KWELI Unywaji wa maziwa mabichi husababisha ugonjwa wa Brucellosis

KWELI Unywaji wa maziwa mabichi husababisha ugonjwa wa Brucellosis

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimeona taarifa ikionesha kuwa unywaji wa maziwa mabichi husababisha ugojwa wa brucellosis na mimi kwa upande wangu nimekuwa nikinywa maziwa mabichi kwa muda kidogo japo sijawahi kuona changamoto yoyote.

Screenshot 2024-09-17 120734.png


Jambo hili lina madhara?
 
Tunachokijua
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO) Brucellosis ni ugonjwa wa bacteria unaosababishwa na bakteria jamii ya Brucella unaoathiri wanyama kama vile ng’ombe, nguruwe, mbuzi, kondoo, mbwa n.k. Binadamu hupata ugonjwa huu endapo kutatokea uhusiano wa moja kwa moja na mnyama aliyeathirika na ugonjwa huu aidha kwa kula au kunywa mazao yatokanayo na wanyama hao.

Ugonjwa huu umpatapo binadamu unaweza kuonesha dalili tofautitofauti kama vile kupata homa kali, maumivu ya kichwa, maumivu ya tumbo, joto la mwili kuongezeka maumivu nyuma ya shingo ambapo ni muhimu kuchukua hatua uonapo dalili kama hizi.

Kwa mujibu wa maktaba ya tiba ya taifa ya markani Ugonjwa huu husambaa kwa wanyama kupitia unywaji wa maji au ulaji wa chakula kilichobeba bakteria wa ugonjwa huu, ambao hupatikana zaidi kwenye uchafu utokanao na uzazi kwa wanyama. Shirika la afya ya wanyama (WOAH) duniani linaonesha ni ugonjwa ambao huweza kupelekea kutoka kwa ujauzito kwa wanyama hata kusababisha ugumba kwa wanyama.

Kumekuwepo na machapisho mitandaoni yanayoonesha unywaji wa maziwa mabichi ya ng’ombe husababisha ugonjwa wa Brucelloisis kwa binadamu huku kwa kiwango kikubwa jamii za wafugaji hutumia maziwa yaliyotoka kukamuliwa pasi na kuchemshwa.

Uhalisia wa jambo hili upoje?
JamiiCheck imepitia machapisho mbalimbali kutoka vyanzo vya kuaminika na kubaini kuwa ni kweli utumiaji wa maziwa mabichi kutoka kwa wanyama walioathiriwa au waliobeba bakteria wa ugonjwa wa Brucellosis huweza kusababisha kupatwa na ugonjwa huo kwa binadamu.

Bakteria wanaosababisha ugonjwa huu huingia mwilini mwa binadamu kupitia mdomo, pua, macho au ngozi iliyochubuka na baadae kuingia mwilini na kuathiri ini, moyo, ubongo na mifupa ambapo pia bateria hawa huweza kutoka mtu mmoja na kwenda mtu mwingine kupitia ngono isiyo salama, unyonyeshaji na hata kutoka kwa mama mjamzito kwa mtoto ambaye bado hajazaliwa.

Kituo cha kuzuia na kupambana na magonjwa cha nchini Marekani katika chapisho lake kinaonesha kuwa si unywaji wa maziwa mabichi pekee bali hata ulaji wa nyama mbichi huweza kupelekea kusambaa kwa ugonjwa huu, hivyo inashauriwa kuchemsha maziwa kwa kiwango cha nyuzi joto Centigredi 100 au kupika nyama mpaka iive vizuri ili kuua bacteria waliomo kwenye mazao hayo ya wanyama ambayo hutumiwa kama chakula na binadamu.

Kuna uwezekano mdogo wa Brucellosis kusababisha kifo ambapo kwa mujibu wa Cleverland Clinic ya nchini Marekani katika kesi zote zilizoripotiwa juu ya ugonjwa huu ni asilimia 1% mpaka 2% ya vifo vilivyotokea kutokana na brucellosis.

Inashauriwa kuwaona wataalamu wa afya hasa watu walio hatarini kupata ugonjwa huu hasa ambao shughuli zao zinawahusisha na wanyama kwa ajili ya vipimo na matibabu zaidi hasa uonapo dalili za ugonjwa huu ili kukabiliana na ugonjwa huu kwa binadamu kwani huweza kuathiri ini, moyo, ubongo, mifupa na sehemu zingine za mwili.
Back
Top Bottom