Finder boy
JF-Expert Member
- Jan 20, 2012
- 608
- 150
kwanza naomba radhi kwa wale wote ambao kwa namna moja au nyingine nitawakera. Mimi ni mhitimu wa kidato cha sita 2013, naishi kijijini, yaani hakuna umeme, maji na hata mitandao ya simu hakuna isipokuwa airtel peke yake ndo tunaipata huku. Kwa wenyeji wa mkoa wa SIMIYU wilaya ya BUSEGA nipo kijiji kiitwacho 'MWAMUJULIRA'. Hivyo kwa yeyote aliye mjini na ambaye anajua utaratibu wa kuomba chuo na mkopo anijulishe. Nasikia pia kuna kitu kinaitwa guidebook ambacho kwangu ni msamiati(japo najua maana yake kwa kiswahili). Ivyo pia naomba anayejua yaliyomo kwenye guidebook iyo ya tcu anijulishe. Asanteni!