Kama kuna neno ambalo leo tunaliogopa kuligusa ni neno "unyonyaji". Kimsingi neno hili lilitokana na dhana ya jinsi kupe anavyoishi kwa kunyonya "host" wake kama ng'ombe, mbwa n.k Kwa maneno mengine mnyonyaji ni mtu ambaye anatumia kila mbinu kujitajirisha kwa kutumia "migongo" ya wengine.
Mwanzoni mwa jamhuri yetu wanyonyaji tuliwaimba na kuweka misemo kama "usiwe mnyonyaji kama kupe" tukiwahimiza watu wafanya kazi au wale kutokana na jasho lao. Tukasema kuwa watu pekee ambao wanastahili kuishi kwa jasho la watu wengine ni watoto, wagonjwa, na wazee ambao wameshachumia juani. Tukawakatalia watu wengine wote ambao wanataka kuishi "kwa njia za mkato".
Hata hivyo baada ya mabadiliko ya kiuchumi yaliyotokea tabaka la wanyonyaji limeanza kujitokeza kwa kiasi kikubwa ambapo kuna watu ambao pasipo kufanya kazi (biashara au kuchakarika kihalali) wanatumia nafasi zao na vyeo vyao kutengeneza fedha ya haraka haraka.
Ni hapo ndipo tumeanza kuona kundi la watu tuwaitao "mafisadi". Wakati neno fisadi linatumika kuelezea kila aina ya uovu katika utumishi wa umma (rushwa, wizi, ubadhirifu, matumizi mabaya ya cheo, ofisi au jina n.k) neno "mnyonyaji" lilikuwa linatumika kuelezea mtu ambaye kimsingi anavuna asichopanda na anameza asichotafuna.
Mnyonyaji ni mtu ambaye hana wasiwasi wa maisha yake kwa sababu ametegesha mirija yake kwenye mabenki, ofisi, n.k ambapo hata akiwa katika ziara ya Rais au akikaa kwenye kiti chake cha ngozi nyeusi mirija hiyo inaendelea kufyonza kama ina kichaa. Mnyonyaji haitaji kufanya kazi yoyote isipokuwa kuweka mrija huo mdomoni na kama mtu anayefyonza ulanzi au mzee aliyekalia kibuyu cha chimpumu au yule anayepulizia mbege basi anajinoma taratibu huku mashavu yake yakitanuka kama chura apigaye mluzi!
Tunachoona sasa hivi ni kuwa wanyonyaji ambao tuliwakatia mirija mwaka 1967 ili angalau na wengine tuweze kunenepa ndio wamerudi kwa ari na nguvu mpya na sasa hivi wananyonya huku wameinua miguu juu kwani wanajua hawanyonyi peke yao. Wakati umefika wa kuchora katuni ya "wanyonyaji mambo leo" ambao wamemzunguka Mtanzania na mirija yao mdomo wakimfyonza kama vile mbu anavyonya damu kama anatumia drill ya kufyonza mafuta!
Wanyonyaji hawa weusi, leo wanasimama wakijua kuwa wanalindwa na hakuna mwenye ujasiri wa kuifyeka mirija yao na kuwakatisha uhondo wao huo. Cha kuudhi ni kuwa sisi Watanzania ndio tumekaa pembeni na kupiga kelele lakini ni kelele za kushangaa siyo kukasirika na kutaka kuikata mirija hiyo. Ndio maana hadi leo hii tunaendelea kuwalipa dowans, Mkapa ameendelea kushika mrija wa Kiwira, na wengine wameshikilia mirija yao huku baadhi yao wakishikilia mirija kwenye kila kidole huku wakicheka cheka na kucheua mafuta yanukayo!
Kinachoendelea si ubepari jinsi unavyoeleweka Magharibi ambapo unajitahidi kuonesha angalau huruma kwa wanyonywaji; wa kwetu ni unyonyaji unaojifanya ni ubepari! Ni nani atakayethubutu kukata mirija hii na kuwakatisha wanyonyaji hawa uhondo wao! Ni nani ambaye yeye mwenyewe si mnyonyaji atakayeona uchungu wa kile kinachoendelea?
