Alfredwanka
New Member
- Jul 16, 2021
- 2
- 2
Kwa mujibu wa Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto, Mkataba wa Afrika kuhusu Haki na Ustawi wa Mtoto, Sera ya Maendeleo ya Mtoto na Sheria ya Mtoto Na. 21 ya 2009; inaeleza kuwa, Mtoto ni mtu yeyote mwenye umri ya miaka kumi na nane (18). Watoto wote wanazo haki zao za msingi bila kujali tofauti zao, kama zilivyoainishwa katika Makubaliano ya Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Mtoto (1989) ambazo ni haki ya kuishi, haki ya kuendelezwa, haki ya kulindwa pamoja na haki ya kushiriki. Hivyo kwenda kinyume na matakwa ya haki hizo, ni kutekeleza unyonyaji na unyanyasaji dhidi ya watoto.
Katika maeneo mengi nchini, suala la unyonyaji na unyanyasaji dhidi ya watoto, limekithiri hasa katika maeneo mengi ya vijijini. Hii ni kwa sababu udhibiti wake umeelekezwa katika baadhi ya vikundi, taasisi au mashirika ambayo yanajishughulisha na haki za watoto na haki za binadamu kwa ujumla na si jamii nzima ilihali watekelezaji ama wahusika wakuu wa jambo hilo ni wanajamii wenyewe, ambao mara nyingi hulifumbia macho ama kuliongelea jambo hili katika ujazo dhaifu aidha kwa kuhofia kuaibika, kuumbuka au kudharirika kwa baadhi ya wahusika.
Licha ya kuwa, suala la unyanyasaji na unyonyaji dhidi ya watoto huweza kutokea mahali popote, lakini kwa kiasi kikubwa maeneo yanayoathirika zaidi na kadhia hii ni maeneo ya vijijini, na hii ni kwa sababu zifuatazo:
Kukithiri kwa imani za kishirikina; hii ni kutokana na idadi kubwa ya watu waishio maeneo ya vijijini kuamini ama kutegemea imani potofu ili kufanikisha ama kutatua maswala mbalimbali yanayowakabili. Hii imepelekea kuwapo kwa baadhi waganga wa jadi ambao huwapa wateja wao masharti tata na chonganishi ili kukamilishiwa ama kutatuliwa shida zao kama vile, kushiriki ngono na wazazi, ndugu na hata watoto.
Kwa mujibu wa Sera ya Ulinzi wa Mtoto (2019) inaeleza kuwa, unyonyaji wa mtoto ni pamoja na kufanya au kumlazimisha mtu mwingine kufanya kitendo au vitendo vya unyonyaji dhidi ya mtoto. Kwa mfano katika kituo cha kulelea watoto (Jina linahifadhiwa) kilichopo mkoani Katavu, wanalelewa mabinti wawili ambao wamekumbwa na kadhia hii huku mmoja akiwa ameingiliwa kimwili na baba yake mzazi na mwingine akiwa kafanyiwa hivyo na kaka yake.
Ulevi wa pombe pamoja na madawa ya kulevya kama vile marijuana; Katika maeneo mengi ya vijijini kumekuwepo na tabia ya wazazi kwenda katika vilabu vya pombe na watoto wadogo migongoni mwao na wakati mwingine huwanywesha pombe licha ya kuwa umri hauwaruhusu.
Kwa mujibu wa Sera ya Ulinzi wa Mtoto (2019), hii ni aina nyingine ya unyanyasaji dhidi ya mtoto uliopo katika kundi la unyanyasaji wa kihisia ambapo, mzazi humtelekeza mtoto kwa kushindwa kumpa mtoto (ambapo wazazi wako katika nafasi ya kufanya hivyo) mazingira ambayo yanakubaliwa kitamaduni kuwa muhimu kwa ukuaji wake kimwili, kihisia na ustawi.
Lakini pia matumizi ya marijuana na madawa mengine ya kulevya huweza kumchochea mhusika kushiriki ngono, kubaka, kumshika mtu sehemu nyeti bila ridhaa yake ambapo wahanga huweza kuwa wa rika lolote hata kwa watoto. Jambo hili ni kinyume na Sera ya Ulinzi wa Mtoto (2019) inaeleza kuwa, unyanyasaji wa kingono dhidi ya mtoto ni pamoja na kumtumia mtoto kujitosheleza kingono kunakofanywa na mtu mzima au na mtoto mwenye umri mkubwa zaidi yake au kijana aliyebalehe.
Hali duni ya kiuchumi; hii ni kwa sababu katika familia nyingi zinazopatikana maeneo ya vijijini zinakumbwa na ukata hivyo kuzifanya ziishi katika maisha duni. Ili kujikwamua na hali hiyo, baadhi ya familia zilizojaaliwa kuwa na watoto wa kike, huwaozesha bila kujali kigezo cha umri lengo likiwa ni kujipatia mali ili kujikwamua kutoka katika hali duni ya maisha. Kwa mujibu wa Sera ya Ulinzi wa Mtoto (2019) inaeleza kuwa, unyonyaji wa mtoto ni pamoja na kumtumia mtoto kujinufaisha, kwa kazi, kujitosheleza kingono au faida nyingine ya kibinafsi au kifedha.
