Unywaji chai kwa wingi ni hatari kwa afya?

Unywaji chai kwa wingi ni hatari kwa afya?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Nice_Cup_of_Tea.jpg

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 47 kutoka jimbo la Michigan nchini Marekani amepata ugonjwa adimu sana
(rare disease) wa mifupa baada ya kunywa chai iliyotengenezwa kwa aina mia moja ya majani ya chai kwa wingi (lita 3 kwa siku) kwa miaka 17 mfululizo, watafiti kutoka Marekani wamesema.

Mwanamake huyo alikwenda hospitali kuonana na Daktari baada ya kuwa na maumivu makali kwenye kiuno,mikono,miguu na kiuno kwa miaka mitano.

Baada ya kufanyiwa kipimo cha
X-ray iligundulika mama huyo ana ugonjwa huo adimu ambao huonyesha dalili za kuongezeka kwa uzito wa mifupa ya uti wa mgongo(dense spinal vertebrae) pamoja na kushikana(calcifications of ligaments) kwa viunganishi vya mifupa ya kwenye mikono’’ alisema mmoja wa watafiti Dr. Sudhaker D. Rao, Daktari bingwa wa magonjwa vichocheo vya mwili

na virutubisho vya mifupa na vya mwili
(Endocrinologist and bone and mineral metabolism physician) katika hospitali ya Henry Ford Hospital,Marekani.

Dr. Rao alihisi mama huyo ana ugonjwa wa mifupa unaojulikana kama skeletal fluorosis unaosababishwa kwa kutumia kwa wingi madini aina ya fluoride
(Fluoride hupatikana kwenye maji au chai)

Kiwango cha madini ya fluoride katika damu ya mama huyo kilikuwa juu mara nne zaidi ya kiwango kinachohitajika kwenye mwili wa mwanadamu.

Ugonjwa wa skeletal fluorosis huonekana sana kwenye maeneo ambayo kiasili yana madini ya fluoride kwa wingi kama baadhi ya maeneo nchini India na China
(katika nchi nyingi kiwango kidogo cha fluoride huweka kwenye maji, dawa za meno kama kinga dhidhi ya ugonjwa wa meno unaojulikana kama cavities)

‘’Mgonjwa alipewa rufaa ya kuja kuniona kwa sababu madaktari walie muona mwanzo walidhani ana saratani ya mifupa, lakini baada ya mimi kuona
X-ray za mgonjwa,mara moja nilitambua kuwa ni ugonjwa wa skeletal fluorosis kutokana na kuwahi kuona wagonjwa wa aina hiyo nilipokuwa kwetu nchini India’’alisema Dr. Rao

‘’Kwa kawaida mwili huchukua kiwango cha madini ya fluoride kinachohitajika tu na kiwango chochote cha ziada hutolewa kupitia kwenye figo.Iwapo mtu atakunywa fluoride nyingi kama mgonjwa huyu alivofanya kutokana na tabia yake ya kunywa chai kwa wingi,basi baada ya muda mrefu madini haya ya fluoride hujikusanya kwa pamoja na kujipandikiza kwenye mifupa’’ aliendelea kusema Dr. Rao.

Dr. Rao alisema huko nyuma waliwahi kupata wagonjwa wengine wachache wa skeletal fluorosis ambao walikuwa wakinywa lita 3.7 za chai kwa siku na baada ya kuwaambia wagonjwa hao waache kunywa chai, dalili za ugonjwa huo zilianza kupungua na wagonjwa kupata nafuu kubwa.

Mkusanyiko wa madini ya fluoride kwenye mifupa hupotea baada ya muda mrefu ikiwa mgonjwa ataacha kunywa chai kwani mifupa ina kawaida ya kujirekebisha (bone repair) yenyewe baada ya muda.

Utafiti huu unapatikana katika jarida la New England Journal of Medicine liliochapwa tarehe 21 march 2013. Madini ya fluoride hupatikana kwa wingi katika maeneo ya kaskazini mwa Tanzania.chanzo.
Unywaji Chai Kwa Wingi ni Hatari kwa Afya?

