Ununuzi wa bidhaa online (JUMIA, KAYMU)

Dupe

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2013
Posts
1,668
Reaction score
811
Nimependa staili za hawa jamaa wa JUMIA, huwa unaweka order online na wanakufikishia mpaka ulipo na utalipa hela ya bidhaa baada ya mzigo kufika mkononi mwako, hawa ndio JUMIA kwakweli huduma zao safi sana?

Jana tu niliweka order ya Sim ila leo napigiwa sim mzigo ushafika mjini ni mimi kwenda kuchuKua tu.

KAYMU:- Hawa jamaa utaratibu ni uleule lakini wao unalipa kwanza pesa ndipo wanakuletea mzigo na ukifika usipoupenda unaacha na hela yako utarudishiwa kwa njia uliyotumiwa ? japo sijawahi kujaribia kuomba na kufika kwa bidhaa zao ila hama wangeweka kama JUMIA tu ingekuwa poa sana.
 
Hivi Tanzania ukiagiza mzigo mnapelekewa wapi maana Uku tunaletewa hadi mlangoni na nyie uko Hamna anuwani za Makazi ya kueleweka
 
Hivi Tanzania ukiagiza mzigo mnapelekewa wapi maana Uku tunaletewa hadi mlangoni na nyie uko Hamna anuwani za Makazi ya kueleweka

Kwa niaba ya watanzania makabwela I take this as offence against Malofa.

Tutake radhi, vinginevyo tunakushusha kibusha huko huko Denver unapopiga box.

Blalifuli!!
 
Kwa niaba ya watanzania makabwela I take this as offence against Malofa.

Tutake radhi, vinginevyo tunakushusha kibusha huko huko Denver unapopiga box.

Blalifuli!!

Tena kidafu kilekile cha mpiji kwa minaz iliyo karbu na bahar kidafu chake hatar
 
yote uliosema ni kweli! ngoja niwaulize kama wanaweza kunletea SAMAKI hapa home!
 
Tatizo Nguo ya 5000 mnauza 19500.. nani Atanunua sasa
 
Kaymu pia wanakuletea ulipo,unalipa hapo hapo
 
Hivi Tanzania ukiagiza mzigo mnapelekewa wapi maana Uku tunaletewa hadi mlangoni na nyie uko Hamna anuwani za Makazi ya kueleweka

Ha ha ha huu ukweli wenyewe hawapendi kabisa kuusikia
 
Kaymu inanjia tatu za ulipaji.
WAweza kulipa pale unapoletewa mzigo, unaweza kulipa kwa mobile money (airtel money, tigo pesa na mpesa) na pia waweza ukaweka order na kwenda kuuchukua mzigo mwenyewe kwa muujazi kukwepa gharama za usafirishaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…