Uchaguzi 2020 Uoga ni adui kama ilivyo ujinga, umasikini na maradhi. Tuendelee kuupiga vita

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2017
Posts
7,101
Reaction score
18,051
WanaJF,

Nimewaza sana kuhusu hili. Uoga ni kitu kibaya sana. Uoga unawafanya watu wawe wanyonge na kunyong'onyea. Lakini pia waweza kupigwa vita na kuondoka. Kabla Lissu hajarudi, watu walikuwa wanasisimkwa mwili kufikiria tu kuwa atarudi tena Tanzania. Haya Lissu akarudi. Kabla ya kuteuliwa, akaanza mashambulizi - akawa anayapeleka palepale kwenye kitovu ambako watu hawapendi kuongelea hata wawapo wenyewe chumbani. Vyombo vya habari vikawa havitaki kabisa kuongelea habari za Lissu. Vyombo vikaunga juhudi za Rais na chama chake.

Lissu akandelea na uzi ule ule. Baada ya mwezi wa kazi ya Lissu, watu wamegundua kuwa yule self-proclaimed malaika na mungu-mtu kumbe naye ni binadamu anayekula, kunywa na kwenda toilet kama wengine. Sasa hivi naona vyombo vya habari vilevile vya mwezi mmoja uliopita, vinamzungumzia Lissu kama kawaida. Tena vinaweka kwenye taarifa zao hata kauli za kushambulia CCM na mgombea wake! Katika mwezi mmoja, watu wameondoa uoga. Uoga umeondoka ghafla! Watu wanamzomea hata yule aliyejitangaza kuwa ni malaika! Nani alitegemea haya katika Tanzania hii? Hata Membe alikuwa hana ujasiri wa kutaja chama cha kijani na mgombea wake. Akawa anamwita, "bwana yule"!

Tarehe 28 Oktoba 2020, shime Watanzania wenye miaka 18 na kuendelea, tuliojiandikisha kupiga kura, tujitokeze kwa wingi wetu tumpigia kura Lissu. Mfumo kandamizi utoke. Tupate uhuru, haki, amani na maendeleo kwa pamoja. Maendeleo yanaweza patikana bila watu kufungwa jela kwa ghiriba ama kupigwa risasi.

Lissu oyeeeeeeeeee! Yule aliyetaka kukuua anaona kama anapambana na mzimu wako vile. Sidhani kama atapata ujasiri wa kutaja jina lako kwenye majukwaa. Mwenezi wake pia anakuita eti "mgombea wa chama cha Mbowe" ili tu aepuke kukujata jina!

Pia tukumbuke kulinda kura zetu.
 
HOFU inaondoka kwa kasi miongongoni mwa wananchi. Katika miaka mitano ya GIZA, iliishaanza kuwa kama uhaini vile kuonekana una mtazamo tofauti na wa JIWE.

Malaika JIWE alikuwa hana anachokosea. Kila kitu hata akinywa maji anashangiliwa. Watu wazima kabisa, wasomi wananyamazia na wengine kusifu ukandamizaji na uvunjaji wa katiba.

Sasa BASI
 
Lissu ni mtu jasiri wa hali ya Juu tangu mdogo amekuwa akihoji mambo mbali mbali bila hofu wala Woga wowote.

Hata alipokuwa JESHI JKT Hali yake ya kuhoji bila woga wala hofu iliwahi kupelekea baadhi ya Maofisa wa jeshi kuhisi Lissu ni Afisa wa Usalama wa Taifa.

NI YEYE
 
Asante sana kwa kuweka wazi ukweli. Ni kweli kabisa Lissu ameondoa woga kwa watanzania na amewafumbua macho watanzania sana! Bila Shaka ccm wenyewe wanashukuru manake walikuwa kama punda tu.

Back
Top Bottom