Kwa wale wanaopenda kunywa chai basi wajitahidi wasinywe zaidi ya vikombe tano kwa siku.Mimi Mwenyewe ni Teja wa chai lakini chai yangu ninaweka tangawizi kavu na Mbadalasini siwezi kupata hayo maradhi inshallah.
 
MziziMkavu chai ziko za aina nyingi kama green tea, na nyinginezo
tofauti tofauti, naomba unijibu maswali 2
1-Chai gani hapa iliokusudiwa?
2- Wataalam mara nyingi wanasisitiza watu wanywe chai sana kama green
tea n.k kuwa zina faida nyingi, sasa mbona hii makala yaako inapingana??
Thanx in advance
 
MziziMkavu chai ziko za aina nyingi kama green tea, na nyinginezo
tofauti tofauti, naomba unijibu maswali 2
1-Chai gani hapa iliokusudiwa?
2- Wataalam mara nyingi wanasisitiza watu wanywe chai kama green
tea n.k kuwa zina faida nyingi, sasa mbona hii makala yako inapingana??
Thanx in advance
Mkuu Boflo chai iliyokusudiwa hapa ni chai ya Rangi inayonywea kwa wingi wa watu kila siku wengine hawajuwi kuwa kuna chai ya Green Tea Mkuu Boflo Hii hapa chini

Chai+Babooneh_TS.jpg
 
Mie teja mkubwa wa chai hapa nishagonga kikombe kimoja! ila huwa sinywi zaid ya viwili kwa siku!
 
MziziMkavu swali langu la 3 kwa nn Turkey wamepiga
marufuku kamari(casino) za aina yote wakati sio nchi ya Kiisalam?
 
Mie teja mkubwa wa chai hapa nishagonga kikombe kimoja! ila huwa sinywi zaid ya viwili kwa siku!
Mkuu Chimunguru mimi leo ninakupa faida ya chai nunuwa chai boksi moja kisha nunuwa tangawizi kavu ya unga gramu 25 nunuwa Mbadalasini ya unga gramu 25 changanya kwenye hayo majani yako ya chai pika uwe unakunywa kila siku itakuwa inakusaidia sana matatizo ya nguvu za kiume haya tena usimwambie mtu fanya hivyo kisha utakuja kunipa feedback kama shemeji hakutoka mbio kitandani kwa nguvu za kiume zinavyozidi kwako kazi kwako mkuu.
 
Last edited by a moderator:
MziziMkavu swali langu la 3 kwa nn Turkey wamepiga
marufuku kamari za aina yote wakati sio nchi ya Kiisalam?
Mkuu Boflo Turkey ni nchi ya kiislam lakini haifuati sheria za Kiislam

karibu asilimia 99% ya Waturuki wote ni Waislam na ukumbuke Turkey ilikuwa inatawaliwa na utwala wa ki Sultan utawala wa Ottoman

Empire kwa muda wa miaka 700 na huo utawala ulikuwa chini ya sheria za dini ya kiislam sasa utaniambia kuwa Turkey sio nchi ya Kiislam? Waswahili wanasema

Mtoto wa Nyoka ni nyoka tu Mtoto wa nyoka hawezi kuwa ni Paka. soma hapa huo utawala wa Ottoman Empire bonyeza hapa https://en.wikipedia.org/wiki/Ottoman_Empire
 
Mkuu Chimunguru mimi leo ninakupa faida ya chai nunuwa chai boksi moja kisha nunuwa tangawizi kavu ya unga gramu 25 nunuwa Mbadalasini ya unga gramu 25 changanya kwenye hayo majani yako ya chai pika uwe unakunywa kila siku itakuwa inakusaidia sana matatizo ya nguvu za kiume haya tena usimwambie mtu fanya hivyo kisha utakuja kunipa feedback kama shemeji hakutoka mbio kitandani kwa nguvu za kiume zinavyozidi kwako kazi kwako mkuu.

