Kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara ya wanafunzi wanaosoma katika chuo hiki.Matatizo hayo ni pamoja na kutokusikilizwa kwa matatizo yanayowakumba chuoni hapo,kucheleweshwa kupewa mikopo yao hata mara baada ya kusaini huku wakiambiwa hawatakiwi kuonekana vikundivikundi wakijadili mambo ya chuo eti wanapanga maandamano,na la mwisho ambalo mi ni shahidi nalo ni huduma itolewayo na zahanati ya chuo!mm mwenyewe nilienda kupima malaria nikaambiwa sina ila hali ikaendelea kuwa mbaya na nilipoenda zahanati nyingine nikagundulika nina malaria 3 na typhoid nyingi!na utafiti unaonyesha inasemekana vyao havifanyi kazi.sasa nawauliza hili ndio dhumuni la chuo hiki!mbona huu ni unyanyasaji kwani wanafunzi hulipia huduma hii ya matibabu