Suala la elimu; licha ya kuwa huduma za kielimu zimenea kwa kiwango kikubwa hadi kufikia maeneo ya vijijini, lakini bado jamii nyingi hazijalipokea jambo hili kwa mikono miwili hivyo kutokupewa kipaumbele au ujazo wa kutosha. Hii ni kutokana na uhuru wanaoupata watoto kutoka kwa wazazi wao pamoja na kujiendesha wanavyotaka katika suala zima la elimu.
Kwa mfano, mtoto huwa huru kusoma au kutosoma, lakini pia kusoma hadi hatua au darasa fulani. Sera ya Ulinzi wa Mtoto (2019) inaeleza kuwa, unyanyasaji wa kihisia ni pamoja na kumtelekeza mtoto; ambapo mzazi au mlezi hushindwa kumpa mtoto mazingira yanayokubaliwa kitamaduni kuwa muhimu kwa ukuaji wake kimwili, kihisia na ustawi.
Suala la malezi; suala hili pia huweza huweza kuchochea, kusababisha na kuendeleza unyanyasaji dhidi ya mtoto. Wazazi wengi hasa waliopo maeneo ya vijijini bado wamekumbatia aina ya malezi ambayo hulalia upande mmoja. Yaani jinsia fulani hukandamizwa huku jinsia nyingine ikipata ahueni. Katika familia za aina hii, mara nyingi mtoto wa kike huwa mhanga katika hili kwani hushiriki shughuli nyingi za nyumbani kuliko mtoto wa kiume.
Vile vile, wazazi wengi huamini katika udikteta kama njia au mbinu bora ya malezi ambapo watoto huelekezwa kwa kuadhibiwa vikali, kutukanwa ama kujeruiwa. Unyonyaji huu huwa endelevu kwani watoto hujifunza na huyaishi malezi hayo hata katika familia zao pindi wanapojitegemea.
Kwa mujibu wa Sera ya Ulinzi (2019) huu ni unyanyasaji wa kimwili ambao hutekelezwa kwa matumizi ya nguvu dhidi ya mtoto ambayo humsababishia madhara. Kwa mfano kumpiga, kumsukuma, kumuwekea sumu n.k. Vile vile kumwadhibu au kumrekebisha mtoto kwa njia isiyofaa au kumtaka mtoto kufanya mambo yanayozidi uwezo wake au ya kudharirisha ama kumtolea maneno ya kudharirisha.
Suala la uchache au kukosekana kwa vikundi, vyama, mashirika pamoja na taasisi zinazohusika na maswala ya haki za watoto na haki za binadamu kwa ujumla. Hii ni kwa sababu maeneo mengi ya vijijini hukosa msaada kutokana kukosekana au umbali mrefu kati ya maeneo hayo na ofisi za taasisi au mashirika yahusikayo na utoaji wa huduma za haki za kibinadamu.
Hali hii huwafanya waharifu kuwa huru katika kutekeleza vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu. Kwa mfano, yapo baadhi ya maeneo yasiyokuwa na vituo vya polisi, ofisi za ustawi wa jamii n.k. Vili vile, wahusika katika taasisi hizo, kutotembelea mara kwa mara maeneo ya vijijini kwa sababu tofauti tofauti hivyo kuwapa mwanya waharifu kutekeleza unyanyasaji bila kuwapo na vikwazo vyovyote.
Baada ya kujadili sababu zinazopelekea unyonyaji na unyanyasaji dhidi ya watoto, yafuatayo ni mapendekezo nini kifanyike ili walau kupunguza ama kukomesha vitendo hivyo:
Kutilia mkazo suala la elimu; Kwa mujibu wa Shirika la World Vision Tanzania katika kitabu cha "Ulinzi na Usalama wa Mtoto ni Wajibu Wetu Sote" inaelezwa kuwa, wajibu wa wazazi au jamii katika kuhakikisha watoto wanapatiwa haki zao, ni pamoja ni pamoja na kuwaandikisha shule, kufuatilia maendeleo yao shuleni na kuwapatia mahitaji yote ya shule. Kwa kufanya hivyo, kutawasaidia watoto kuzitambua haki zao za msingi pamoja na kutengeneza jamii yenye uelewa mzuri kuhusu haki za watoto na haki za binadamu kwa ujumla na si kuisusia serikali ama kuwaachia watoto uhuru wa kuamua mustakabali wa elimu au maisha yao bila usimamizi wa mzazi.
Kuanzishwa kwa vikundi, vyama, mashirika au taasisi zinazohusika na usimamizi wa haki za watoto na haki za binadamu kwa ujumla hasa katika maeneo ya vijijini. Hii ni kwa sababu, mashirika pamoja na taasisi zinazoshukughulikia maswala ya haki za watoto au haki za binadamu, kutotoa huduma katika uzani sawa baina ya miji na vijiji. Kwani maeneo mengi ya mijini hupewa kipaumbele zaidi huku maeneo ya vijiji kusahaulika ama kupata huduma hafifu.