Mkuu Thanks alot, tangawizi natumia sana ila mdalasini sijawahi tumia, ngoja leo nitafute ni mix km ulivyoelekeza halafu nikamkimbize mtoto wa kichaga hahahahahah
 
Mkuu Thanks alot, tangawizi natumia sana ila mdalasini sijawahi tumia, ngoja leo nitafute ni mix km ulivyoelekeza halafu nikamkimbize mtoto wa kichaga hahahahahah
Mkuu Chimunguru Ikiwa hujamuowa usije ukamtia tu mimba mtoto wa kichaga shauri yako dawa kiboko hiyo mmi huku shemeji yako ninamuendesha mchakamchaka ananiuliza kulikoni mume wangu unatumia Viagra ninacheka tu nina ongeza na asali kijiko kimoja kabla ya mechi kuanza wee kasheshe kweli shemeji yako anaomba Half time uwanjani.
 
Last edited by a moderator:
MziziMkavu swali langu la 3 kwa nn Turkey wamepiga
marufuku kamari(casino)
za aina yote wakati sio nchi ya Kiisalam?

Turkey imekuwa nchi ya "born again"/ imeokoka,ulokole ndio sababu wamepiga marufuku kamari. Niliuliza swali kama lako kwa mturuki mmoja na alinipa maelezo hayo..sijui alitania au ndio ukweli. Alisema, Jehova(mungu wao) amekataza kamari.
 
Mkuu Chimunguru Ikiwa hujamuowa usije ukamtia tu mimba mtoto wa kichaga shauri yako dawa kiboko hiyo mmi huku shemeji yako ninamuendesha mchakamchaka ananiuliza kulikoni mume wangu unatumia Viagra ninacheka tu nina ongeza na asali kijiko kimoja kabla ya mechi kuanza wee kasheshe kweli shemeji yako anaomba Half time uwanjani.

HAHAHA huyo ni wife halali kabsaaa so ataona mchezo unakuwa wa kasi ya ajabu
 
Turkey imekuwa nchi ya "born again"/ imeokoka,ulokole ndio sababu wamepiga marufuku kamari. Niliuliza swali kama lako kwa mturuki mmoja na alinipa maelezo hayo..sijui alitania au ndio ukweli. Alisema, Jehova(mungu wao) amekataza kamari.
Mkuu Nonda Serikali ya U-Turuki haifuati sheria za Kiislam ila wananchi ndio wenye kuifuata shria ya dini ya Kiislam cheza na mturuki lakini usicheze na dini ya kiislam iliyopo nmchini Uturuki Ukitaka kufa au kuuliwa na mturuki basi tukana dini ya Kiislam anaweza kukuchinja naserikali ikamuweka ndani kwamuda tu huyo aliyekuuwa wewe kwa kuitukana dini ya Kiislam Mtukane M-turuki lakini usitukane dini yake atakumaliza wakati wowote ule Mkuu. Waturuki wanafuata aya hii ndani ya Kuraan 5.Surat Al-Maida AYA YA 90

(90. Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa. [SUP]90)
[/SUP]

Imebakia Ulevi (Pombe) kupiga Marufuku na hii haitochukuwa muda mrefu kuanzia hivi sasa utasikia pia hakuna ruhusa ya kulewa au mambo ya Pombe au viwanda vya Pombe vitafungwa muda sio mrefu kuanzia hivi sasa.
 
...Imebakia Ulevi (Pombe) kupiga Marufuku na hii haitochukuwa muda mrefu kuanzia hivi sasa utasikia pia hakuna ruhusa ya kulewa au mambo ya Pombe au viwanda vya Pombe vitafungwa muda sio mrefu kuanzia hivi sasa.

MziziMkavu

Hao waturuki ndio watakuwa na maisha? Ndio kuishi vipi huko?

Wamepiga marufuku Kamari(bahati nasibu), Watapiga marufuku ulevi(maji ya uzima)....
Kitimoto(holy flesh) vipi watatuachia? Au hata hii ndafu wataipiga marufuku?
 
