Cecil J
JF-Expert Member
- Oct 12, 2023
- 434
- 1,024
Hivi sasa ni saa 1 na dakika 38, nawasalimu wanajukwaa. Huku niliko hali ya hewa ni ya kiubaridi kidogo, anga limetandwa na kiza na nyota kadhaa zimeanza kuonekana.
Narejea kwenye mada, kwa wale ambao hawamfahamu mhusika wa kubuni anayefahamika kwa jina la Alex Mahone naanza nao hivi; Alex Mahone alikuwa mhusika wa kubuni kwenye series ya Prison Break iliyotoka kwa mara ya kwanza Agosti 29, 2005 na msimu wake wa Tano (5) kutolewa mwaka 2017 Mei, 30.
kutoka upande wa kushoto ni, Paul Kellerman, Lincoln Burrows, Michael Scofield, Alex Mahone, na Brad Bellick
Series hii inawahusu ndugu wawili walio-share baba ambao ni Michael Scofield na Lincoln Burrows. Michael Scofield ni mhandisi wa Ujenzi (Civil Engineering) akiwa na Elimu ngazi ya Uzamili (Masters), huyu alikuwa kichwa mno. Kwa upande wa pili Lincoln Burrows (half brother) wa Michael Scofield yeye ni mtu ambae kwenye upande wa Elimu hajaandikiwa sana, huyu alikuwa akijihusisha na uhuni na biashara kadhaa za uuzaji wa dawa za kulevya.
Michael Scofield.
Lincoln Burrows alioa mke ambaye walikuja tarakiana nae na alipata mtoto mmoja wa kiume aliyemwita jina la Lincoln Junior, kwa kifupi alipenda kumuita LJ.
Lincoln Junior "LJ" Burrows
Lincoln alikopa dola za Kimarekani elfu tisini ($ 90, 000) ili kulipia karo ya shule ya mdogo wake Michael kutoka kwa bosi wake Crab Simmons. Ilipofikia muda wa kulipa hakuwa na pesa na hivyo akapewa kazi ya kumuua Bw. Terrence Steadman ambaye alikuwa kaka wa makamu wa Rais. Lincoln hakuwa na chanzo kingine cha mapato hivyo akaikubali hiyo kazi, haifahamiki mara ya mwisho Burrows alitumia nini ila alikuwa "high" kwa kuzidiwa na alichotumia (madawa, pombe?).
Lincoln "Linc the sink" Burrows
Lincoln Burrows aliisogelea gari ya Terrence Steadman lakini alipotaka kufyatua risasi alishangaa kuona tayari alikuwa akitazamana na maiti, aliyeua ni nani? Bado haikufahamika.
Baada ya siku kadhaa Lincoln anakamatwa na kuwekwa kwenye gereza la Fox River (level-one-maximum security) lililokuwa katika eneo la Joliet huko Illinois. Taarifa za kukamatwa kwa Lincoln zilipofika kwa Michael Scofield aliamua kufanya uchunguzi wake yakinifu na baada ya hapo alimaliza mpango wake kwa kuchora tattoo mgongoni.
Tattoo ya Michael Scofield ilichorwa na mwanadada Syd, kwasasa tattoo hii kwa bei yake mtaani inagharimu kama dola elfu 20 hivi!
Syd, mchoraji wa tattoo
Tuishie hapo kwenye stori, kuna huyu mhusika mwingine aliyekuwa akifahamika kwa jina la Alex Mahone. Mahone ndie mhusika aliyewekwa angalau kuleta usawazo na upinzani kwa Michael Scofield (Mastermind), shida ya huyu jamaa ni moja tu, yeye alikuwa anatumia madawa fulani ili kukaa sawa kiakili. Ukiangalia kwa jicho la pili ni kama Fox walikuwa waki-push na ku-glorify madawa ya kulevya