoto , mji mkuu wa ufalme wa Kilindi kukataliwa na chifu wa Kilindi kutokana na wasi wasi aliokuwa nao. Eneo la mission ya Masasi lilichaguliwa na Waafrika waliobatizwa na wamissionary waliwapa motisha wa kurudi makwao ambako walikamatwo katika biashara ya utumwa; pamoja na habari za uhakika kuwa sehemu kanisa lilipo siyo sehemu halisi waliyotoka lakini walikuwa na furaha kuanza maisha pale kwakuwa palifanana na maeneo waliyotoka. Kupitia njia hii, wamissionari wawili Charles Janson na William Johnson, kwanza walifika kwenye ziwa; Janson alifariki pale, lakini alitoa jina lake kwa meli ya UMCA iliyowekwa kufundisha dini katika ziwa. Aliyemrithi Steer Charles Alan Smythies, aliweza kusafiri zaidi Afrika katika kazi za kimission. Aliweza kusimamia ujenzi wa Kisiwa cha Likoma, katika ziwa kama station na pia aliweza kujenga diosisis na kuweka miji na askofu na cathedral. Mtakatifu Peter, bado linasimama katika karne ya 21.
Mipango mingine madhubuti ya Smythies ilikuwa kipaumbele cha kuibadilisha Afrika kuwa na mapadre wake yenyewe, mapadre waafrika kwa waafrika, ilibidi kufanya mikakati ya kuwafundisha Kiungani.
Mipango yao iliendelea ikiwa Zanzibar ikiwa makao makuu, Likoma na upande wa Tanzania Bara, mpaka mwaka 1910, ambako kazi ilianza ya Rhodesia ya Kaskazini (Zambia ya sasa). Kazi za kimissionary ziliendelea katika sehemu hizi kwa nusu ya karne ya 20, shughuli zilikuwa pamjoja na huduma za matibabu na elimu na pia kufundisha dini. Umuhimu mkubwa ulionekana katika karne ya 20, pamoja na maaskofu wake akiwemo Frank Weston na John Edward Hine. Wazungu wengine waloonekana kazi hizo, alikuwemo mwandishi wa vitabu Robert Keable, na askofu Chauncy Maples, ambao walijiunga na UMCA kama archdeacon na baadae kuwa Askofu wa pili wa Likoma kabla hajazama kwenye ziwa. UMCA baadae walitengeneza meli iliyokuwa na jina lake kama walivyofanya kwa Charles Janson meli hiyo iliitwa SS Chauncy Maple, ilijengwa mwaka 1899, inaaminika ilikuwa meli ya zamani kuliko zote katika Afrika.
Chauncy Maple na William Percival Johnson