Mkuu Chimunguru mimi leo ninakupa faida ya chai nunuwa chai boksi moja kisha nunuwa tangawizi kavu ya unga gramu 25 nunuwa Mbadalasini ya unga gramu 25 changanya kwenye hayo majani yako ya chai pika uwe unakunywa kila siku itakuwa inakusaidia sana matatizo ya nguvu za kiume haya tena usimwambie mtu fanya hivyo kisha utakuja kunipa feedback kama shemeji hakutoka mbio kitandani kwa nguvu za kiume zinavyozidi kwako kazi kwako mkuu.

MziziMkavu

Na mwanamke/ mke akitumia hii kitu uliyoshauri hapa "kuongeza nguvu" je itakuwaje?

Bwana/ dume linaweza kukimbia mechi pia au kuomba half time?

Maelezo yako huenda yakamfanya Chimurungu afungie mbali/ afiche huo mzigo ili shemegi asijeakautumia na kuleta balaa wakati wa mechi.
 
MziziMkavu

Hao waturuki ndio watakuwa na maisha? Ndio kuishi vipi huko?

Wamepiga marufuku Kamari(bahati nasibu), Watapiga marufuku ulevi(maji ya uzima)....
Kitimoto(holy flesh) vipi watatuachia? Au hata hii ndafu wataipiga marufuku?
Mkuu Nonda Hata kwenye Biblia Takatifu

Kwenye Agano la kale Pombe,Kitomoto,Kamari, Ushoga,Usagaji, Ubasha Vimekatazwa vilivyokatazwa kwenye Quraan na ndio hivyo

hivyo vilivyokatazwa kwenye Biblia kwenye Agano la kale Mungu anatutakia viumbe wake yaliyo mazuri Mungu hatutakii viumbe wake

yaliyokuwa ni mabaya Mkuu. Hata Bwana YESU Kristo alisema hayo kuwa hakuja kuitenguwa Taurati ya Manabii ila amekuja

kuitimiliza. Unajuwa neno Taurati kwa kiswahili ? Taurati kwa kiswahili ni Sharia ya Mungu Amri 10 za Mungu Bwana YESU Kristo hakuja

kuzipinga hata kidogo kazitekeleza hizo amri 10 za Mungu alizopewa Nabii Musa upo pamoja na mimi mkuu Nonda? Kazi kwako kumeza

au kutema Mchanga wa pwani huo mimi Simooooooooooo
 
Kalibu hapa! lakini fumba macho! https://www.jamiiforums.com/jamii-photos/113425-kiti-moto-hiki-ni-balaa.html
 
MziziMkavu kwa nn wa cyprus wanawachukia sana waturuki
wakati waturuki wanadai ni kisiwa chao?
Na kwa nn sasa hv Bongo waturuki wanakuja kwa wingi sana kuekeza na wengine kufanya kazi huku?
 
Last edited by a moderator:
MziziMkavu kwa nn wa cyprus wanawachukia sana waturuki
wakati waturuki wanadai ni kisiwa chao?
Na kwa nn sasa hv Bongo waturuki wanakuja kwa wingi sana kuekeza na wengine kufanya kazi huku?
Mkuu Boflo WAturuki walikichukuwa hicho Kisiwa cha cyprus mwaka 1974 alipokiacha Muingereza hicho kisiwa wenyewe ni WaGiriki alivyoondoka Muingereza kukiacha hicho kisiwa cha (Cyprus) ndipo Serikali ya Uturuki ilipo

peleka Majeshi yake huko Kaskazini ya Cyprus ipo karibu sana na Uturuki, ndipo waturuki wlipokichukuwa hicho kisiwa

cha cyprus kwa upande wa Kaskazini yaani North Cyprus kusini wanacho wenyewe WaGiriki.ndipo walipo peleka

