Uoga wa kufiwa na CCM na Muungano

Uoga wa kufiwa na CCM na Muungano

Kishimbe wa Kishimbe

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2013
Posts
5,566
Reaction score
5,477
Miongoni mwa mambo ambayo yametugharimu sana Watanzania ni hofu kuu ya watawala wetu wa vipindi mbalimbali kuogopa au kuona haya kufiwa na CCM na muungano wa bara na visiwani!

Watu wamepatwa na majanga luluki, hasa huko visiwani, kila chama pinzani kinapoelekea kushinda uchaguzi kwa asilimia kubwa kwa hofu tu kuwa hicho chama kingine kikishika hatamu, japo visiwani tu, basi muungano 'wagendaa'!

Mzee Mkapa, katika kitabu chake, mpaka aliwaomba radhi watanzania kwa aliyoyatenda Visiwani kutokana na kuulinda huo muungano na kuogopa kufiwa na CCM na hayupo peke yake!

NI LINI VIONGOZI WETU, TANZANIA, WATAKOMAA NA KUMUDU KUIKABILI HOFU HII NA KUTUACHA WABONGO TUJIAMULIE HATMA YETU NZURI KWA RIDHAA? HII ITAWAWEKA WAO HURU PIA!
 
Mkiachwa wabongo peke yenu kuna kipi kipya mtafaidika nacho ambacho mnakikosa katika huu muungano

Tuanzie hapa kwanza expert wangu
 
Mkiachwa wabongo peke yenu kuna kipi kipya mtafaidika nacho ambacho mnakikosa katika huu muungano

Tuanzie hapa kwanza expert wangu
Wazanzibar wanatunyonya . Sasa hivi mapato yanayokusanywa Tanganyika mengi yanaenda kuwafaidisha wazanzibar. Hapa either tutengeneze serikali tatu au serikali moja zanzibar isiwe na rais anayejitegemea.
 
Kuna nuru mbele

Mwenyekiti mpya CHADEMA baada ya kutangazwa ametuma ujumbe mzito. Ametumia neno Tanganyika.

Alikuwa anatangaza mkutano wa Baraza Kuu la leo saa tisa, akasema tunaenda kumchagua Party Sectretary na manaibu wake wa Zanzibar na Tanganyika!

Siku yaja tutapindua mi blunder na mi mess up ya mifumo Nyerere.

Miongoni mwa mambo ambayo yametugharimu sana Watanzania ni hofu kuu ya watawala wetu wa vipindi mbalimbali kuogopa au kuona haya kufiwa na CCM na muungano wa bara na visiwani!

Watu wamepatwa na majanga luluki, hasa huko visiwani, kila chama pinzani kinapoelekea kushinda uchaguzi kwa asilimia kubwa kwa hofu tu kuwa hicho chama kingine kikishika hatamu, japo visiwani tu, basi muungano 'wagendaa'!

Mzee Mkapa, katika kitabu chake, mpaka aliwaomba radhi watanzania kwa aliyoyatenda Visiwani kutokana na kuulinda huo muungano na kuogopa kufiwa na CCM na hayupo peke yake!

NI LINI VIONGOZI WETU, TANZANIA, WATAKOMAA NA KUMUDU KUIKABILI HOFU HII NA KUTUACHA WABONGO TUJIAMULIE HATMA YETU NZURI KWA RIDHAA?
Hayo mambo mawili hayana faida hasa upande wa Tanganyika, na CCM ikifa leo ni kheri kwa Watanzania.
 
Back
Top Bottom