Messenger RNA
JF-Expert Member
- Jul 24, 2022
- 1,411
- 3,712
Grace Kuria
Wasichana 85 wa Kenya wamepoteza maisha katika muda wa siku 90 zilizopita, na takriban 1,000 kurejeshwa makwao, hasa kutoka Saudi Arabia.
Haya yalibainishwa na mteule wa Kenya katika nafasi ya Waziri wa Masuala ya Kigeni Dkt. Alfred Mutua, ambaye alisema wasichana hao walinyanyaswa walipokuwa wakitafuta kazi.
Dkt. Mutua alikuwa akijibu swali wakati alipokuwa akipigiwa kura Bungeni, kuhusu hatua ambazo angeweka kuhakikisha wafanyakazi hao wahamiaji wamepewa mikataba katika ajira, wanalindwa, na wanafurahia kikamilifu haki wanazopewa.
"Nimeangalia suala hili, na nimeona kushindwa kwa utaratibu katika mifumo, kutoka kwa jinsi wanavyoajiriwa hapa .... na jinsi wanavyoruhusiwa kufanya kazi wanapofika Saudi Arabia na nchi nyingine."
Mteule huyo aliahidi kuwa iwapo ataidhinishwa, atashirikiana na mamlaka husika, kuruhusu Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai kusafiri naye hadi Saudi Arabia, kuchunguza kila kifo kilichotokea.
"Ili kila mtu aliyehusika katika vifo hivyo ashtakiwe."
Mnamo 2021, Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya ilisema Wakenya 89, wengi wao wakiwa wafanyakazi wa nyumbani walifariki nchini Saudi Arabia katika miaka miwili iliyopita. Hata hivyo vilihusishwa na mshtuko wa moyo.
BBC