Wananchi wao Wa Kituruki huko North Cyprus mwaka 1974 na ndipo mpaka leo hawataki kukiachia hicho kisiwa cha North

Cyprus angalia Ramani chini hapo. Waturuki kuja hapo Tanzania wanaendeleza Mila na Utamaduni wao wa Kituruki

wanavyotaka wao waonekana ni Taifa kubwa kama Marekani au Urusi kiuchumi na kiutamaduni wanapenda sana

kuonekana Wakubwa kwa kila kitu hiyo ndio sifa yao kubwa wanataka kujaribu kurudisha Utawala wao wa kutawala

Dunia kiakili sio kwa kutumia Mbavu kama navyotumia Taifa la Marekani kuwapiga Mataifa Wanyonge. Waturuki

wanataka waonekane kama walivyokuwa zamani za utawala wa Ottoman Empire hiyo ndio sifa yao kubwa sio mbaya

Waturuki sio wabaya ni watu wazuri wanasaidia sana wau duniani kiuchumi na kielimu ingawa elimu yao ni ndogo

ukifananisha na Elimu ya Amerika au Uingereza au mataifa mengine makubwa duniani hiyo ndio sifa ya Uturuki. Kisiwa hicho cha North Cyprus kina utajiri wa Mafuta ndio maana M-Turuki hataki kukiacha hicho kisiwa cha North Cyprus.

Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini

Kupro ya Kaskazini​

Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini (Kituruki: Kuzey Kıbrıs Türk Cumhuriyeti) ni nchi

isiyotambuliwa na jumuiya ya kimataifa iliyoko sehemu ya kaskazini ya kisiwa cha Kupro. Eneo

lake ni 3,335 km² kuna wakazi laki mbili karibu wote ni Waturuki pamoja na Wagiriki 3,000

waliobaki kwenye rasi ya Rizokarpaso. Mji mkuu ni sehemu ya kituruki ya Nikosia.

Ni eneo lililojitenga na Jamhuri ya Kupro baada ya vita ya 1974. Hadi wakati ule Wakupro

Wagiriki (waliokuwa wengi) na Wakupro Waturuki (waliokuwa takriban robo ya wakazi) waliishi

pamoja pande zote za kisiwa. 1974 maafisa Wagiriki wa jeshi la Kupro walipindua serikali ya

Askofu Makarios
kwa shabaha ya kuunganisha kisiwa naUgiriki. Uturuki uliingia kati ukavamia

kisiwa kwa kusudi ya kukinga wakazi wenyeji Waturuki.

Jeshi la Kituruki lilitwaa theluthi ya kaskazini ya kisiwa. Wakupro Wagiriki 160,000 kutoka kaskazini walikimbia kwenda kusini na Wakupro Waturuki

50,000 kutoka kusini wakakimbia kaskazini.

Hata baada ya mwisho wa uasi na kurudi kwa rais Askofu Makarios jeshi la Uturuki likakataa kundoka tena. 1973 Dola la Kujitawala la Kituruki la

Kupro likatangazwa. 1983 Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini ikatangaza uhuru wake lakini haikutambuliwa na UM wala na nchi yoyote

isipokuwa Uturuki.

Wakupro Waturuki walio wengi wameondoka kisiwani wakihamia Uingereza na nchi nyingine. Idadi kubwa ya watu wenye utamaduni wa Kituruki

kisiwani wamehamia kutoka Uturuki bara baada ya uvamizi wa jeshi la Uturuki. chanzo.
Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini - Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa wale wanaopenda kunywa chai basi wajitahidi wasinywe zaidi ya vikombe tano kwa siku.Mimi Mwenyewe ni Teja wa chai lakini chai yangu ninaweka tangawizi kavu na Mbadalasini siwezi kupata hayo maradhi inshallah.

Duh itabidi na mimi nibadili ingredients aisee...maana hapa saivi ni saa 08:26 lakini tayari nshapiga vikombe vitatu tayari!!! i drink more tea than water i guess!!!

Cc: Paloma, niekee snack...lol!!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom