Mkuu,
Kwa yale tuliyoyaona, hakuna mahali kwenye miongozo ya Bodi Ya Mikopo Tanzania imeelekeza kuwa mtu anayeomba mkopo lazima awe na admission number ya chuo kikuu
Bodi imeweka wazi kuwa wale watakao kuwa allocated loans ni wale ambao watapata nafasi katika vyuo vikuu. Tafsiri ni kwamba hutawekewa hela ya mkopo kama hutapata nafasi ya kujiunga chuo kikuu kinacho tambulika nchini.
Wewe omba mkopo, kama jinsi ulivyoomba nafasi za vyuo na round ya kwanza kupita. Mwisho wa dirisha la Maombi ya Bodi ya Mikopo ni tarehe 30.08.2024 ilhali vyuo vingi vitaanza kutoa majibu mwanzoni mwa mwezi wa tisa.
Nadhani umeelewa.