Naomba kuuliza waungwana....Hivi katika Ndoa...Mke akimnyima mumewe Unyumba kwa "zaidi ya mwaka"...yaani hawajakutana kimwili...(miezi 15 sasa) .. Hiyo ndoa bado ipo kweli...?
Hakuna ugonjwa wala nini...ni Mke amemkasirikia mumewe tu .. na mume wala hajafumaniwa, na wala hajaenda nje kuchakachua...
Naomba usaidizi wa maoni...
Kwa Waislaam hatuna shida sana kwa hili, hii hapa ni swali na jibu linalofanana na lako:
[h=1]Mwanamke Ana Haki Kuomba Talaka Ikiwa Haridhiki Na Mumewe?[/h]
SWALI:
Assalaamu Alaykum. Swali langu ni kwamba mwanamke anaye muomba talaka mumewe kwa sababu haridhiki na mumewe kitandani, je mume huyo ana haki ya kutoa talaka kwa mkewe. Wameishi miaka kumi pamoja na wana watoto wawili bado wadogo chini ya umri wa miaka kumi.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mke kutoridhishwa na mumewe kitandani. Mwanzo kabisa tungependa kukuuliza kuhusu mahusiano yako na mumeo hapo awali baada ya kuoana? Je, alikuwa sawa kitandani? Hili tatizo ilianza lini?
Ikiwa mlipoana mlikuwa sawa na tatizo hilo lilianza karibu basi huenda akaweza kusaidika kwani zipo dawa kwa ugonjwa huo. Huo ni ugonjwa na itabidi kabla ya kuchukua hatua ya kutaka akuache basi zungumza na mumeo kwa njia nzuri kuhusu hilo. Kwa kuzungumza hivyo ndio mnaweza kupata ufumbuzi mzuri kwenu nyote. Wapo madaktari na matabibu ambao wanaweza kuwasaidia katika hilo. Ikiwa atakubali basi itakuwa kheri nasi twawaombea mafanikio mema.
Ikiwa atakataa basi itabidi uende kwa Qaadhi umuelezee kuhusu shida yako hiyo, na lau sehemu hakuna Qaadhi basi utakwenda kwa Shaykh aliyekuoza au Shaykh mwengine muaminifu na muadilifu ili asikilize kesi yenu. Mume kutoweza kumtimizia mkewe starehe ya kitandani ni sababu ya mke kuomba talaka. Mara nyingi mume hatotaka kutoa talaka itabidi wewe kutodhurika ukashtaki kwa Qaadhi ili upate haki yako.
Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Awasuluhishie tatizo lenu hilo na Awapatie tawfiki.
Tunapata kujua kuwa hilo lawezekana kisheria na mke atapaswa amrejeshee mumewe mahari yake, kama tunavyoona katika
kile kisa cha mke wa Thaabit bin Qays aliyekwenda kushtaki kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya mumewe, pamoja na kuwa mumewe hakuwa na tatizo la dini wala tabia bali yeye hakumpenda na akawa anakhofia kutotekeleza wajibu wake kama mke. Mtume aliwatenganisha lakini kwa kumtaka mke airejeshe bustani/shamba aliyokuwa amepewa na mumewe kama ni mahari. Hadiyth hiyo ipo katika Swahiyh Al-Bukhaariy.
Na Allaah Anajua zaidi
Source:
Mwanamke Ana Haki Kuomba Talaka Ikiwa Haridhiki Na Mumewe? | Alhidaaya.com