Unywaji wa maziwa uko chini nchini

Unywaji wa maziwa uko chini nchini

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Imeelezwa kuwa unywaji wa maziwa nchini uko chini ya kiwango cha kimataifa, ambapo Mtanzania mmoja anakadiriwa kunywa lita 50 kwa mwaka ikilinganishwa na kiwango cha lita 200 zinazotakiwa kwa mujibu wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 26 kuhusu maadhimisho ya Siku ya Maziwa duniani, Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Anjelina Lutambi, amesema yatafanyika mkoani hapa Septemba 29, 2021 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe.

Soma hapa: Mama anayekamua lita 40 za maziwa yake mwenyewe.

Lutambi amesema kwa kiwango cha unywaji wa maziwa kiko chini hususan katika shule za msingi, ambapo ametoa mfano wa Mkoa wa Kilimanjaro akisema zipo shule 24 zinazotoa maziwa, Mbeya shule nne na Iringa shule mbili, hali aliyosema hairidhishi.

Amesema kwa Tanzani kuna idadi ya shule 210 zenye wanafunzi zaidi 9,000 zenye utaratibu wa kunywa maziwa hivyo kupitia maadhimisho hayo serikali itahamasisha jamii unywaji wa maziwa.

Soma hapa:Maziwa ya nyuki tiba ya magonjwa ya binadamu

Mfanyabishara wa Maziwa, Tausi Azory amesema kuwa licha ya Serikali kuhamasisha unywaji wa maziwa bado soko la maziwa ni dogo jambo linalochangia bei zake kuporomoka kila kukicha.

Naye Janeth Samson amesema kuwa uwekwe utaratibu wa utoaji elimu kuanzia katika ngazi za familia kuhamasisha unywaji wa maziwa katka ngazi za kata na vijiji.

MWANANCHI
 
Kama mlo mmoja kwa siku Ni matatizo hayo maziwa si ndo itakuwa muhali.

Fikiria Lita ya maziwabtsh 2,000/= halafu kutwa nzima Mtu kapata Tsh 1500/= kitakachofiata Happ Ni kununua ugali wa buku na Maharage ya jero wanagombania na watoto siku inakua imekwisha hiyoooo
 
Maziwa ya ngo'mbe tu au ni pamoja na maziwa ya wanyama wengine? Kuna sehemu wanakunywa maziwa ya mbuzi wa kienyeji ambapo kwingine mbuzi hao hawakamuliwi na ni kituko kunywa maziwa ya mbuzi
 
Maziwa ni chakula cha wanyama wachanga kwa ajili ya kukuza mifupa na viungo vingine HARAKA, ndani ya maziwa kuna cassein ambayo mnyama mchanga ndiye mwenye enzyme ya kuimeng'enya na akishakua hiyo enzyme inatoweka na hivyo cassein haiwezi kusagwa tena mwilini... Ina madhara ndiyo(google)

Ni binadamu peke yake ambaye "ananyonya" hadi uzeeni ...ndama akikua ukimpa maziwa anatema maana anajua mwili wake hauitaji tena maziwa.

Eti tunakunywa maziwa kupata protini na madini...viumbe wengine kama nyani, tembo, nk huwa wanapata wapi virutubisho maana wao huacha kunyonya mapema tofauti na sisi!

Watumiaji wakubwa wa madawa kama antibiotic, nk ni ng'ombe wa maziwa na hayo mabaki ya dawa yanaishia kwenye matumbo yetu!

Nyuma ya uhamasishaji wa watu "kunyonya" hadi uzeeni kuna makampuni makubwa ya biashara...hawa wanachotaka ni pesa na sio afya zenu ..
PENDA MAZINGIRA ACHA KUNYWA MAZIWA!
 
Sio kweli, kuna wengine hadi mwaka unaisha hajanywa hata nusu lita,
Labda museme kwa wastani,
Ambayo si takwimu sahihi kiuhalisia
 
hizo lita 50 wana uhakika na mimi hua zinanifikia kweli ?
 
Maziwa ni chakula cha wanyama wachanga kwa ajili ya kukuza mifupa na viungo vingine HARAKA, ndani ya maziwa kuna cassein ambayo mnyama mchanga ndiye mwenye enzyme ya kuimeng'enya na akishakua hiyo enzyme inatoweka na hivyo cassein haiwezi kusagwa tena mwilini... Ina madhara ndiyo(google)

Ni binadamu peke yake ambaye "ananyonya" hadi uzeeni ...ndama akikua ukimpa maziwa anatema maana anajua mwili wake hauitaji tena maziwa.

Eti tunakunywa maziwa kupata protini na madini...viumbe wengine kama nyani, tembo, nk huwa wanapata wapi virutubisho maana wao huacha kunyonya mapema tofauti na sisi!

Watumiaji wakubwa wa madawa kama antibiotic, nk ni ng'ombe wa maziwa na hayo mabaki ya dawa yanaishia kwenye matumbo yetu!

Nyuma ya uhamasishaji wa watu "kunyonya" hadi uzeeni kuna makampuni makubwa ya biashara...hawa wanachotaka ni pesa na sio afya zenu ..
PENDA MAZINGIRA ACHA KUNYWA MAZIWA!
Umeongelea maziwa fresh hapo ni sawa ila ukikuwa maziwa ya mgando kwa mtu mzima ni sawa, jibini na cream pia.
 
Zamani nilikuwa nakunywa maziwa lakini siku hizi siyanywi baada ya kugundua yanachanganywa na unga wa ngano yaonekane mazito. Maziwa haya ukiyachemsha asubuhi mpaka jioni rangi yake inakuwa kama chai ya maziwa.
 
Back
Top Bottom