JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Toleo la awali ni mauzo ya hisa na dhamana kwa umma kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kukusanya mtaji. Kwa lugha nyingine inajulikana kama IPO (Initial Public Offer) Mauzo hayo yana kipindi chenye ukomo.
Baada ya hapo, kama mwekezaji anataka kuwekeza kwenye kampuni hiyo atatakiwa kwenda kwenye soko la pili kupitia madalali wa soko la hisa.
Kwa toleo la awali la ubinafsishaji wa hisa za Serikali kwenye mashirika ya umma kuna vivutio maalum kwa Watanzania. Wasio Watanzania hawaruhusiwi kununua hisa hizo.
Kama ilivyo sera ya ubinafsishaji, Serikali imekuwa inatenga kiasi cha hisa kwa Watanzania wakati inapouza hisa kwa wawekezaji wa nje kupitia Tume ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC).
Kwa matoleo mengine ya awali Watanzania wanapewa kupaumbele wakifuatiwa na raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na hatimaye raia wengine.
Kwa mujibu wa Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana kikomo cha wawekezaji wa nje kwenye masoko ya mitaji sii zaidi ya 60% ya hisa za kampuni. Katika kiwango hiki wawekezaji wa nje na wa ndani wanaruhusiwa kuwekeza.
Kiasi cha 40% kinachobakia ni ajili ya wawekezaji Watanzania pekee. Uwekezaji kwenye dhamana za Serikali ni kwa ajili ya Watanzania pekee.
Upvote
1