Ununuaji wa korosho kupitia stakabadhi ghalani

Ununuaji wa korosho kupitia stakabadhi ghalani

Bartazar

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2011
Posts
1,048
Reaction score
569
Kuna tetesi kuwa wakulima wa Tandahimba na Newala watagoma kuuza korosho zao msimu huu kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa madai kwamba mfumo huo unawanyonya. Kwa hiyo wamekubaliana kuwa wao wenyewe watapeleka korosho mnadani! Itakuwa hivi: Watatafuta soko na watakodi magari kwenda mnadani wenyewe. Kwa hiyo, kila kaya yenye korosho itamtoa mwakilishi mmoja!

Mfumo wa stakabadhi ghalani umekuwa ukilalamikiwa sana kwamba umejaa ubabaishaji na una harufu ya ufisadi, hali ambayo imepelekea wakulima kupoteza imani kabisa kwa mfumo huo, ambao unaonekana kuwa na maslahi kwa viongozi kuliko wakulima wenyewe!
 
Back
Top Bottom