DOKEZO Unyanyasaji kwa wanawake uliokosa mtetezi kwa familia za kijijini

DOKEZO Unyanyasaji kwa wanawake uliokosa mtetezi kwa familia za kijijini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

ginyisi

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2023
Posts
287
Reaction score
465
Habari wakuu

Niende moja kwa moja kwenye mada...nimekutana na kijana mmoja akawa ananisimulia kuhusu unyanyasaji anaopitia mwanamke hyu kutoka familia za kijijini ukweli inasikitisha sana, kisa hichi kimenifanya niamini kuwa huko vijijini kuna wanawake wanaopitia mateso na manyanyaso kama haya...ni hivi.......

Mzee ni mtata kweli kweli yaani hazuiliki kwa yeyote katika maamuzi yake hali ambayo humfanya awe huru kumpiga mke wake atakavyo na hakuna wa kuingilia hata mamake mzazi hamsikilizi...ilifikia wakati huyu mama alitakaga kujinyonga lakini hakufanikiwa ndipo ndugu zake wakaingilia kati na kwenda kumshitaki serikali ya mtaa....

Alivoitwa yule mzee alikuwa mpole na kuomba radhi ili mambo yasiwe mengi....wakakubaliana aandike barua ya kukiri kutompiga tena na akirudia watamchukulia hatua kali zaidi.....basi wakatoa nakala moja ikaenda upande wa ndugu mwanamke na nyingine ikabaki serikali ya mtaa na nyingine wakabaki nayo....lengo ni kutafuta amani....

Lakini haikufanikiwa kwani baada ya mda mzee hyu alianza kumshinikiza mwanamke bila kuzileta barua hizo zote hakutakuwa na amani kwenye nyumba ile.... na kweli mwanamke akakubali kwenda kuchukua nakala zote na kumkabidhi mzee yule akiwa na imani ndio njia sahihi ya kuileta amani lakini hii ndo ilikuwa sawa na kujichumia fimbo.....

Mzee alipambana kurudisha uhuru wake na akafanikiwa na akaendelea kumpiga kila kosa ni mkanda mashine unatembea/kumpiga mbele ya watoto mpaka anajisaidia mbele ya watoto mzee hakuwa na huruma ata kidogo kumpiga kumchania nguo kumburuza yaani ni vitu vya ajabu Mara vitisho vya kumuua na kumwambia ikiwa utanishtaki popote basi nitakimbia na kukuachia watoto peke yake na ataenda kumloga awe chizi.

Huyu mama alishawahi kuondoka lakini alirudi kwa ajili ya watoto na mwanamke hawezi tena kuondoka kwa sababu anawapenda sana watoto wake anasema bora afe katikat ya watoto wake....huyu mama amekuwa ni mtu wa kulia kila kukicha kutokana na anachofanyiwa na mume wake.......

Ushauri wako utasaidia sana kumuokoa mwanamke huyu kwenye manyanyaso haya...ahsanten.
 
'Bora kufa kwenye hali hiyo kuliko kuwaacha watoto'! Hapo ndipo anapokosea. Akifa atawatetea vipi? Aondoke, hakuzaliwa hapo, awaache watoto, huyo mume kama atawatesa, serikali iingilie.
 
Ni sahihi matendo haya yapo sana kwenye jamii za vijijini.

Umenikumbusha mbali sana.

Sasa hiyo Gavo ya mtaa walikubali vipi kukabidhi barua irudishwe kwa mtuhumiwa?
 
Hao watoto mbona inaonekana km ni wadogo sasa atafika kweli kwa mwendo huo, hukko serikalini alikoenda hata km amechukua makaratasi ya kukiri kutompiga tena viongozi si ni walewale? Arudi awaambie amepoteza wampatie nakala ya makubaliano. Mzee pengine ameshamfanya msukule kwa waganga atafute kanisa afanyiwe maombezi. Ndugu zake si wamsaidie?
 
Back
Top Bottom