unywaji wa pombe

steveachi

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2011
Posts
10,643
Reaction score
12,247
baada ya masaa mangapi tokea kumaliza dozi ya UTI unaruhusiwa kunywa pombe.
Nakala: MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
........Duuu!
yaani UTI ilikufanya ukumbuke "ulabu" uliuisi sana..... lakini kama
ukiisusa kabisa itakuwa vema zaidi .....

Yaani we acha tu kaka,hapa nilipo nina mchupa wangu mkubwa wa maji ya kilimanjaro,najaribu kuufuata ushauri wa MziziMkavu kwani hyu jamaa namtrust mno
 
Last edited by a moderator:
MziziMkavu;

Nilitegeme majibu majibu mazuri kama haya tokea kwako baada ya kuona thread hii!

Upo Kamanda wangu? Mi mzima wa afya njema!

Mbona kanijibu Mkuu,ona posti yake ya kwanza kabisa,na kwa kuona umuhm wake ktk fani hyo nikammensheni kabisa ili anione,na namshukuru allah nimefanikiwa kujibiwa nae,vp kuna la zaidi mkuu wng?
 
Last edited by a moderator:
Mbona kanijibu Mkuu,ona posti yake ya kwanza kabisa,na kwa kuona umuhm wake ktk fani hyo nikammensheni kabisa ili anione,na namshukuru allah nimefanikiwa kujibiwa nae,vp kuna la zaidi mkuu wng?
Mkuu.@steveachi Uwe unapunguza kunywa na hata siku za mbele ikiwezekana uache kabisa kunywa Pombe sio nzuri kiafya haswa wewe ukizingatia umeumwa ugonjwa UTI huo ndio ushauri wangu punguza kunywa pombe au acha kabisa ikiwezekana.
 
Mkuu.@steveachi
Uwe unapunguza kunywa na hata siku za mbele ikiwezekana uache kabisa
kunywa Pombe sio nzuri kiafya haswa wewe ukizingatia umeumwa ugonjwa UTI
huo ndio ushauri wangu punguza kunywa pombe au acha kabisa
ikiwezekana.

Poa mkuu,ila mi sio mnywaji sana kivile,kwa wk naweza nikanywa mara 1 au 2 tena tubia tuchache tu,mkuu hvyo uwezekano wa kuacha upo,sijawa addicted saana,kuna uhusiano gani kati ya pombe na UTI??
 
Poa mkuu,ila mi sio mnywaji sana kivile,kwa wk naweza nikanywa mara 1 au 2 tena tubia tuchache tu,mkuu hvyo uwezekano wa kuacha upo,sijawa addicted saana,kuna uhusiano gani kati ya pombe na UTI??
Hakuna Uhusiano kati ya UTI na Unywaji Pombe.


Sababu za UTI

UTI yaweza kusababishwa na vijidudu vya namna nyingi. Mathalani ni vimelea
(bakteria) japo pia na jamii nyingine ya vijidudu vinaweza kusababisha UTI. Bakteria aina ya Escherichia coli kwa kiasi kikubwa ndio inayosababisha UTI japo pia bakteria


wengine wapo. Vijidudu hivi vyaweza kuingia katika njia ya mkojo kutokea nje ya mwili au hata kwa kupitia damu ya mhusika.


Kwa wanawake, fangasi katika sehemu za siri imekuwa ni tatizo kubwa sana. Uwepo wa fangasi hasa kwenye uke na maeneo jirani pia huweka mazingira ya mvuto kwa bakteria kuvamia maeneo hayo na kuleta maradhi, hasa UTI.


Kwa wanaume mara nyingi kutokana na maumbile yao na mfumo mzima wa mkojo na viungo vyake, huwa siyo waathirika wakubwa wa UTI.