Hali hii inapelekea ugumu katika kutoa taarifa kwa wakati sahihi pindi matukio ya unyanyasaji dhidi ya watoto yatukiapo. Kwa mujibu wa shirika la World Vision Tanzania katika "Ulinzi wa Mtoto ni Wajibu Wetu Sote" inaelezwa kuwa katika kuhakikisha watoto wanapata haki zao, wazazi na jamii nzima wanapaswa kuwalinda watoto dhidi ya kunyanyaswa, unyonywaji, kutelekezwa, kufanyiwa ukatili na kuchukua hatua pale ambapo haki za mtoto zimevunjwa. Pia kushirikiana na serikali na wadau wengine katika kuhakikisha huduma zinapatikana kwa kiwango stahiki katika maeneo yao.
Kutoa malezi bora kwa watoto; Hii ni kwa sababu, unyanyasaji dhidi ya watoto si tu unatekelezwa na watu wa mbali katika jamii, bali hata katika familia unyanyasaji dhidi ya watoto hutokea. Hivyo familia hasa zilizopo katika maeneo ya vijijini zinapaswa kuachana na dhana ya udikteta katika malezi kwani katika familia nyingi dhana hii imekuwa ikiaminika na kutumika kama silaha ya kuleta heshima au nidhamu katika familia.
Wazazi katika familia zao, wanapaswa kutumia njia bora katika malezi ya watoto huku wakitimiza majukumu yao pasi na kuleta unyanyasaji dhidi ya watoto. World Vision Tanzania katika "Ulinzi wa Mtoto ni Jukumu Letu Sote" Inaelezwa kuwa, wazazi wana wajibu wa kuwahudumia watoto wao na kuhakikizha wanapata mahitaji yao ya mzingi.
Kuziacha imani potofu na kuziishi tamaduni sahihi. Kwa mujibu wa Shirika la World Vision Tanzania katika "Ulinzi wa Mtoto ni Jukumu Letu Sote" inaelezwa kuwa, ili kuhakikisha watoto wanapata haki zao za msingi, wazazi na jamii nzima wanapaswa kuhakikisha kuwa watoto wanashirikishwa, kuongozwa na kuhakikisha watoto wanatimiza wajibu wao kikamilifu ikiwa ni pamoja na kufuata imani, tamaduni sahihi, kuzingatia masomo, kujilinda n.k.
Kwa kufanya hivyo, watoto watakuwa huku wakifuata na kuishika misingi bora ya kiimani na kitamaduni ikiwa ni pamoja na kujilinda. Hali hii itasaidia kujenga jamii isiyoamini au kutegemea imani potofu zinazochangia kwa kwa kiasi kikubwa uvunjifu wa amani pamoja na ukiukwaji wa haki za watoto na haki za binadamu kwa ujumla.
Kuanzisha kwa vyanzo mbadala vya kipato; hii ni kwa sababu maeneo mengi ya vijijini yamebarikiwa kuwa na ardhi yenye rutuba nzuri pamoja na madini, misitu pamoja na vyanzo vya maji. Endapo rasilimali hizo zitatumika katika namna inayofaa kama vile kuanzisha shughuli za kilimo, uvuvi, ufugaji, uchimbaji madini pamoja na biashara basi uchumi katika maeneo hayo unaweza kuimarika na hivyo kuzifanya familia zilizopo katika maeneo hayo kuimarika kiuchumi pamoja na hali ya maisha na si kutegemea mabinti kama mtaji wa familia ama kuwahusisha watoto katika ajira mbali mbali.
Hivyo, swala la unyonyaji na unyanyasaji dhidi ya watoto ni nyeti na pana kwani lipo katika maeneo yote nchini japo hujidhihirisha katika namna tofauti tofauti. Hivyo si sahihi sana kuliacha mikononi mwa taasisi au mashirika ya kiserikali na yasiyokuwa ya kiselikali pasi na kuishirikisha jamii katika namna inayofaa. Hii ni kwa sababu ulinzi wa haki za mtoto huanzia katika ngazi ya chini kabisa ambayo ni mtu mmoja mmoja kisha familia zilizopo katika jamii husika. Hivyo ni vema kuwepo na muunganiko ama ushirikiano chanya kati ya mtu na mtu, familia na familia kabla ya kufikia hatua za juu zaidi, kwani jambo hili litasaidia kupunguza kwa kiasi fulani kumaliza kabisa tatizo la unyanyasaji na unyonyaji dhidi ya watoto.
MAREJELEO
Sera ya Ulinzi wa Mtoto. Toleo 2.2 Februali 2019.
World Vision Tanzania. Ulinzi na Usalama wa Mtoto ni Wajibu Wetu Sote.

Upvote
1