Katika tamko la Waziri wa Nishati na Madini la kudhibitisha kufungwa kwa mjadala wa Serikali kununua mitambo ya Dowans na badala yake Serikali inafanya mpango wa kununua mitambo mipya yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 150,Waziri alielezea kushangazwa kwake na kamati ya Bunge kukataa kununuliwa kwa mitambo ya Dowans iliyotumika lakini siku za nyuma ilikubali kununuliwa kwa mitanbo ya IPTL ambayo nayo imekwishatumika.
Je mitambo ya IPTL ilikuwa na mlolongo wa matatizo kama ilivyo ya Dowans na kama ni tofauti Waziri hajui,wana JF karibuni tuelimishane.

Waziri alielezea kushangazwa kwake na kamati ya Bunge kukataa kununuliwa kwa mitambo ya Dowans iliyotumika lakini siku za nyuma ilikubali kununuliwa kwa mitanbo ya IPTL ambayo nayo imekwishatumika.
.
Mazingira ya IPTL na Dowans hayana tofauti kabisa. Nadhani Waziri amejieleza vizuri sana.
1. Wote IPTL na Dowans wameingia nchini kwa matatizo.
2. Mitambo yote ni iliyokwisha tumika. Infact ya IPTL ni michakavu zaidi.
3. Wote walikuwa na mikataba na Serikali.
4. Mitambo yote inadaiwa na Benki.
5. Hapa inaonyesha wazi kuwa wakina Sitta, Mwakyembe na Shellukindo ni wanafiki kwa kuwa na double standards. Inakuwaje wanatumia hoja ya Sheria ya Ununuzi wa Umma kukataza ununuzi wa mitambo ya Dowans wakati huo huo wanahimiza kununua kwa IPTL. Hapa lazima tumuamini Waziri kwa kuwa ame quote Hansard ambayo huwa haisemi uwongo.
6. Mwakyembe aliudanganya umma kuwa management ya Tanesco haikupata kibali cha Board yake wakati Waziri Ngeleja anasema Bodi ilitoa kibali. Hapa lazima tumuamini Waziri mwenye dhamana ya Shirika hilo.
7. Shellukindo na Mwakyembe walikuwa katika kamati hiyo na Sitta alikuwa Spika. Kwa hiyo kama wanakubali walikuwa mabwege mwaka mmoja tu uliopita mpaka wakapigia makofi uamuzi wa kununua mitambo ya IPTL jee huo ujajanja wa hivi sasa wameupata wapi?
8. Walisema Tanesco na Kamati ya Zitto walikula mlungula kwa kutaka kukiuka sheria.. Kwa vigezo hivyo hivyo na Akina Mwakyembe inaonyesha nao wamekula mlungula kwa IPTL kwa kukiuka sheria hiyo hiyo. Unaona matokeo ya mambo ya kufuatana futana sasa siri yao nayo imefichuka.
9. Serikali iache woga na ichukue maamuzi kwa maslahi ya taifa. Ikiwa Bunge litaleta maneno basi Rais avunje Bunge warudi kwa wananchi. Kwa mtindo wa sasa wa Primaries za CCM 75% ya wabunge hawarudi. Kwa hiyo hawana msuli wa kupambana na serikali.
10. Spika Sitta kurudi kwake Bungeni kama Spika kuna wasiwasi asilimia 75 kutokana na anavyotaka kuendesha yeye kila kitu.