Vihatarishi

Sababu hatarishi (risk factors) za UTI zipo nyingi, kulingana na umri, jinsia na mazingira ya mhusika. Mfano sababu hatarishi za
mtoto mchanga kupata UTI si sawa na mtu mzima jinsia ya kike. Maumbile na mfumo wa kibiologia ya mwanamke humweka

katika nafasi hatarishi zaidi ya kupata UTI. Vile vile ngono, tena ya mara kwa mara ni moja ya sababu zinazoweza kuchangia mtu kupata UTI.


Kwa kupitia ngono, bakteria waliopo katika sehemu za siri za mhusika vinaweza kupata nafasi ya kupenya na kuingia katika mfumo wa njia ya mkojo kwa urahisi zaidi.


Sababu nyingine ni upungufu wa kinga mwilini kwa sababu yeyote, ikiwamo ujauzito kwa wanawake n
a ugonjwa wa kisukari
(diabetes). Lakini pia, sababu nyingine kadha wa kadha zinazosababisha upungufu wa kinga mwilini.@steveachi

 
Athari za muda mrefu za pombe


Athari za muda mrefu za pombe hutapakaa baina ya uwezekano wa faida za kiafya kwa watumiaji wa viwango vya chini vya pombe hadi madhara makubwa katika hali ya matumizi mabaya ya pombe kwa muda mrefu. Viwango

vya juu vya matumizi ya pombe huhusiana na ongezeko la hatari ya kuendeleza ulevi, ugonjwa wa moyo,

kutofyonza vyakula, ugonjwa sugu wa kongosho , ugonjwa wa ini kutokana na pombe, na
kansa. Uharibifu kwa mfumo mkuu wa neva na mfumo wa neva za pembeni unaweza kusababishwa matumizi kila mara ya pombe.

Matumizi ya pombe kupita kiasi kwa muda mrefu yanaweza kuharibu takribani kila kiungo na mfumo katika mwili.Ubongo unaokua wa kijana aliyebaleghe huwa hasa katika hatari kubwa ya kudhurika na sumu ya pombe.


Kihistoria, madaktari wametetea pombe kwa faida zake za kiafya na hivi karibuni kwa ajili ya uwezo wake wa kulinda watumiaji dhidi ya ugonjwa wa moyo. Kuna ushahidi wa faida kwa mishipa ya moyo inayotokana na

kutumia kinywaji 1- 2 kwa siku, hata hivyo, faida za kiafya kutokana na unywaji pombe kwa wastani ni swala lenye utata. Shauku zimetolewa kuwa sawa na ilivyo katika sekta ya dawa, wadau wa sekta ya pombe

piawamehusika katika kutilia chumvi faida za kiafya za pombe. Pombe inapaswa kuonekana kama dawa ya burudani yenye uwezo mkubwa wa kusababisha athari mbaya kwa afya na hipependekezwi kwa-ulinzi wa moyo badala ya mbinu nyinginezo za salama na zilizothibitika za jadi kama vile lishe bora mazoezi na tiba za dawa.


Baadhi ya wataalamu wanadai kuwa faida za matumizi ya pombe ya wastani zinaweza kupitwa na ongezeko la hatari ikiwa ni pamoja na majeraha, vurugu, uharibifu wa mimba, aina fulani za saratani, ugonjwa wa kongosho

na presha. Kwa vile faida bainifu za kiafya za matumizi ya pombe ya wastani ni ndogo kwa watu walio katika hatari ndogo ya kupata maradhi ya
moyo, wataalamu wengine wanatahadharisha itumike kwatahadhari kwa

sababu ya uwezekano kwamba kupendekeza matumizi wastani ya pombe kunaweza kusababisha ongezeko la hatari ya matumizi mabaya ya pombe, hasa miongoni mwa vijana.
Manufaa haya ya matumizi wastani ya pombe yanapitwa na hatari za matumizi ya pombe wastani
 
Mkuu MziziMkavu, thanks very much for taking your time to advise me, be blessed,nitajitahidi kufuata ushauri wako,ngoja nikajivinjari na lile movie lako la 'mama yangu adui wangu',manake sijalipitia kama wiki mbili hv,nahisi nitakuwa nyuma sana.
 
Last edited by a moderator:
Ulikua na UTI?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…