Msemaji Mkuu wa Serikali Thobias Makoba amesema zoezi la uokoaji kwenye eneo la ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo mkoani Dar es Salaam limemalizika.
Akizungumza na waandishi wa habari Makoba amesema hatua zinazofuata baada ya kukamilika kwa zoezi hilo ni kukaa na wafanyabiashara wa jengo hilo lililoporomoka na kuchambu mali ambazo zipo.
"Naomba nitangaze kwamba tumemaliza zoezi la uokoaji na tumefika level ya chini kabisa kwenye basement ambapo kuna watu walikuwa wamenasa." amesema Makoba.
Sahihi angesema zoezi la kutoa watu walioangukiwa na jengo so wasikilizaji watajiongeza kama walitoka wafu au wakiwa hai siyo kusema uokoaji huwezi kusema unaokoa mtu aliyekaa chini ya kifusi kwa siku 8 tena Tanzania nchi iliyojaa stress za kila namna.