JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Takriban asilimia 80 ya ardhi inayotumiwa kwa kilimo Tanzania inatumiwa na wakulima wadogo wadogo wanaolima kwa ajili ya chakula.
Wakulima katika maeneo mengi ya Tanzania wanakumbana na changamoto kubwa ya unyang'anyi wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji hasa wa watu binafsi hali inayowalazimu kukosa maeneo ya kutosha kuendesha shughuli zao ili kumudu gharama za maisha.
Aidha changamoto nyingine zinazowakabili ni ukosefu wa pembejeo pamoja na kukosa taarifa muhimu kuhusu kilimo hasa mabadiliko ya tabia ya nchi.
Jamii za Wamasai ndizo hukumbwa na unyang'anyi wa ardhi sana Tanzania. Wengi wao huishi maeneo ya hifadhi hivyo hunyang'anywa ardhi kwa ajili ya kupanua maeneo hayo ili Serikali iingize kipato zaidi kupitia utalii.
Mwaka 2017 Wamasai walifukuzwa kwenye hifadhi ya Serengeti hali iliyopelekea kukosa makazi pamoja na malisho ya mifugo yao.
Upvote
0