Je, mfanyabiashara na mwekezaji anaweza kufanya biashara yake vizuri na akapata faida bila kuwa mnyonyaji wa kutupwa. Je tunaweza kuwaacha watunyonye ilimradi wanatulisha na tunanenepa kidogo kuliko wakitunyonya tukiwa kimbaumbau!? Tufanye nini ili tuwanyang'anye mirija hiyo au tufanye nini ili tuweke machujio kwenye mirija hiyo ili wanapofyonza basi wasivyonze vyote!?
Au tukubali tu kuwa wanyonyaji wana haki ya kutunyonya kwa sababu tumeweka wenyewe migongo yetu wazi ili watunyonye huku tumeipakaa mafuta ili kuitamanisha? Je tuwaache watunyonye kwa sababu wanaweza na jaribio lolote la kutishia kukata mirija hiyo litakutana na upinzani kuwa tunataka kurudia "utaifishaji" na tunataka kutishia wawekezaji?
M'kijiji,
Vitu hivi tusivisahau...
- Kabla ya Azimio la Arusha kulikuwa na baadhi ya watu na tabaka fulani za watu zilizokuwa zimefaidika tokea enzi za ukoloni na kujijengea economic base nzuri ya kujenga utajiri. Utajiri wao uliongezeka kwa kasi na gap kati ya maskini na matajiri ikawa kubwa sana.
- Come 1967, Nyerere and TANU had no option but to Nationalize utajiri huu kuondoa hatari ya tabaka lisilo na mali ambalo lilikuwa majority kulipiga tabaka la matajiri ambalo lilikuwa minority. Though Azimio lile liliumiza matajiri but in another way liliwaokoa na kilichokuwa kinakuja mbele.
- 1977 Sokoine akachukua uPM. Operation ya Azimio la Arusha iliingiliwa na vita. Vita viliathiri uchumi na ile system iliyokuwa imeanza kujengeka ikabomoka. Likazuka tena tabaka la WABADHIRIFU wakishirikiana na WAHUJUMU wa uchumi. Sokoine akaanza kamata kamata tena na kutaifisha mali zao. Haikusaidia tukazidi kudidimia na hayo mashirika, WABADHIRIFU wakawa wengi.
- 1984 Sokoine akafariki. Nyerere akatambua wazi kwamba hana kingine cha kutaifisha na mpira ulikuwa kwake, amlaumu nani? Cha kufanya...akaamua amwage manyanga 1985.
- Mwinyi alichofanya na kuachia tena watu wajenge vitakavyokuja kutaifishwa baadaye? Au aliamini tuko level moja na tunaweza wote compete sawa? Pamoja na kuonekana kuwa mzee wa ruksa. Mabadiliko mengi yalifanyika enzi zake.
- Mkapa alikamata kijiti wakati watu waliheshimu biashara kuliko kufanya kazi serikalini. Mkapa akajenga tena lile tabaka la civil servants ambao hutumia ofisi zao kama biashara zao. Hawa ndio waliokufuru katika kujilimbikizia mali.
Hawa ni wanyonyaji kwani:-
(1) RADAR - Wametubebesha mzigo mkubwa katika bei kuliko ilivyokuwa.
(2) IPTL - Wametubebesha mzigo mkubwa katika bei ya umeme.
(3) EPA - Tumeamini deni letu la nje limepungua kumbe hela wamechukua wao.
(4) TANGOLD/MEREMETA - Kiini macho cha kuchukua hela zaidi.
(5) Import Support - Wamegawana wao na kutengeneza makampuni yao.
The list goes on...
Sasa swali? Tutaifishe kila kitu tena? Au tutumie selective Nationalization?
NB: Usisahau na Ukabaila ;-)