Unyonyaji wa Bodi ya Mikopo (Higher Education Student's Loan Board)

Sifahamu sana kuhusu HESLB lakini kwa hali ya kawaida kama mkataba(makubaliano) yalionesha mengine na badae yakaja kubadilika si huwa kuna haki ya kukataa kulipa?

Ikitokea deni halijalipwa kabisa ni hatua gani inafanyika kwa aliyekataa kulipa?
Anakamatwa mdhamini wake ambaye utakuta ni mzazi wa huyo anayedaiwa. Mzazi sasa ni mstaafu na anatakiwa aitoe hiyo pesa kupitia "tundu" (sorry to say so) lolote kile hadi pesa hiyo ipatikane.
 
Anakamatwa mdhamini wake ambaye utakuta ni mzazi wa huyo anayedaiwa. Mzazi sasa ni mstaafu na anatakiwa aitoe hiyo pesa kupitia "tundu" (sorry to say so) lolote kile hadi pesa hiyo ipatikane.

Ooh,okay
 
Dawa ya deni kulipa! Maliza mkopo na wadogo zako wasome!
 
Mkuu, ni kweli unachosema hii taasisi haiko fair hata kidogo, kwani lengo lake ilikuwa ni kuwasiaidia maskini ambao uwezo wa kulipa hiyo pesa wakati wa kusoma hawana,sasa unajiuliza mtu huyu maskini amemaliza shule hajapata anaanzaje kulipishwa penalty wakati hata kazi hajapata?

Hata taasisi za fedha zinakopesha na kudai interest lakin huwa haziweki penalty sasa unajiuliza taasisi hii ambayo lengo lake ni kusaidia maskini inachaji interest+ penalty kiukweli kuna mambo yanayofanyika nchi hii Mungu ndo anajua ila hapa watu wanaumia sana na kwa anaehisi kuwa anaweza kudai haki mahakamani kwa utaratibu huu wa .... ni gharama kuliko haki yenyewe.
 
The shilling today is worth the shilling tomorrow!
 
Jamani mimi sijui itakuwa imefika shingapi mana tangu 2013 nimemaliza chuo nimesugua kitaa hadi 2016 ndio nikapata kikazi kakupata ugali sasa sijui deni langu litakuwa kiasi gani
Hapo jiandae kisaikolojia, kwanza kuna penalty ya kushiba, ukiongeza VRF na administration charges utaisoma namba nzuri. Wakikunasa wanafyeka 15% ya mshahara wako kila mwezi
 
Hapo jiandae kisaikolojia, kwanza kuna penalty ya kushiba, ukiongeza VRF na administration charges utaisoma namba nzuri. Wakikunasa wanafyeka 15% ya mshahara wako kila mwezi
Duh mkuu sasa inakuwaje inamana nikajisalimishe huko kwao wakati ajira zenyewe zio za kudumu unaweza kuamka asubui kwenda job ukaambiwa kazi hakuna sasa si nitulie zangu tu au unanishaurije mkuu
 
Hapo penalty inakuhusu, kuanzia 2015 ukijumlisha na retention fee ( riba ) ya kila mwaka, kitu ndio kama unavyoona hapo.

Na sasa kuna NIDA Deni halikwepeki labda usifanye kazi sekta rasmi.
Mie nimeamua kupiga mishe zangu tu. Kama zikiendelea kukaa poa, hakika sitalipa kabisa. Labda wanifuate nyumbani.
 
Katika namna yoyote ile, usifagilie maisha ya jeshi hata siku moja. Vyovyote vile itakavyokuwa, ila kazi ya jeshi hapana kwa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…