Uombaji wa Ruzuku Pasi na Kutangazwa Wito wa Uwasilishaji wa Michanganuo ya Miradi (Proactive Grant seeking)

Uombaji wa Ruzuku Pasi na Kutangazwa Wito wa Uwasilishaji wa Michanganuo ya Miradi (Proactive Grant seeking)

Joined
Jun 21, 2021
Posts
6
Reaction score
12
1629255939434.png

Kuna aina mbili za uombaji wa fedha ama ruzuku kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi; aina ya kwanza ni kuomba ruzuku baada ya kutangazwa wito wa kuwasilisha michanganuo ya miradi (hii tunaita "Reactive Grant seeking") aina ya pili ni uombaji wa ruzuku pasina kutangazwa wito wa uwasilishaji wa michanganuo ya miradi, ambayo hujulikana "proactive grant seeking" ambayo ndio msingi/maudhui ya andiko hili.
Kabla ya kuomba ruzuku kwa njia hii, muombaji anapaswa kuzingatia yafuatayo;
  • Mwenendo wa utoaji wa mfadhili husika (giving pattern)
  • Uhusiano uliopo kati ya lengo la Asasi yako (mission) na lengo la Mfadhili. Kwa mfano huwezi kumfata mfadhili ili umuombe ruzuku ya mradi wa kutetea haki za wanawake katika ushiriki wa utoaji wa maamuzi, halikuwa yeye (mfadhili) amejipambanua na kujikita katika eneo la uhifadhi wa mazingira.
Namna Taasisi za Ufadhili Zinavyofanya kazi (How Foundations Do Business)
Aina ya uendeshaji na miundo ya Taasisi za Ufadhili kwa kiasi kikubwa inatokana na; kiasi cha mali kinachomilikiwa na Taasisi husika (asset ownership), muundo wa uongozi (governance structure) na eneo/maeneo ya utekelezaji (focus areas). Asilimia kubwa ya Taasisi za Ufadhili (funding organizations) zina utaratibu wa kutoa miongozo ya uombaji wa ruzuku. Miongozo hii huaininsha eneo/maeneo ambayo Taasisi ya Ufadhili inajikita, kwa mfano yaweza kuwa; Utawala Bora, Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Makundi Maalum, Kutetea Haki za Watu Wenye Ulemavu n.k. na Taasisi hizi huwa na utaratibu wa kuchagua baadhi ya Asasi (pre-selection) na kuzipatia ruzuku. (Kumbuka kwamba; hapa Wito wa Uwasilishaji wa Miradi hautolewi "they do not issue Call for Proposals) Kwa maana hiyo ni kwamba Asasi ambayo inahitaji kuomba fedha kwa Taasisi za namna (in a proactive manner) inapaswa itafute au iombe muongozo wa utoaji wa ufadhili, kisha waandae mchanganuo wa Mradi kwa kufuata muongozo huo. Miongoni mwa Taasisi zenye utaratibu huu ni ABILIS (Hii ni Taasisi ya Ufadhili iliyoko Finland, ambayo inatoa ufadhili kwa asasi za watu wenye ulemavu) zingine ni "Corporate Foundations" kama Vodacom Foundation, Mo Foundation na nyinginezo.

AINA ZA TAASISI ZA UFADHILI
Kuna aina kuu mbili ya Taasisi za Ufadhili, ambazo muombaji wa ruzuku kwa nja ya "proactive" anapaswa kuzizingatia, Taasisi hizo ni;
  1. Taasisi za Ufadhili Binafsi (Private Foundations). Katika kundi hili kuna Tasasisi za Kifamilia (Family Foundations), Programu za utoaji za makampuni ya kibiashara (Corporate Giving Programs), Taasisi ambazo kiasi kikubwa cha mali zao hutumika kuendeshea shughuli zao kama utafiti n.k (Operating Foundations) Taasisi zilizoanzishwa na Makampuni ya kibiashara (Corporate Foundations)
  2. Taasisi za Ufadhili za umma (Grant making public charities). Katika kundi hili kuna Taasisi za Kijamiii (Community Foundations), pia kuna programu za utoaji kwaajili ya maendeleo ya umma; mfano fedha zinazotengwa na halimashauri kwa ajili ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Kundi la kwanza kwa maana ya "Private Foundations" ndio lenye kujumuisha Taasisi nyingi ulimwenguni; kwa asilimia 89. Idadi kubwa ya hizi Taaaisi ziko Ulaya na Marekani, ambapo sheria zao zinazitaka Taasisi hizi kila mwaka kuchaangia asilimia 5 ya mali zao (assets) kupitia utoaji wa ruzuku (grant making). Inapotokea uwekezaji katika "assets" umeshuka kifaida, basi na kiasi cha ruzuku watakachotoa katika mwaka husika kitashuka, tofauti na hivyo kiasi cha ruzuku kitabaki vile vile au kitapanda.

MBINU ZA KUTUMIA KATIKA UTAFUTAJI WA RUZUKU KWA NJIA YA "PROACTIVE"
Kwa Asasi ambayo inaamua kutumia njia hii ili kutafuta ruzuku kwa ajili ya kutekeleza Mradi, inapaswa kuzingatia mbinu zifuatazo;
  • Utafutaji wa Taarifa za Taasisi za Ufadhili (Foundations Search)
  • Kusoma muongozo wa utoaji wa ufadhili/ruzuku (reading grantmaking guidelines)
  • Hakikisha unatafuta mawasiliano ya afisa wa ruzuku au meneja wa programu (Grant Officer/Program Manager)
  • Anzisha mazungumzo juu ya azima ya Taasisi yako kuomba ruzuku na aina ya mradi ambao unahitaji ufadhili
  • Mara nyingi baada ya mazungumzo, utatakiwa kupeleka "Letter of Inquiry" kabla ya kuwasilisha mradi kamili. "Letter of Inquiry" ni maelezo juu ya wazo la Mradi ambao unataka kufanya
  • "Letter of Inquiry" yako ikikubalika; basi utatakiwa kuwasilisha andiko kamili la Mradi

Ahsante
 
Back
Top Bottom